Another brain teaser: A water tank reservoir is connected to three water pipe supplies, pipes a, b and c. Pipe a alone can fill the tank in 30 minutes while pipe b can fill it in 45 minutes and pipe c alone can fill it in 90 minutes. How long will the reservoir tank fill up if all water pipes are opened to the tank at the same time.
Naomba nijibu hili swali katika namna ambayo hata yule ambaye hajui hesabu atatelewa.
BOMBA A lina uwezo wa kujaza TANK kwa muda wa dakika 30. Kwa hiyo lina uwezo wa kujaza 1/30 ya tank kwa muda wa dakika 1, na kwa maana hiyo basi:
BOMBA A litajza 1/30 ya TANK kwa muda wa dakika 1
BOMBA B litajza 1/45 ya TANK kwa muda wa dakika 1
BOMBA C litajza 1/90 ya TANK kwa muda wa dakika 1
Mabomba yote matatu yatajaza (1/30) + (1/45) + (1/90) = 1/15 kwa muda wa dakika 1! (
siyo dakika 3 tafadhali)
Kwa hiyo kama mabomba matatu yanaweza kujaza 1/15 ya TANK kwa muda wa dakika 1, then yana uwezo wa kujaza 15/15 ya TANK kwa muda wa dakika 1x15= dakika 15
Hivyo mabomba yote matatu yatajaza TANK hilo kwa muda wa dakika 15.
MUHIMU:
Hili swali limekaa katika mfumo wa applied/ business mathematics zaidi, yaani mahesabu ambayo yanatumiwa na watu katika shughuli za maisha za kila siku kama vile kwenye business. Na kama ni Chuo Kikuu, swali la mfumo wa namna hii anatkiwa aulizwe sana sana mtu anayesoma digrii kama vile ya Bachellor of Commerce au Engineering, na si mtu anayesoma let's say degree ya mahesabu perce. Hivyo unapofikia hatua ya kuli-solve kwa kutumia KDS na KKS (GCF and the like), unakuwa uko sahihi katika jibu, ila kwenye njia yako ya kufikia jawabu kidogo inakuwa ina mgogoro ukizingatia nature ya swali lenyewe.
Still, swali hili liko katika kiwango cha chini sana kuweza kuulizwa katika ngazi hizo nilizozitaja na nakumbuka kama wakati enzi hizo wakati sisi wazee tunasoma shule za msingi, maswali ya aina hii yalikuwa yanapatikana katika kitabu kimoja maarufu sana kilikuwa kinaenda kwa jina la:
JIANDAE VEMA KUMALIZA ELIMU YA SHULE YA MSINGI, manuscript iliyokuwa popular sana enzi hizo kwa wanafunzi wa shule za msingi na tulikuwa tunakatiza kwa kuiita
"JIANDAE". Ilikuwa ni enzi hizo miaka ya 1947 wakati tuku shule za msingi, enzi za mkoloni.