Kwa wale waliowahi kutoa mahari halafu wakatamani/wakaingia mitini

Habari wana jf, hususani great thinkers, kuna mwenzetu anaomba ushauri, mimi nitasimama kwa niaba yake kuna jambo linamtatiza sana , pia naomba samahani kwa uzi huu mrefu, ila usisite kuusoma wote,

NOTE
Ili umshauri vizuri soma uzi wote

ILIPOANZIA
Ni hivi, nipo kwenye mahusiano na mwanamke kwa miaka takribani 5 sasa, mwanzoni 2013 nilivyoanza nae mahusiano alikuwa ni binti muelewa sana naweza sema wife material.

Tangu tunaanza muda mwingi wa mahusiano alikuwa ananisisitiza sana nimuoe hadi wakati mwingine nikawa naona kero.

Kwa kweli mimi nilikuwa nina nia ya kumuoa na sikuwahi kumuonesha tabia zozote zinazoashiria ukosefu/uvunjifu wa uaminifu, ila sikuwa tayari kwa wakati ule maana sikuwa nmejipanga, ila nilikuwa namsisitiza tu kuwa awe na imani nami, nitamuoa

Lakini pia, akinibana sana kuhusu kumuoa nikawa napata hasira namuuliza "kwa nini una haraka sana ya ndoa?" . Majibu yake kwa kweli hayakuwa yananipa hamasa, maana alikuwa anajibu kuwa nimuoe kwa kuwa

1) wakati wake anaona umefika/ ana kiu ya kuwa na mume

2)umri wake umeenda( she is 28 now)

3)Rafiki zake wote aliosoma nao washaolewa hivyo nae anatamani ndoa
4) Hataki uzinzi, hivyo bora aolewe

Kwa kweli nilikuwa nachoka majibu hayo, nilitamani anijibu

" Napenda tufunge ndoa ili tupate nafasi ya kujenga familia iliyo bora na tupange malengo yetu vizuri kwani tutakuwa mwili mmoja"
au angenijibu kwa namna yoyote ile kuonesha kuwa yeye ni great thinker

Hali ya kunihamasisha ndoa iliendelea sana, yani hata mkiwa pamoja mnapiga stori, lazima atazungumzia ndoa. Yaani alikuwa ananihamasisha sana, hadi kuna kipindi kinachohusu ndoa kinarushwa na tbc kila j2 saa 1 usiku alikuwa ananilazimisha nikitazame.....

CHEMBE CHEMBE ZA USALITI
By 2005, niliwahi kuzifuma sms za kimapenzi za mwanaume mwingine, nikambana sana kwa nini anawasiliana na mwanaume mwingine wakati ana mahusiano nami, huku akilia kwa uchungu, aliniambia,

" amefanya vile kwa kuwa anaona ntakuja kumuacha maana mahusiano yetu hayana security(ndoa), hivyo anatafuta mwanaume mwingine ili amuoe" . Kiasi fulani nilimuelewa, nikaona bora nimsamehe , na nikamuahidi mwaka 2016 ntapeleka mahari kwao then ndoa ya kikristu

NATOA MAHARI
Mwaka uliofuata 2016 dec, nilienda kwao (niliambatana na ndugu+mshenga) ,
Kwa kuwa tulikuwa tunatoka mbali tuliwaomba watutajie mahitaji yote yanayotakiwa kulipwa kwani tunataka tumalize kila kitu pale pale (posa na mahari), Mimi nilibeba fedha taslimu Milioni 2

Orodha ya vitu tuliyopangiwa ilikuwa kubwa sana kwa kweli, jumla gharama ilikuwa m 5, . Kwa kuwa kuna msemo " mahari huwa haiishi" niliwaomba tulipe m 2 nilizobeba afu waturuhusu tuendelee na process za ndoa. Walizichukua zile m 2 ila wakasema hawatoi kibali cha ndoa hadi nipunguze tena mahari .
Kwa kweli mimi sikujisikia vizuri niliwajibu naomba nikazitafute hizo hela, nikizipata nitazileta.
Tulirudi nikiwa sina furaha kwa kweli, lakini sikuwa na jinsi.

Nilirudi kuzisaka hizo pesa but kwa morali ndogo, pia katika kipindi hiki yule msichana wangu akaanza kubadilika taratibu (ngozi yake halisi), nadhani alifikiri kwa kuwa nishaenda kwao hakuna tatizo tena.
Maana alianza kuwa mlalamikaji, mgomvi, matusi, mkali nk.

Kuna kipindi nikawa na mawazo sana, nishatoa sehemu ya mahari afu mchumba haeleweki! vp......
Pia kule ukweni walivyoona kimya sana(takriban mwaka) wakampigia simu mshenga wangu, kuulza mliahidi mtarudi mbona kimya!! mimi nikamwambia awajibu " yule kijana(yaan mm) bado anatafuta hizo pesa na kwa sasa hana kazi kasimamishwa!
Walituambia twende hivyo hivyo hakuna tatizo....kwa kweli niliagiza baadhi ya ndugu waende na kiasi fulani cha pesa, wakapokelewa vizuri na wakatuambia tuwatajie tarehe ya harusi ili nao wajiandae(sendoff)


SASA
Kwa kweli, sijawatajia hiyo tarehe baada ya kugundua madudu yake(majuzi hivi kuna akili iliniambia ni install spy app kwenye simu yake, yaani nilichoka kabisa!!!! kumbe ana mabwana wawili apart from me, texts na calls zao zote nimeziona na kuzisikia kwa masikio yangu)

