Kwa wale waliowahi kutoa mahari halafu wakatamani/wakaingia mitini

kosa lako la kwanza ni kutoa mahari kabla hujajiridhisha......ulitoa kwa kushurutishwa....kosa kubwa sana hilo.....amekwambia anataka ndoa tuu....ili jamii inayomzunguka wajue ana ndoa.....na sio maisha ya ndoa.....miaka 5 yote unatafuta nini kwake...wachunguza nini??? kosa pia hili......nyie wote ni vijana damu inachemka....but mmoja kwenye gas na mwingine kwa umeme.....hamuwezi fika salama huko mbele.....dai mahari ni haki yako........hujapoteza kitu....si ushamkula....
mahari sitadai, ila nitawaeleza kuhusu ishu nzima. Ila wakiamua kunirudishia nitaipokea
 
Haitakiw kuchukua muda mrefu Sana kwenye uchumba hayo ndo madhara yake kwa Sasa atafute Aman ya moyo wake unataka Nn
Ukisema hivyo unakosea, huwezi kuoa bila ya kumfahamu vizuri mwenza wako, kikubwa ni uaminifu tu katika mahusiano.
 
achana na mahari, anza maisha mengine hilo bomu mkuu, mi binafsi nilisamehe mahali tatu...na nikaja muoa ambaye mahali nililipa msahafu tu...au ungapenda fahamu kwanini nilisamehe hizo mahari?
Tujuze huo ushujaa
 
Kwanza pole sana;

Pili unapotaka kuo mwanamke isipokuwa kwa sababu za kiufundi usikae nae katika uhusiano kwa muda mrefu sana.Sababu za kiufundi ni kama vile masomo,umbali,muda mchache wa kuonana na vitu kama hivyo.Pili kama mwanaume unatakiwa uhakikishe kuwa unapoamua kumuoa binti basi uwe una taarifa kamili na cha muhimu sio mahari,wala ndoa ya kikiristu wala hizo mambo za spy app.Cha muhimu ni utayari wa huyo binti pamoja na wewe kukaa pamoja na kuyajenga.

Mimi binafsi napenda zaidi kufanya test drive,yaani kama mwanamke anataka ndoa na mimi basi anakuja tunaishi tunatibuana tunajuana kisha katikati hapo nikiona ulazima basi natangaza ndoa tunalipa mahai pamoja na faini.Mwanamke akiniletea habari za ooh uzinzi oo ndoa kwanza ooo sijui vijikanuni vingi basi ujue huyo hakufai.Wanawake ambao wanamasharti mengi kwako basi ujue hawajafall vizuri yani inshort ni kwamba haqjakupenda vizuri ndo maana anaweza kukupa masharti.

Sasa ndugu umeshalipa mahari,kwa mila za kwetu huyo sasa ni mkeo,kwa kuwa umeona hizo tabia za ajabu kwanza mchane live ajue unajua kisha mwambie sasa hufungi ndoa ya shela na kahaba na kwamba inabidi aje kwako muyajenge,ukae nae umle mpaka akuzalie mtoto mmoja ukiona kama anafaa bado basi nenda naye altareni ukiona bado hajawa na utulivu basi utajua cha kufanya.Ili NAKUONYA USIENDE MADHABAHUNI NA MTU AMBAYE HUMUAMINI
mkuu agiza konyag ntalipa
 
Mimi nimepita kujifunza tu mkuu .

Ila lazima nikuambie kitu,, Therenis no excuse in cheating !!

Achana naye ,piga chini ,tena usikae kimya hapa ndo mnakoseaga , weee mwambie ukweli juu ya madudu yake basi ,alafu unakaa kimya... Kama atajutiaa sanaa waweza msamehe km utaona anachukulia kawaida Achana naye..... Huyo keshakuonyesha ye nimwanamke wa aina gan, nakwasababu anaitafuta ndoa kinaga ubaga ,,,take from me KWASASA WAOAJI NI MMOJA OUT OF 10 kwaiyo hao wawili wanasafisha rungu tuu kisha wamuache.


Hapa ndipo Mima white cute upekee wako ulipo, uyu mwanamke kwanza wivu wake alafu anatumia mbinu yoyote anayoweza kuhakikisha kwamba unakaa bila hofu juu yake.

