mtafuta-maisha
JF-Expert Member
- Nov 5, 2016
- 1,982
- 2,934
Katika squel ya movies ambayo uwa siichoki kuitazama ni hii Bourne.
Toka nitazame The Bourne Identity 2002, ikaja The Bourne Supremacy 2004, ikaja The Bourne Ultimatum 2007 hizo zote zimechezwa na Matt Demon huku director akiwa Paul Green Grass.
The Bourne Legacy ya mwaka 2012 Matt Demon aligoma kucheza kwenye hii movie kwakuwa Paul Green hakuwa ndiye director hivyo ikawabidi watafte mtu mwingine. Hii sikuipenda sana kama alizocheza Matt Demon
Kuna Jason Bourne 2016 ambapo Matt Demon alirudi kuicheza hii.
Movie hizi zimechezwa kutokana na novel za Van Lisbader zijulikanazo Jason Bourne ila kuna mabadirika makubwa kwenye story ya movie ni vitu vichache vinafanana na story za novel hizo japo majina ya movie yanakuwa sawa na mtiririko wa hizo novel.
Ambaye hajatazama hizi movie azitafute ni tamu sana.
Kwenye The Bourne Supremacy kuna hii conversation
Tom Cronin: He's making his first mistake.
Nicky: It's not a mistake. They don't make mistakes. They don't do random. There's always an objective. Always a target.
Pamela Landy: The objectives and targets always came from us. Who's giving them to him now?
Nicky: Scary version? He is.
Hapo ilikuwa anatafutwa Jason Bourne na mara passport yake inayofahamika ika ring kuwa kaingia Italy na kakamatwa na polisi wa Italy. Sasa huyo Tom hakuwa anamjua Bourne ndipo anadai ameanza kufanya makosa.
Huyo Nicky anamfahamu Bourne ndiyo anawambia kuwa hawezi kuwa kafanya makosa, na uwa watu wa aina yake hawafanyi vitu ovyo ovyo bila sababu, hivyo hiyo passport lazima kaitumia makusudi tu ili akamatwe.