Nguli, umenishika pabaya. Umenikumbusha wazee waliokaa (kari) nyuma ya full suit(nyumba ya iliyoezekwa na majani ya mgomba), kina mama wako kwa mbele huku mbege ikigawanya na mzee wa heshima. Anachota kata kubwa anapelekewa mzee mkubwa zaidi kiumri, jamaa anapiga (pafu) la nguvu, mzee baada ya kuipokea anamtafuta aliye na umri mdogo kuliko yeye anamwambia (bencho/ riya) kunywa kidogo, jamaa anapiga pafu kidogo anamrudishia mzee. Daah, mzee anaipokea na kwa ustadi mkubwa anaipuliza kidogo kusogeza(miincho) ulezi pembeni halafu anaipiga kama mara tatu hivi, kwa! kwa! kwa! Zoezi linaendelea hadi watu wakikolea (mbasa) ngoma inaanza...! Kumbuka wakati huo nyimbo za dini kama TUPALIZE SAUTI ZEETU, WOTE TUMTUKUZE LEOO....zinaimbwa kwa sauti kuubwa. ni raha sana. Mimi naaza mapema kabisa kula (ngesi) dawa ya kusafisha tumbo!