Ubarikiwe sana Mima.
Na kwa nn
Kuwekana.roho juu
 
Yani ndugu, kuna mengi sana kanifanyia sijayaweka hapa ili nisije nikaonekana ni mpumbavu sana, nimempa second chance mara nyingi sana, but hadi sasa nisha give up
km ndo hvo mkuu jitoe kwenye mtandao mapema af wanawake wengi wachepukaji huwa hawatumii kondom
 
huu ni moja ya mahari niliyosamehe

nilifahamiana na huyo binti ki mazabe tuu, lakini kwa bahati nzuri tukaelewana, na yeye alinielewa zaidi akaingia mapenzini mazima, nami nikampokea jao tayari kuna mahari mbili nilishazisamehe kabla yake, hivyo nikawa nimekubali kuwa nae ili niangalie mapungufu yake kama nitayaweza basi tuyaaendeleze maisha tukiwa pamoja.

historia ya huyo mwanamke, kwao wao vizuri tu, familia yao inajiweza, mimi nikiwa na maisha ya kuunga unga, maisha ya kutumia akili nyingi kila siku, hapo nilikuwa nikisoma chuo, huku nikiwa dereva wa magari makubwa ia nikiwa fundi wa fani kama nne tofauti, kote nipo, na namudu kula, kuvaa na kufanya mambo yangu yaonekana fresh kwa wengine jao mi sikuwa fresh kiivyo, siri ya mtungi aijuaye kata..sasa huyu dem alikuwa akifanya kazi bandari kavu moja hivi, mimi niko D.I.T, pia niko barabarani, huyo manzi tukayajenga, na baada ya muda wa kama miezi miwili hivi, akaomba nikajitambulishe kwao, nikafanya hivyo, alinitambulisha kama rafiki yake tu, lakini mama yake alitokea kunielewa sana, na alipouliza kuhusu, familia yangu, elimu yangu na maisha nayaonaje nikafunguka ninavyojua mimi..haikupita wiki mbili yule dada akaniambia anataka kuhama kwao, nami nihame kwangu, tutafute nyumba kubwa tuishi pamoja, nilipinga mwanzo, lakini yeye alilazimisha kuhama, tukatafuta nyumba upande maeneo ya kigogo, chumba changu kule nilikokuwa nikikaa awali sikukirudisha niliendelea kukilipia kama kawaida, mapenzi yakawa mubashara kweli, ananiheshimu, ananisikiliza, ananishauri mambo mengi ya maendeleo, sasa nikawa namchunguza kwa makini sababu nilisha vunja ndoa mbili mbele yake sababu ni tabia tu za hao waliotangulia, kuna jambo nikagundua kuhusu huyu msichana...ni mlevi, sio mnywaji ni mlevi lakini tangu awe na mimi akawa kaificha ile tabia, sasa kuna siku nikamtoa yeye na rafiki zake wawili, wao china kwa sasa, hiyo siku hao watu watatu walikunywa kreti mbili...nikaona sasa nimeingia kwenye anga za Ninja..maisha yakawa yanaenda fresh tu, lakini familia yangu haikuenda yale mahusiano yetu, mara nyingi nilikuwa naambiwa wao watoto wa ndugu wengi tu wa kuwastiri, wakiwa na maana ya mabinamu, nilikataa sababu hawa mabinamu wote nilikuwa nishafanya yangu na nawajua kuliko wazazi wao, wanavyowafahamu watoto zao kwa mwonekano wa nje.,

siku moja mama wa yule dada aliniita, hapo nikiwa nishaenda kutoa mahari na nakumbuka ilikuwa ni kama m1 na laki nne hivi, nikawa na deni la laki tatu, yule mama aliniuliza swali moja ambalo si sitakaa nilisahau, aliniambia mwanangu, ni kweli unampenda mtoto wangu? pamoja na mapungufu yake? nikauliza mapungufu kama yepi mama? akaniambia usijifanye huyajui baba, najua wafahamu, nikamuuliza ni pombe? akanijibu ndio, binti yangu nampenda sana, lakini tabia yake ya unywaji wa pombe inanitia sononi sana, nahisi mtashindwana, miezi sita hii amekuwa mwema ametulia, ananawili tofauti na alivyokuwa hapa nyumbani, sasa baba ukiweza kumbadilisha huyu binti, mimi nitakupa maisha mwanangu, nitakupa nyumba na pesa ufanye kitu unachoona kitasaidia kufanya mzidi kuishi kwa amani na furaha, ufanye biashara..nilifurahi sana, ila akaniambia, kijana unaonekana ni mwema sana, pia kama utashindwana na binti yangu, sijui kama kuna mwanaume mwingine atamuweza, na ukishindwana nae, ama akikukorofisha kwa lolote naomba uniambie mapema, kama atatokea msichana ukampenda kuliko unavyompenda mwanangu njoo, mimi nitakulipia mahari na nitaisimamia ndoa hiyo..
nilishangaa sana huyu mama mpaka anasema hivi ina maana huyu binti ni Ninja kunizidi?
nikamwambia mama huyu hanishindi usijali..nikaondoka, na bahati mbaya ilikuwa upande wangu yule mama jioni yake akapata presha ya ghafla akafariki njiani tukimpeleka hospital..picha likaanzia hapo....ntarudi
rudi fasta mkuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom