kwa wajasiriamali wa sekta ya kilimo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

kwa wajasiriamali wa sekta ya kilimo

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by JBAM, Sep 17, 2012.

 1. J

  JBAM Member

  #1
  Sep 17, 2012
  Joined: Feb 16, 2012
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari zenu wadau.Mwanzoni mwa mwaka huu nilianzisha uzi ulokuwa ukiongelea changamoto zinazotukabili wadau wa sekta ya kilimo (cha kisasa) na moja ya sababu nilizozieleza ilikuwa ni wataalamu wa kilimo wanaoweza kumshauri mkulima anaetaka kulima kibiashara kufikia ndoto zake. nilieleza pia kuwa tuliamua kuanzisha umoja wa vijana graduates wa kilimo ambao tuliamua kutoa huduma ya ushauri wa jinsi ya kulima kibiashara mazao yote yanayostawi katika ukanda wetu wa africa mashariki. tumekuwa tukitoa huduma hizo online kwa kuwasiliana na mteja wetu (mkulima) na kumjibu maswali yake na pia kwa kufika shambani na kutekeleza ushauri husika kwa vitendo. huduma hizo zililenga kuongeza ubora na wingi wa mazao kwa mkulima kwa kumpatia ushauri sahihi kuanzia uandaaji shamba, aina ya mbegu, matumizi ya madawa ya kudhibiti wadudu na magonjw, uvunaji na post harvest handling. pia kufanya cost analysis kabla ya kuingia katika uzalishaji na pia soil analysis ili kujua mahitaji halisi ya mbolea na aina ya mbolea katika shamba la mkulima. pia tumekua tukijishughulisha na uendeshaji wa mafunzo kwa vikundi vya wakulima na watu ambao wanataka kuingia katika kilimo cha kibiashara kama watu binafsi/NGO's na Makampuni mbali mbali. Ili kuweza kufanikisha haya kwa wigo mpana zaidi sasa tumekwisha sajili kampuni ambayo imejikita zaidi katika kutekeleza hayo kwa vitendo. wadau tunazidi kuwakaribishampate huduma zetu kupitia kampuni yetu ya MBONOTECHNOLOGIES (T) LTD. tutafanya kazi yako popote pale ulipo katika mipaka ya nchi hii ndani ya muda mfupi sana na kukupatia majibu sahihi. gharama zetu ni nafuu sana ila hutofautiana kutegemea shamba lako lilipo. ofisi zetu zipo moshi mjini pamoja na dakawa morogoro. kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana nasi kwa simu nambari 0653649152. usiku au mchana tutapokea simu yako na kukupatia majibu sahihi. Asante
   
 2. Mwanahisa

  Mwanahisa JF-Expert Member

  #2
  Sep 17, 2012
  Joined: Jun 29, 2012
  Messages: 1,397
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu pongezi kwako, na MBONOTEC kama kampuni.
  Labda ungefunguka zaidi aina za huduma za online na zile za kukutana moja kwa moja.
  Gharama pia ungeweka wazi kwani hii ni huduma kwa wote na mnahaki yakulipwa ujira kwa kazi yenu.
  Na je licha ya simu, Anuani ya barua pepe ya kampuni ipo au sanduku la barua?
  Mwanzo mzuri, ni hayo tu kwa sasa.
   
 3. Mangaline

  Mangaline JF-Expert Member

  #3
  Sep 17, 2012
  Joined: May 19, 2012
  Messages: 1,052
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mkuu, mmejikita zaidi katika Kilimo mazao tu, au hata Kilimo-Mifugo??????
   
 4. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #4
  Sep 17, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  Nataka kulima matikiti nina msingi wa mil2 nishauri nianzaje?
   
 5. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #5
  Sep 17, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,128
  Trophy Points: 280
  Mkuu Hongera sana kwa hili, Ila mimi nitakuwa na Maswali Machache ya kuwauliza,

  1. Mkuu kwenye shughuli mnazo fanya mmejaribu kuelezea matatizo ya wakulima katika vitu vifuatavyo

  - Mbolea
  - Udongo
  - Mbegu
  - Madawa
  - Uvunaji na Uhifadhi

  Mkuu labda Ungejaribu kuweka Maelezo kwa Ufupi kabisa, trend ya Kilimo cha Tanzani kiko vipi na kama hizo ndo factor kuu zinazo fanya wakulima wasipige hatua,

  1. Mkuu mmeisha wahi kufanya tafiti na kugundua sababu kuu zinazo zorotesha kilimo?

  2. Nyie bila shaka ni Graduate wa Sua au Chuo chochote kile cha kilimo, Je Mna mashamba yenu ya Kufanyia Demonstaration? au Mashamba Darasa?

  3. Mmesema Mko Moshi, Ok kwa sasa Mkoa wa Kilimanjaro watu wameshindwa Kuvuna kabisa na Mkoa unakaribiwa na Njaa je sababu ni nini?

  4. Na kwa Mkoa wa Arusha ni hivyo hivyo, kULE Karatu ambako ndo ilikuwa Kituo kikuu cha Mazao mambo yamebadilika je sababu ni zipi?

  Kwa sababu ukijarubu kutembelea Mikoa Mingi ya Tanzania, unaweza Kuja na Jibu tofauti kabisa na Mnayo yaongea, Chukulia Mfano wa Mikoa inayo lima PAMBA kwa sasa watu wamekata tamaa ya kulima Pamba kabisa
  ,
   
 6. J

  JBAM Member

  #6
  Sep 17, 2012
  Joined: Feb 16, 2012
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mkuu tunashukuru kwanza kwa kusoma na kuona umuhimu wa kukomment. Kampuni hii inawataalam wa kila idara kwenye maswala ya kilimo ikiwa ni pamoja na mifugo. karibu upate huduma ya hali ya juu.
   
 7. J

  JBAM Member

  #7
  Sep 17, 2012
  Joined: Feb 16, 2012
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kaka kwanza hongera sana kwa kuwa na milioni mbili. tunaomba kukuhakikishia kuwa huo ni mtaji tosha kwa kuanzia hasa katika small scale. kumbuka hata mbuyu ulianza kama mchicha. karibu tukusaidie kuvuka hatua nyingine katika maisha. thanx
   
 8. J

  JBAM Member

  #8
  Sep 17, 2012
  Joined: Feb 16, 2012
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mkuu kwanza karibu sana mbono technologies. kilimo cha tanzania kina matatizo mengi mojawapo ikiwa ni "mambo ya kisera na mifumo" lakini pamoja na changamoto zilizopo bado tunaopportunities nyingi sana ambazo zinaweza kutufanya tuendelee.

  hayo tuliyoyaeleza ni baadhi tu ya kazi ambazo tunashughulika nazo lakini yapo mengi zidi tunayoyafanya katika sekta ya kilimo.

  hakuna wakati hata mmoja ambambo sekta ya kilimo itakosa changamoto katika nchi hii na duniani kwa ujumla. nitakupa mfano wa climate change kwa sasa ni kitu ambacho hakikuwepo miaka 40 iliyopita na kwa maana hiyo swala la irrigation halikuwa kipaumbele kwa wakulima wetu, pia kama uko kilimanjaro swala la upatikanaji wa ardhi bora ya kilimo ni changamoto kwa sasa kitu ambacho hakikuwa hivyo miaka 30 ilopita kwamaana hiyo unahitaji kuongeza tija (productivity) kwa eneo dogo ulilonalo (yield per unit area) kukidhi mahitaji ya chakula yanayoongezeka kila siku.

  tunashamba na tunalima na kufuga kisasa.nawe karibu tukufanyie demonstration shambani kwako uonje utamu wa kilimo cha kisasa.

  ni kweli tunaofisi moshi. swala la njaa kwa mkoa wa kilimanjaro na arusha na maeneo meeeeeengi ya nchi yetu kwa kiasi kikubwa ni matokeo ya factors nyingi lakini kubwa zaidi ni kilimo cha mazoea ambacho tunaendelea kukifanya. kwamfano kama umepita barabara ya arusha moshi kunamto mkubwa (mto kikavu) baada ya barabara ya machame kuelekea kwa sadala. mto huo unamaji yanayotiririka hata sasa lakini maajabu ni kuwa mahindi yaliyolimwa pembezoni mwa mto huo yamekauka ati tunasema mwaka huu mvua haikunyesha kabisa. hii ni dhihaka kubwa na haihitaji utafiti wala tume.

  mkuu kwaufupi kizazi hiki cha "face book farmers" kinahitaji kubadilika, tuingie kwenye kilimo cha kisasa kwa vitendo, tuache kulalamika na kumtafuta mchawi. start now as an individual/ group. soko lipo yaani tunaimport kilakitu mpaka mayai?? Aibu kubwa. tunazungukwa na kenya, somalia sudan na nyingine nyingi ambazo zinahitaji chakula, mboga. matunda tuchape kazi mkubwa kwa kutumia kile tulichonacho.
   
 9. J

  JBAM Member

  #9
  Sep 17, 2012
  Joined: Feb 16, 2012
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kaka kwanza hongera sana kwa kuwa na milioni mbili. tunaomba kukuhakikishia kuwa huo ni mtaji tosha kwa kuanzia hasa katika small scale. kumbuka hata mbuyu ulianza kama mchicha. karibu tukusaidie kuvuka hatua nyingine katika maisha. thanx
   
 10. Root

  Root JF-Expert Member

  #10
  Sep 17, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 26,293
  Likes Received: 13,004
  Trophy Points: 280
  Kilimo Uti Mgongo wa Taifa (KUMTA)
   
 11. r

  rhysrose Member

  #11
  Sep 18, 2012
  Joined: Aug 8, 2012
  Messages: 13
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Habari,
  nahitaji kufanya soil test-- hii number nikipiga haiconnect, kama una number nyingine naomba, au hata email address itakuwa poa!
   
 12. J

  JBAM Member

  #12
  Sep 18, 2012
  Joined: Feb 16, 2012
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mkuu pole sana kwa usumbufu. Tulikuwa field mahali penye shida ya mtandao. tucheki kwenye hiyo tigo au jaribu na 0784828927. karibu sana.
   
Loading...