Mkuu pongezi kwako, na MBONOTEC kama kampuni.Habari zenu wadau.Mwanzoni mwa mwaka huu nilianzisha uzi ulokuwa ukiongelea changamoto zinazotukabili wadau wa sekta ya kilimo (cha kisasa) na moja ya sababu nilizozieleza ilikuwa ni wataalamu wa kilimo wanaoweza kumshauri mkulima anaetaka kulima kibiashara kufikia ndoto zake. nilieleza pia kuwa tuliamua kuanzisha umoja wa vijana graduates wa kilimo ambao tuliamua kutoa huduma ya ushauri wa jinsi ya kulima kibiashara mazao yote yanayostawi katika ukanda wetu wa africa mashariki. tumekuwa tukitoa huduma hizo online kwa kuwasiliana na mteja wetu (mkulima) na kumjibu maswali yake na pia kwa kufika shambani na kutekeleza ushauri husika kwa vitendo. huduma hizo zililenga kuongeza ubora na wingi wa mazao kwa mkulima kwa kumpatia ushauri sahihi kuanzia uandaaji shamba, aina ya mbegu, matumizi ya madawa ya kudhibiti wadudu na magonjw, uvunaji na post harvest handling. pia kufanya cost analysis kabla ya kuingia katika uzalishaji na pia soil analysis ili kujua mahitaji halisi ya mbolea na aina ya mbolea katika shamba la mkulima. pia tumekua tukijishughulisha na uendeshaji wa mafunzo kwa vikundi vya wakulima na watu ambao wanataka kuingia katika kilimo cha kibiashara kama watu binafsi/NGO's na Makampuni mbali mbali. Ili kuweza kufanikisha haya kwa wigo mpana zaidi sasa tumekwisha sajili kampuni ambayo imejikita zaidi katika kutekeleza hayo kwa vitendo. wadau tunazidi kuwakaribishampate huduma zetu kupitia kampuni yetu ya MBONOTECHNOLOGIES (T) LTD. tutafanya kazi yako popote pale ulipo katika mipaka ya nchi hii ndani ya muda mfupi sana na kukupatia majibu sahihi. gharama zetu ni nafuu sana ila hutofautiana kutegemea shamba lako lilipo. ofisi zetu zipo moshi mjini pamoja na dakawa morogoro. kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana nasi kwa simu nambari 0653649152. usiku au mchana tutapokea simu yako na kukupatia majibu sahihi. Asante
Mkuu Hongera sana kwa hili, Ila mimi nitakuwa na Maswali Machache ya kuwauliza,
1. Mkuu kwenye shughuli mnazo fanya mmejaribu kuelezea matatizo ya wakulima katika vitu vifuatavyo
- Mbolea
- Udongo
- Mbegu
- Madawa
- Uvunaji na Uhifadhi
Mkuu labda Ungejaribu kuweka Maelezo kwa Ufupi kabisa, trend ya Kilimo cha Tanzani kiko vipi na kama hizo ndo factor kuu zinazo fanya wakulima wasipige hatua,
1. Mkuu mmeisha wahi kufanya tafiti na kugundua sababu kuu zinazo zorotesha kilimo?
2. Nyie bila shaka ni Graduate wa Sua au Chuo chochote kile cha kilimo, Je Mna mashamba yenu ya Kufanyia Demonstaration? au Mashamba Darasa?
3. Mmesema Mko Moshi, Ok kwa sasa Mkoa wa Kilimanjaro watu wameshindwa Kuvuna kabisa na Mkoa unakaribiwa na Njaa je sababu ni nini?
4. Na kwa Mkoa wa Arusha ni hivyo hivyo, kULE Karatu ambako ndo ilikuwa Kituo kikuu cha Mazao mambo yamebadilika je sababu ni zipi?
Kwa sababu ukijarubu kutembelea Mikoa Mingi ya Tanzania, unaweza Kuja na Jibu tofauti kabisa na Mnayo yaongea, Chukulia Mfano wa Mikoa inayo lima PAMBA kwa sasa watu wamekata tamaa ya kulima Pamba kabisa,
Mkuu, mmejikita zaidi katika Kilimo mazao tu, au hata Kilimo-Mifugo??????
Habari,
nahitaji kufanya soil test-- hii number nikipiga haiconnect, kama una number nyingine naomba, au hata email address itakuwa poa!