Kwa Wakristo: Si vibaya tukashare misa ya leo

Kwa Wakristo: Si vibaya tukashare misa ya leo

mimi nimeguswa na Injili ya leo "Angalieni msifanye wema wenu machoni pa watu ili mtazamwe nao......."
ukitaka kusali jifungie chumbani kwako uongee na baba yako wa Sirini atakusikia, siyo kupayuka ovyo....
Ukifunga siyo basi uso wote umepauka, kisa mfungo..... paka mafuta midomo yako, tembea unatabasamu.... Mungu wako atajua kwamba umefunga na atapokea sala zako.........
Tuwe na Kwaresma njema wapendwa...... tuba ya kweli ndo inayotakiwa

Ameen dada mkubwa.... Nimebarikiwa sana hapo kwenye blue!!!
 
Nilichojifunza ni kwamba, vingine vyote vinaweza subiri kesho lkn sio 'kuwa tayari kwa kurejea kwa muumba' maana hatujui siku wala sekunde.
 
i feel guilty sijasali...Bwana Yesu nisamehe bure. mwenye mabaki ya jivu anipake hapo kwenye avatar (just joking)....but seriously, i feel guilty..

Ha ha ha...vituko huwa havishi humu ndani..Mungu kesha kusamehe..
 
Kuhusu neno lishasemwa hapo

Kanisa lilikuwa na watu wengi na ilikuwa misa yA mchana,hii inaashiria self emplyed ni wengi au mabosi kazini ni waelewa wamerhusu ibada wakati wa kazi!nimependa hilo

Mwongo wewe Mass zilikuwa tatu asubuhi saa 7:00am,saa01:00pm na 5😛m

na watu lukuki acha hizo. Mkuu
 
Sisi kama Kondoo tumepotea, tumeenenda katika njia zetu wenyewe ("All we Like sheep, have gone astray....every one on his own way") Isaya 53.6

Ni kweli mkuu lakini ametuahidi kutuokoa kama ilivyoandikwa katika kitabu cha,

Waefeso 2:8-9
Kwa maana mmeokolewa kwa neema
kwa njia ya imani ambayo hiyo haikutokana
na nafsi zenu ni kipawa cha Mungu wala si
kwa matendo mtu awaye yote asije akajisifu....
 
Nilichojifunza ni kwamba, vingine vyote vinaweza subiri kesho lkn sio 'kuwa tayari kwa kurejea kwa muumba' maana hatujui siku wala sekunde.

:amen: :amen: Mpendwa Kaunga..... Na biblia inasisitiza hili katika kitabu cha..

Mathayo 24:42-44
"Kesheni basi kwa maana hajui ni siku gani
atakayokuja Bwana wenu lakini fahamuni
neno hili; kama mwenye nyumba angalijua
ile zamu mwivi atakayokuja angalikesha
asingeliacha nyumba yake kuvunjwa. Kwa
sababu hiyo ninyi nanyi jiwekeni tayari kwa
kuwa katika saa msiyo dhani mwana wa
Adamu yuaja.
 
Last edited by a moderator:
Hakika nimebarikiwa sana na huu uzi Mungu anisamehe sijahudhulia ila baada ya kufungua hapa nimebarikiwa sana, nafeel kama nipo kanisani.
 
Hakika nimebarikiwa sana na huu uzi Mungu anisamehe sijahudhulia ila baada ya kufungua hapa nimebarikiwa sana, nafeel kama nipo kanisani.

:amen: :amen: Mdada... Karibu!!!!!!!!
 
Kazi ya majivu ni kutakatisha na kung'arisha vitu, hivyo kupakwa majivu ni ishara ya kusafishwa dhambi zetu. Rangi ya kijivu ni mchanganyiko wa Rangi Nyeusi (dhambi) na Rangi Nyeupe (Toba), hivyo hiki ni kipindi cha kutubu dhambi zetu.
 
Mwenye Nyimbo za Kwaresma atupie hapa ili tuendelee kubarikiwa
 
Mwongo wewe Mass zilikuwa tatu asubuhi saa 7:00am,saa01:00pm na 5😛m

na watu lukuki acha hizo. Mkuu

sikumbuki mara ya mwisho kuitwa mwongo ilikuwa lini kwa sababu udanganyifu sio character yangu...anyway mimi niliingia misa ya mchana na nimeshare nilichojifunza ktk misa hiyo...kwamba japo ilikuwa mchana lakini watu walikuwa wengi na nikatoa ninazodhani ni sababu....uongo wangu upo wapi dada yangu????!!!!!
 
Mbona umegeneralize wakristo kana kwamba wote wanaamini mambo hayo?cc wengine misa na mambo ya majivu 2nayaona ni upagani na ushirikina wa Roma yaliyoasisiwa na Ibilisi.
 
Mbona umegeneralize wakristo kana kwamba wote wanaamini mambo hayo?cc wengine misa na mambo ya majivu 2nayaona ni upagani na ushirikina wa Roma yaliyoasisiwa na Ibilisi.
Then why did you have to put such a derogatorty comment? Mkristu "safi" kama wewe "usiyeasisiwa na ibilisi" huwezi kutoa comment kama hiyo dhidi ya Mkristo mwenzako
 
kiboko wa mahubiri ya jumatano ya majivu ni padri Dr mbiku wa UDSM, mnamkumbuka lakin? leo mie nimesali udsm full maupako na mistari ya biblia kibao...
 
Back
Top Bottom