CHIMBULI WA CHIMBULI
JF-Expert Member
- Jan 10, 2013
- 468
- 160
Kupenda ni suala ambalo ni innate/ in born tendence ni jambo la Asili. haliepukiki mtu kupenda na wengi wetu tumeshapendwa au kupenda, tumeshawahi au tupo kwenye mapenzi. kwangu mimi napenda tu kueleza kuwa ni bora kupendwa kuliko kupenda linapokuja suala la Kusalitiwa. hapa nazungumzia mapenzi ya Kweli kwani ukimpenda mtu UTAMWAMINI, utamjali, utamthamini, utatumia muda mwingi ufikirie usimkwaze na umridhishe mwenzio. Lakini cha kushangaza yule unaempenda kwa dhati anaweza kugeuka na Kuwa chanzo cha matatizo kwako kwani anaweza pelekea usipate ladha ya chakula, usilale kwa amani, ujute kumjua, ujute kutumia rasilimali kadhaa ikiwemo raslimali muhimu zaidi yaani muda kwake. kwangu mimi simuamini mwanamke yeyote na kutokana na yaliyonikuta nimemuweka mwanamke kuwa mtu asie na msimamo, Haaminiki, hata umpende vipi ipo siku atakufanyia jambo la ajabu sana never trust a woman. naamini wapo wanawake hawawaamini wanaume. Tupeane uzoefu mapenzi yamewahi kukuathiri je yalikuathiri vipi? karibuni wadau.