Kwa wadada wenzangu: tuwe makini na aina hii ya wanaume....... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa wadada wenzangu: tuwe makini na aina hii ya wanaume.......

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Michelle, Mar 5, 2011.

 1. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #1
  Mar 5, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Kwa wadada wenzangu....wanasema experience is the best teacher....leo tu share experience na tupeane ushauri......

  Wengi wetu tutakuwa tumekutana na wanaume ambao mimi ninawaita wanaume malengo ya mbele na wanaume waharakisha mambo na wanaume maneno.....

  Mwanaume ya malengo mbele ni Yule ambaye kupitia maneno yake anakujengea picha ya baadaye ili apate mahitaji yake ya sasa.Yeye anakujengea picha ya nyie mkiwa na familia yenu,watoto,ndoa nzuri,mkienda matembezi pamoja mwisho wa mwaka nk....hii yote ni ili kukujengea picha kuwa wewe ni sehemu ya maisha yake na kwamba kila analoliwaza analiwaza kulifanya akiwa na wewe siku za mbeleni.
  Kwa furaha wanawake walio wengi huwapokea wanaume wa aina hii kwa mikono miwili na wengine wetu huenda hata kutoa sadaka maombi yetu yamejibiwa na kuanza kuwaweka maanani aina hii ya wanaume......

  Wanaume waharakisha mambo ni wale ambao wana haraka sana utafikiri wanakimbizwa na moto...hawa ni wale unakutana nae na mara moja anahakikisha umekuwa nae karibu sana kwa wakati mfupi....anahakikisha huoni wala huzifahamu tabia zake chafu.hawa tofauti na wanaume malengo mbele,kwa muda mfupi sana wanahakikisha umewaweka kwenye akili yako,kila saa wanapiga simu,wanaandika message,wanataka kuwa pamoja nawe kila saa,wanakutambulisha kwa ndugu wale kama binamu,mpwa na si wazazi na marafiki zao,wanakupa funguo za nyumba zao na ujanja mwingine wa aina hiyo.
  Hawa wanajenga hisia za msichana kwao haraka na wanataka muwe na uhusiano wa kimapenzi haraka.....
  Kwa akilo ya kawaida utajiona hakuna kama wewe hapa duniani na una bahati sana,ila baada ya muda mfupi sana watakuliza vibaya walio wengi.

  Wanaume maneno.....hawa ni wanaume wazuri sana kwenye kusema...yaani anaweza kuahidi kila awezacho na atakujengea mazingira ya kuamini anaweza kufanya hivyo....ila hawatekelezi na hawana uwezo huo wa kufanya hivyo ,na wengine hata kama wanao uwezo hawafikirii ndani ya roho zao kufanya hivyo,wanaahidi wapate wakitakacho........

  Ushauri wangu sasa:

  1.Wasichana tuwe makini na tuchukue muda kuwafahamu wanaume wanaokuja kutaka mahusiano na sisi....haraka haraka haina baraka.....mtu hata jina lako la pili halijui anakuahidi ndoa sijui nini....tuweni makini....there is no fire,you do not have to rush kutoa akili.moyo na mwili wako kwa mwanaume usiyemfahamu vizuri. Kile kipindi cha dating tukitumia vizuri kuwasoma na kuwafahamu wanaume...na si wakati wa dating umeshatoa mwili na akili yako na hata moyo wako.....open your ears and eyes and intelligency 100% and not your legs.

  2.Tuache tabia ya kuamini ovyo,mtu anakuahidi hiki hafanyi,kile hafanyi....he does not keep promises....wewe nawe umo tu unaendelea nae ukiamini atabadilika au amesahau au unaogopa kumuuliza.....mtu anayekupenda atatenda lile alisemalo kwa wakati,na kama atashindwa utakuwa wa kwanza kujua sababu na zitaeleweka......tuwe wakali kidogo na tuhoji....unamuogopa oh,nikimuuliza ataniacha,kama ni wakukuacha atakuacha tu.