Kweli wanakuambia spy at your own risk, nimevurugwa sana na hapa nafikiria niachane na huyu mwanamke na ni give up hiyo mahari, maana sijamuoa bado je nikimuoa si atanisumbua huyu!!!!!! ,

NAHITAJI USHAURI
1.Kwa situation hii niliyokueleza, Je unanishauri nini??
2.Pia ningependa wale waliowahi kupata situation kama yangu, waniambie wao walisolve vipi? na ilikuaje kuaje ili nijifunze kutoka kwao
daa asee we ni pacha wangu
 
Mpe pole,lakini nafikiri anaweza kumpa second chance uyo msichana..huenda alijiengage na hao wanaume for security sababu aliona yeye(mwenye stori) haeleweki.

Wanawake wana iyo tabia sana ya kuseek security hasa wakiisi wataachwa..na icho kilanga cha kuinstall spy application sio mpango

Aongee nae amsikilize.l na yeye bibi harusi mtarajiwa anasemaje.
 
Kusema kweli Jambo lako ni ngumu sana
Napenda kukushauri kuwa sikiliza moyo wako unatakaje ila hakuna mwanamke mwaminifu kwa 100%
Kaa na mwenzako mwambie sababu zote hizi kisha umsikilize anasemaje hakika mapenzi kitovu cha Uzembe mahali ml 5
Wakati ningekuwa mimi nilishapata heka moja kule Bwama au mwanzo mgumu
Ila unaweza kisamehe pesa ni kitu chakutafutwa
Kikubwa ni amani ya moyo wako
 
Kwanza pole sana;

Pili unapotaka kuo mwanamke isipokuwa kwa sababu za kiufundi usikae nae katika uhusiano kwa muda mrefu sana.Sababu za kiufundi ni kama vile masomo,umbali,muda mchache wa kuonana na vitu kama hivyo.Pili kama mwanaume unatakiwa uhakikishe kuwa unapoamua kumuoa binti basi uwe una taarifa kamili na cha muhimu sio mahari,wala ndoa ya kikiristu wala hizo mambo za spy app.Cha muhimu ni utayari wa huyo binti pamoja na wewe kukaa pamoja na kuyajenga.

Mimi binafsi napenda zaidi kufanya test drive,yaani kama mwanamke anataka ndoa na mimi basi anakuja tunaishi tunatibuana tunajuana kisha katikati hapo nikiona ulazima basi natangaza ndoa tunalipa mahai pamoja na faini.Mwanamke akiniletea habari za ooh uzinzi oo ndoa kwanza ooo sijui vijikanuni vingi basi ujue huyo hakufai.Wanawake ambao wanamasharti mengi kwako basi ujue hawajafall vizuri yani inshort ni kwamba haqjakupenda vizuri ndo maana anaweza kukupa masharti.

Sasa ndugu umeshalipa mahari,kwa mila za kwetu huyo sasa ni mkeo,kwa kuwa umeona hizo tabia za ajabu kwanza mchane live ajue unajua kisha mwambie sasa hufungi ndoa ya shela na kahaba na kwamba inabidi aje kwako muyajenge,ukae nae umle mpaka akuzalie mtoto mmoja ukiona kama anafaa bado basi nenda naye altareni ukiona bado hajawa na utulivu basi utajua cha kufanya.Ili NAKUONYA USIENDE MADHABAHUNI NA MTU AMBAYE HUMUAMINI
 
Mpe pole,lakini nafikiri anaweza kumpa second chance uyo msichana..huenda alijiengage na hao wanaume for security sababu aliona yeye(mwenye stori) haeleweki.

Wanawake wana iyo tabia sana ya kuseek security hasa wakiisi wataachwa..na icho kilanga cha kuinstall spy application sio mpango

Aongee nae amsikilize.l na yeye bibi harusi mtarajiwa anasemaje.
yani, bado hajamuambia neno lolote ndio anajipanga amuambie madudu yake kwanza
 
Fanya maamuzi sahihi.kama roho yako inakataa kumuoa na ushaanza kugundua madudu yake na sio mwaminifu ni bora kumtema tu ukafanya mambo mengine hyo pesa uliyoipeleka kwao hisabia kama ni hasara tu kama hasara nyengine
Sawa mkuu, asante sana, nmekuelewa vzuri
 
Kusema kweli Jambo lako ni ngumu sana
Napenda kukushauri kuwa sikiliza moyo wako unatakaje ila hakuna mwanamke mwaminifu kwa 100%
Kaa na mwenzako mwambie sababu zote hizi kisha umsikilize anasemaje hakika mapenzi kitovu cha Uzembe mahali ml 5
Wakati ningekuwa mimi nilishapata heka moja kule Bwama au mwanzo mgumu
Ila unaweza kisamehe pesa ni kitu chakutafutwa
Kikubwa ni amani ya moyo wako
asante mkuu
 
Aiseee hlo n bom mwambie
Jamaa yako atupilie mbali hayo
Mahar waschana n wengi
Huyo na kibur chake aende
Kwa hao


Watakao muoa maana hayo.
Madharau anaonesha co poah
Kabsa kisa umetoa mahar

Nb: ngekua mm bhas nlishafanya
Maamuz magumu ktambo sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom