Wisest man
JF-Expert Member
- Jul 29, 2013
- 993
- 333
Si vibaya kuomba ama kupewa ushauri na mtu humu jukwani, ninachotaka kusema ni kuhusu aina ya ushauri unaoupata! humu jukwaani kuna watu ambao ambao wanaweza kukupa ushauri bila ya wawe kumuelewa kwa undani ni mtu wa namna gani na analichukuliaje tatizo ambalo unahitaji ushauri wa kulitatua, nimesema hivi kwa sababu nilikuwa sehemu fulani nikakuta watu wnajadili mada fulani hapa jf, nikaingia moja kwa moja jf nkaikuta hiyo thread na nikakuta comment ya jamaa mmoja ambaye ni mmoja wao, hao jamaa walikuwa wamelewa vibaya sana hadi anatukana,cha kushangaza alicho-comment kikawa kinafurahiwa jukwaani! nkaishia kujiuliza tu! Muwe makini kwa kuchuja ushauri mnaopewa, isije kuwa mzee wa miaka 50 anachukua ushauri wa mtoto wa miaka 13 na kuufanyia kazi mwisho anaishia kupata majanga tu! humu jf kuna watu wa aina tofauti wapo maprofesa,madaktarri,walimu,wapiga debe,makahaba,vibaka,wapelelezi,walevi,hadi watoto wa chekechea! cha msingi ukipewa ushauri wewe changanya na zako.
Nawasilisha.
Nawasilisha.