  3.Tukubali kuwa tumedanganywa na tuwe wajasiri wa kusonga mbele.Mara kibao unasikia msichana anasema najua ananidanganya ila sasa nifanyeje ndo nimeshalala nae,nimezaa nae,siwezi muacha,tutabanana hapo hapo hadi anioe.....we si wa kwanza kudanganywa,kaa chini lia kama inakubidi,fikiria ulivyodanganywa na ukadanganyika na jifunze then tulia kwa muda na chukua uamuzi wa kuondoka kwenye utumwa wa kosa la kudanganyika then songa mbele kwa kujiamini,kuwa makini na kumuomba Mungu kwa sana.

  Ni hayo tu,.....nawapenda wote na nawatakia wikiendi njema.
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Mar 5, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  good point.....
  but they say attraction is not a choice....

  so usiwalaumu sana....

  sometimes we fall in love with the wrong people while we know its a mistake....
  because atraction is not a choice,it just happens..........
   
 3. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #3
  Mar 5, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Siwezi mlaumu mtu kwa kuwa nami yamenikuta....ndo maana nikasema experience is the best teacher....i have learnt my lessons and i ought to share my lessons.....

  umeadimika Boss.....
   
 4. CPU

  CPU JF Gold Member

  #4
  Mar 5, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Nilikuwa nashangaa mbona uko kimya sana wakati nakuona on air
  Kumbe KOBE ALIKUWA ANATUNGA SHERIA??!!! Safi sana mpenzi wangu

  [​IMG]
   
 5. k

  kukubata Member

  #5
  Mar 5, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  havyo hunayo waambia wenzako wanaelewa
   
 6. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #6
  Mar 5, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  CPU we ni type ipi kati ya hizo?
   
 7. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #7
  Mar 5, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Kweli eeeh!!!!! asante kwa kuwasemea wenzangu.....!!!!
   
 8. CPU

  CPU JF Gold Member

  #8
  Mar 5, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135

  No one falls in love by choice, it is by CHANCE

  No one stays in love by chance, it is by WORK

  And


  No one falls out of love by chance, it is by CHOICE

   
 9. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #9
  Mar 5, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  Michelle nipo....
   
 10. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #10
  Mar 5, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
   
 11. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #11
  Mar 5, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160

  i think we ought to work together.....but if you do not keep promises, you dissapear and come back after sometime.....how am i suppose to work with you to build something out of the so called "LOVE?"
   
 12. CPU

  CPU JF Gold Member

  #12
  Mar 5, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  My dia, mimi sio muongeaji sana
  Hata nikisema simo kati ya hizo bado naweza nisiaminike, dawa ni hii hapo chini


   
 13. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #13
  Mar 5, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  eti we si muongeaji sana? ila kwenye keyboard unaweza andika sana eeeeh.....haya bwana!!!
   
 14. Jahmercy

  Jahmercy Member

  #14
  Mar 5, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 69
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Kwa ambaye hayajamkuta ni vigum sana kuyatambua hayo, eti wanadai mapenz ni upofu.
   
 15. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #15
  Mar 5, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Sometimes its not good to rush things ni bora kukaa na kukubaliana way forward
   
 16. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #16
  Mar 5, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Jambo Jambo
   
 17. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #17
  Mar 5, 2011
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  unfortunatelly umeshindwa kuinclude katika maelezo yako wanaume wa type yetu............mimi ni type ya akili kumukichwa................ naomba ufafanuzi basi kwa dada zetu sisi ni watu wa aina gani ili tukiwapigia vuvuzela wachape lapa............
   
 18. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #18
  Mar 5, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  ni kweli....unapofuka ila kuna mambo yatakufungua macho tu.....tulishapofuka sana ila kwa tabu tulizopata...tuliona na kusonga mbele macho wazi na masikio....
   
 19. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #19
  Mar 5, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  kweli aisee,utaepuka mengi.....wewe ni type ipi hapo kaka?
   
 20. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #20
  Mar 5, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  mi sijambo,u hali gani the happiest man alive.....???
   
Loading...