Kwa Walimu Wote, Bara na Visiwani.

tinkanyarwele

JF-Expert Member
Dec 30, 2016
2,017
1,940
Salaam, Leo imesikika kuwa hakimu amemhukumu kunyongwa hadi kufa Mwl, aliyetoa adhabu hadi kupelekea mauti ya mwanafunzi wake. Naamini kila mzazi au mlezi au mwalimu hakupendezwa na kifo cha mtoto baada ya kuadhibiwa na mwalimu, lakini naamini kwa mwalimu yeyote aliyesikia Hukumu hii lazima ametafakari kwa undani juu ya hatima yake katika kazi yake. Binafsi napenda kuwashauri WALIMU ACHANA na watoto wa watu, nashauri mwalimu abakize kazi moja tu ya KUFUNDISHA NA KUELEKEZA. Nahisi wakati umefika wa mwalimu kuachana na kutoa adhabu kwa watoto hasa adhabu zinazo gusa mwili moja kwa moja, hakuna anayependa mtoto alelewe hovyo lakini kwakuwa Nafsi ya MTU ni TAMU ni vyema kabisa mwalimu apoteze kazi siku ukibainika umeshindwa kuwalea vizuri wanafunzi kuliko kupoteza UHAI wako Kisa tu ulikuwa unamjenga mtoto wa MTU. Acha wafeli, acha wawe majambazi, acha wawe na nidhamu mbovu, acha wabebe mimba nk lakini msitoe adhabu ambazo zinaweza kupelekea matatizo makubwa kama kuuwaumiza watoto kiasi cha kuleta Ulemavu, Matatizo ya kisaikolojia na pengine kuleta Vifo. Nimeyaandika Haya kwani naamini mwalimu ni mlezi, mlezi hawezi kutoa adhabu akiwa amelenga kumdhuru mtoto, lakini hakuna ajue kilicho mbele yake , unaweza kumgusa mtoto kumbe huo ndo ulikuwa mwisho wake, hatimaye unaishia kwenye mikono ya kitanzi, jera nk. Haya mambo yanaumiza sana, hakuna mzazi anayependa kumpoteza mtoto wake vivyo hivyo hakuna mwalimu anapenda kupoteza maisha yake au kazi yake. Walimu nawaomba na kuwasihi, jitafakari upya na kama itawezekana hata nchi nzima huo uwe mfumo na utaratibu, kama mwanafunzi atakuudhi kupindukia basi omba ruhusa rudi nyumbani kalale. Usiogope, wakifeli hutakosa la kujieleza, wakikufukuza kazi rudi kwenu shika jembe kalime maisha si lazima upate msahara wengi hatuna mishahara na tunaishi. Poleni walimu, poleni wazazi, poleni wadau wa elimu na poleni walimu.
 
Mkuu hebu mlete mwanao nimfundishe hesabu hapa na akikosea nimpe kipigo kama cha yule marehemu huku ukishuhudia,bila shaka utaelewa ni nini mahakama inajaribu kukizuia.
Kukosa maadili ya kazi kwa mwanaume mmoja wa miaka 50 kumezima ndoto za yatima wa miaka 13 ambaye alishapata malaika wa kuyaokoa maisha yake,then ulitegemea serikali ilichukulie simple?hili ni tukio la ngapi la aina hii ndani ya miaka 10 iliyopita?unaelewa kazi ya mahakama katika jamii?unajua wajibu wa kwanza wa serikali kwa raia wake ni upi?
Kuna vitu hupaswi kuvitetea,naamini wapo walimu timamu ambao wanaweza kukemea walimu wenzao wa aina yako,unaaibisha fani mkuu.
Suala ni nguvu inayotumika kupiga watoto mpaka unaua.Mahakama imejiridhisha kuna nguvu kubwa ilitumika
Pili,ualimu mmefundishwa saikolojia,hivyo kumuadhibu mtoto ukiwa na hasira usiyoweza kuidhibiti kwa fani yenu ni ukosefu wa maadili ya kazi.Ni sawa na askari polisi kuua mtuhumiwa anayemtukana matusi,mie raia wa kitaa inaweza kuwa excuse ya kupunguza adhabu (provocation) lakini sio wewe professional unayesimamia maadili ya jamii uliyefundishwa kucounter changamoto hizo
 
wanafunzi wengine wanaudhi walimu sana. bora kubeba vitabu na kwenda darasa jingine na kuwaacha na utovu wao wa nidhamu. Ni ngumu kufukuza wanafunzi shule kama wahuni na wavuta bangi.
 
Utaratibu ni huu....
tapatalk_1551868204801.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
sheria ya viboko, ipo, inaeleweka.
Huyo mwalimu wa nidhamu sifa zake zimemponza, kwanza hana hata ruhusa ya kumshikia mwanafunzi kiboko sasa ilikuwaje awe na kihelehele? kama sio kutaka tu sifa na hivi mkoba ulikuwa wa mwalimi ya kike ndio basi akaona pa kukusanyia point hapo!!

Pole yake.
Hasira harasa.
Ila pole zaidi ya familia yake na waliokuwa wanamtegemea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wanafunzi wengine wanaudhi walimu sana. bora kubeba vitabu na kwenda darasa jingine na kuwaacha na utovu wao wa nidhamu. Ni ngumu kufukuza wanafunzi shule kama wahuni na wavuta bangi.
NA WALIMU WENGINE NI WA HOVYO SANA NI WATESAJI HAWANA HURUMA HAWAJUI ("KUPIGA SIO KUFUNZA"Na NZURI PESA 2019)
 
wanafunzi wengine wanaudhi walimu sana. bora kubeba vitabu na kwenda darasa jingine na kuwaacha na utovu wao wa nidhamu. Ni ngumu kufukuza wanafunzi shule kama wahuni na wavuta bangi.
MUACHE KU DISPLACE STRESS ZENU KWA WANAFUNZI
 
Tukishatoka vyuoni tunasahau mambo yote tuliyofundishwa jinsi ya kuishi na wanafunzi
Kiukweli wanafunzi wana maudhi sana maana wapo wa tabia tofauti kabisa kwa hiyo inatakiwa tuishi kulingana na tabia zao maana kuna wengine utafanikiwa kuwabadilisha kutoka mwenendo mbaya na kuwa wazuri kinidhamu na kuna wengine wanashindikana kitabia hilo lipo sana hasa katika shule zetu za umma/serikali.

Kama mwalimu ninasisitiza utoaji wa adhabu uwe ktk mazingira aidha kufanya usafi wa darasa au kupalilia maua muda ambao usio wa vipindi

Mimi nilishawahi kupandwa na hasira mwanafunzi alinikera sana darasani mpaka hamu ya kufundisha iliniisha ila niliondoka darasani nikamuambia unifuate muda wa mapumziko
Aliponifuata hasira yangu ilikua imeshukua nikamuonea huruma nikamwambia jitahidi ujikomboe ktk ujinga kuliko kushindana na ujinga kufanya ujinga utakua mjinga.
 
Wapo walimu wasio na muono mbali kama umemchapa mwanafunzi viboko vikaisha ukaamua kuchukua kuni huku walimu wenzako wakikusihi uache bado unawapuuza na kuendelea kupiga mithili ya nyoka! Mtoto akazimia na alipoamka akaendelea kumpiga! Alafu mwisho wa yote kumbe hakuwa na hatia ya kuiba hicho kilichomfanya ampage!Hapana hii haija kaa sawa nia ovu ilikuwepo tu tofauti na mwilimu anayechapa viboko idadi kadhaa kwa mtoto ambaye imethibitika ana kosa.Walimu wenye uelewa na maono watatumia elimu yao kukabiliana na watoto watukutu.Ushauri walimu wa ngazi zote wajitahidi kujirizisha bila kuacha shaka yoyote kwamba mtoto huyu amefanya kosa kwa maksudi bila halali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom