Kwa wadau wa makulaji

Mphamvu

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
10,710
2,000
Pamoja na mambo mengine, mimi hupenda kula. Sio mvivu wa kula na wakati mwingine huwa nashiba vitu vidogodogo vidogo vya kula njiani, mradi tu visiwe vyakula ----- (vyenye masukari mengi na visivyo na faida mwilini.

Majuzi katika pitapita zangu nikatokea Msikiti wa Kiblatan (au Qiblahtein) ulioko maeneo ya Kariakoo (jina la mtaa sijui) lakini si mbali sana kutoka sokoni ukiwa unaelekea Kongo. Hapo nikakuta meza nyingi za kuuza mapochopocho, ukiwemo urojo ambao naupenda saanah. Pia kuna mishkaki, mihogo ya kuchoma, ndizi choma, juisi ya miwa, tende, matunda, chipsi, kuku choma, supu ya pweza, ngizi, samaki wa kukaanga na vingine vingi.

Nikaweka kituo kwa muda, nikapata nilichokipata.

Karibuni....

CC: vanmedy
 
Last edited by a moderator:

Judgement

JF-Expert Member
Nov 13, 2011
10,338
1,225
Mimi ukitaka unifikishe kileleni nipe ugali (dona) uliyomixiwa na unga wa muhogo na harage lililoungwa kwa mawese/nazi .
Nitakua nimeitendea haki nafsi .
 
maroon7

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
9,012
2,000
Hivi sio wewe tulikaa siti moja kwenye bus? Ulianza kununua mahindi ya kuchemsha, mbele kidogo karanga, mbele tena chips mayai, tuliposhuka kuchmba dawa ukanunua visheti na vitumbua, mayai ya kuchemsha ukala pale chalinze, kibaha ukala apples, mbezi ukanunua vipande vya nanasi..ukashukia kimara nikaona unanunua mahindi ya kuchoma
 
Kiswahili swanifu pipo kama huyu anaitwa MABUKANYA !
 
Mphamvu

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
10,710
2,000
Napita kwanza

Pita kwa amani mama, ukirudi uje tujiunge hapa kwenye kujenga mwili...

Mie nakuja kula huo urojo...

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
Karibu bibie, mie niko hapa meza ya jirani napata jiusi ya miwa...

He he heeeeee, we kama mm. Kula baba, mwili haujengwi kwa matofali

Hilo nalijua zamani, acha tule tukiwa na afya, visukari vikishaanza tuwe wapole tu.

Wali maharage/samaki ndio mpango mzima
Nalog off
Hata mimi nauelewa huo, sema makulaji haya ni kwa ajili ya kuchangamsha mdomo tu...
 
Mphamvu

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
10,710
2,000
Hivi sio wewe tulikaa siti moja kwenye bus? Ulianza kununua mahindi ya kuchemsha, mbele kidogo karanga, mbele tena chips mayai, tuliposhuka kuchmba dawa ukanunua visheti na vitumbua, mayai ya kuchemsha ukala pale chalinze, kibaha ukala apples, mbezi ukanunua vipande vya nanasi..ukashukia kimara nikaona unanunua mahindi ya kuchoma

Safarini huwa nazuia kichupa cha Val**u, miksa kina mrija kwa juu na kimefungwa kwa karatasi...
 
maroon7

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
9,012
2,000
Safarini huwa nazuia kichupa cha Val**u, miksa kina mrija kwa juu na kimefungwa kwa karatasi...
Hahahaaa...kuna jamaa alikua anakunywa maji nikawa nashangaa jamaa anachangamka tu kumbe ni konyagi kaweka kwenye chupa ya Maji ya uhai
 
shansarie

JF-Expert Member
May 25, 2013
5,694
1,500
Hivi sio wewe tulikaa siti moja kwenye bus? Ulianza kununua mahindi ya kuchemsha, mbele kidogo karanga, mbele tena chips mayai, tuliposhuka kuchmba dawa ukanunua visheti na vitumbua, mayai ya kuchemsha ukala pale chalinze, kibaha ukala apples, mbezi ukanunua vipande vya nanasi..ukashukia kimara nikaona unanunua mahindi ya kuchoma

Tumbo balaa
 
Mamndenyi

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
31,600
2,000
Huwa napenda pia tafuna tafuna njiani hasa nikiwa private car. Nakulaga apple Au korosho na wakati mwingine karanga.
 
Katavi

Platinum Member
Aug 31, 2009
41,393
2,000
Hivi sio wewe tulikaa siti moja kwenye bus? Ulianza kununua mahindi ya kuchemsha, mbele kidogo karanga, mbele tena chips mayai, tuliposhuka kuchmba dawa ukanunua visheti na vitumbua, mayai ya kuchemsha ukala pale chalinze, kibaha ukala apples, mbezi ukanunua vipande vya nanasi..ukashukia kimara nikaona unanunua mahindi ya kuchoma
Huyu sio mtu wa kawaida.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom