Ushauri na uzoefu wa kutatua janga la kupenda

sibbonnobo

JF-Expert Member
Aug 24, 2019
724
877
Wana nzengo ngoja na mimi nitiririke kidogo leo kutokana na masaibu yangu.

Waswahili wanasema "Unaweza kupenda chongo ukaita kengeza au kipendacho roho hula nyama mbichi n.k".

Kwa miaka miwili nimekuwa na demu wangu tulikutana tu kwenye mitandao ikatokea tumependana tukaanza mahusiano, lakini kwa upande wangu hasa ninampenda sana na nilikuwa na nia ya kumfanya mama watoto.

Katika uchunguzi wangu niligundua kuwa amepitia mahusiano mengi sana na wengine walidiriki hata kumfungulia biashara ila zilikufa baadae. Niligundua pia shoga zake ni wadangaji. Hata yeye alikuwa katika hayo mambo.

Kwa kuwa nimependa, nilijaribu sana kumuondoa katika maisha yasiyo na muelekeo na alionyesha kutii hilo japokuwa kuna matukio nilikuwa siyaelewi elewi.

Kilichokuwa kikiniudhi anaweza kuvunja hata appointment na wewe kisa marafiki zake wamemuita. Ukimwambia nikutoe anasema hajisikii ila rafiki zake wakimualika lazima ahudhurie mwaliko. Na akija geto muda mwingi yuko busy anachati. Na hataki kabisa usogelee simu yake.

Cha kushangaza anapenda sana kuchunguza simu yangu na akikuta madudu ni ugomvi sana. Nikiri tu kuwa ni kweli nilikuwa nawapelekea moto wanawake na ni kwa sababu kutolipa kipaumbele suala la kukutana na yeye kimwili akidai tuwe busy na kutafuta hela hayo mapenzi yapo tu.

Kuna wakati nampigia simu usiku yupo viwanja vya starehe bila taarifa ukimuuliza yuko wapi ni ngumu kukupa jibu.

Ni mengi ila najaribu kufupisha. Jana nimemgombeza sana kiasi kwamba kwa hasira kuna maneno mazito niliongea na aka rise issue kwamba nimemkashifu na mwisho wetu ndio huo hataki lolote kutoka kwangu.

Shida inakuja kati ya moyo na akili zangu. Nikifikiri kwa kina akili inasema huyu si mwanamke wa kuwa nae ila moyo bado unampenda sana. Nifanyeje??

Naomba niishie hapo. Kwenu wakuu.
 
Kusoma hujui hata picha huoni. Hajaacha udangaji ndio maana wenzake wakimwitia kazi fasta anaenda. Ni sawa na wewe mwana akuitie deal.
 
Mzee si utafute Mwanamke mwenye wazazi wake na Usimamizi wa Kueleweka, Huyo keshavuka mipaka kiasi hutamuweza tena kama Utamuoa japo na We unapaswa Kutulia acha kubadili wanawake ila Kwa Huyo Mwanamke hakufai japo Inategema na tabia yako Maana Huenda Mungu kakupa mtu wa Kufanana nae
 
Mkuu kwanza nikupe pole Sana kwa yanayokusibu. Ushauri wangu tu Ni kwamba acha kuuendekeza moyo,,usitumie moyo wako kufanya maamuzi hata kidogo,,moyo una upofu mkubwa Sana. Tumia akili yako kufanya maamuzi hapo ndipo utaona vitu katika upana zaidi.

Kukutana mitandaoni sio tatizo shida inakuja kwenye hizo tabia alizonazo, huyo Ni mdangaji na bado hajaacha, muache kaa tulia na kwakua yeye ndo amekutamkia kuwa Ni mwisho bas tulia kimya Kama hujawahi kumjua,, moyo wako utapona na utampata wa kufanana nawe,, after all no hurry in Africa
 
Mmekutana mtandaoni, ana mashoga wadangaji, anawasikiliza sana rafiki zake kuliko wewe. had hapo ujajua kuwa unatoka na kamalaya kumoja kajanja kamjini?
anapenda kukagua sim yako na akikuta madudu ni ugomvi(wivu uliopitiza una reflect kile kilichopo ndan mhusika)
Asante kwa kunipa moyo. Unajua huwa najiuliza kwa nini nampenda huyu demu coz ana kila harufu ya maovu.

Na wakati mwengine ananipaga story za ndani kabisa jinsi gani watu wanadanga. Na hata tabia za jamaa aliowahi kuwa nao.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Hamna kitu hapo...tumia akili kwenye mambo hatari Kama hayo..moyo utakupa majuto haunaga shukrani hata kidogo
Kweli mkuu. Sikutaka tu kuandika hadithi ndefu ila kuna jamaa wengi walishataka kumchukua kwa jumla lakini waliishia njiani. Kimeo kabisa.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom