oneflash
JF-Expert Member
- Oct 4, 2014
- 814
- 600
Bara letu tukufu la la Afrika limekuwa likidharauliwa kila kuchao.Tumebakia nyuma kimaendeleo licha ya kuwa na raslimali sii haba. Lakini kadri ya uwezo wetu, bado twaendelea kujizatiti angalau kujinasua kwenye taswira hii mbaya ya wale wasiojiweza. Ni wajibu wetu kama raia na uongozi wa nchi mbalimbali husika kuwa na bidii ya mchwa ili kuafikia malengo yetu. Bila shaka kuna baadhi ya nchi ambazo ni za kupewa kongole kwa kazi nzuri ya kutwalia bara hili sifa kochokocho.
Aghalabu kwa upande mwingine ukweli unasalia kuwa ule ule ya kwamba, baadhi ya nchi imekuwa tuu ni majanga na aibu. Mfano ni kama: Somalia na Sudan ya kusini na zinginezo ambazo sijataja, kwa vita na uongozi mbaya hawajambo. Kwa mataifa mengine, mbali na kuwa na amani bado'wapo wapo' tuu, sio kimichezo, kiuchumi etc.
Kwa watani wetu wa kusini, kwa maelezo na ikiwezekana kwa mapicha vile nilivyofanya hapo Chini. Ni kitu gani unahisi nchi yako kama TZ imefanya kulisaidia bara hili kutambulika kwenye ramani ya ulimwengu? Nimejaribu kuwaza hali ingekuwa aje kama Nigeria ingetolewa Afrika ya magharibi, Afrika kusini ikatolewa kusini, misri itolewe kaskazini na vile vile Kenya ikatolewa Mashariki! Si bara lingebaki gofu? Nawasilisha!....
I