Kwa viongozi wetu: Asili ni asili tuu. Mbuga zetu, milima yetu n.k hata zikiwa zote Kilwa, bado ni mali ya Taifa. Tuviboreshe kwenye asili zake.

Kididimo

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
3,791
3,360
Asbh hii, nimemsikia kiongozi mmoja anahoji, "kwa nini Watalii iwe ni Kaskazini tuu na siyo pengine? Akaendelea, mimi nataka nifungue vivutio vingi kwingine ili watalii wapungue kule Kaskazini waende na kwingine ninakotengeneza vivutio kama vya kule."
Mimi sina mtizamo wa kupinga hoja hii, ila kuna hoja nimeshindwa kuzielewa;
1. Mbuga na vivutio vingine kama Mlima Kilimanjaro viliwekwa na nani?
2. Je, watalii kuongezeka Kaskazini, na mapato kuongezeka ni manufaa kwa nani?
3. Kwa utafiti mdogo, watalii hawaendi sehemu kuona jambo moja tuu, hupendelea zaidi kuona vivutio vingi zaidi wakijua viko sehemu moja. Ukiacha mbuga za wanyama, kuna mfano mlima Kilimanjaro ambao ni kivutio kikubwa barani Afrika. Na huu unaweza kuwa ndiyo kivutio namba moja kwa Kaskazini. Hapa itakuwaje uhamisho wake?
4. Kama lengo ni kulazimisha kutawanya watalii hadi kule wasikotosheleza haja zao, ikatoea wamegairi, fidia ya mporomoko wa hayo mapato, nani awajibike?
Kiujumla, nini mashaka na matamko haya, japo nia ya Kiongozi huyu inaweza kuwa njema, ila tujadili hili.
 
Ni ishara ya ubaguzi na kuligawa taifa. kwa kawaida tumefundishwa Kila kitu kilichokua ndani ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ni Chetu, haijalishi kipo wapi ndomaana tunamuingiliano mkubwa wa kijamii. kwa hali tunayopelekewa leo inaamisha jamii wao ni watu tofauti baina ya kusini na kasikazini au mashariki na magharibi.
 
Ngororo Crater ni moja ya maajabu ya dunia, sehemu tambarare isiyo na mwinuko na wanyama wanaishi kwenye natural environment.

Kilimanjaro ni mlima wa pili kwa urefu duniani.

Serengeti ni mbuga yenye uoto wa asili na wingi wa wanyama wanaoishi kwenye mazingira asilia.

Mtalii akinunua ticket anapanda mlima , kuona Crater na kuona Serengeti katika safari moja.

Burigi kuna ajabu gani?
 
Ukabila kwenu ni genetical behavior
 
natamani ningekuwa igpi
natamani ningekuwa padirii
natamani ningekuwa maalaika
natamani Sherengeti iwe burigii

Maendeleo hayana chama

Msemo unaovuma kitaa:KWANI UNATESEKA!
 
Hivi hawajiulizi ni kwanini Mikumi au Ruaha(mbuga kubwa kuliko zote) zinapokea idani ndogo ya watalii kuliko Ngorongoro? au Serengeti? Mtalii haji kuangalia wanyama tu,kama ingekuwa hivyo basi wasingekuja maana kwenye zoo zao wana wanyama karibu wote wanaopatikana duniani,kuanzia Africa,Asia hadi wa huko south america.
Uniqueness ndio kitu pekee kinachowavutia watalii.Serengeti great migration ndio imeifanya hii mbuga kuwa maarufu zaidi duniani pengine kuliko hata nchi ya Tanzania yenyewe.Yaani mtu wa huko ukimwambia natoka Tanzania haijui ila anaijua au ameisikia serengeti.TV station maarufu duniani zimeonesha na zinaendelea kuonesha sifa hii ya Serengeti nchi mbalimbali.Nenda nchi yoyote ya Ulaya hauwezi kupita mwaka serengeti migration haijaoneshwa.
Vile vile mlima Kilimanjaro mrefu kuliko yote africa ni maarufu kwa upekee wake hivyo mtalii anakuwa na dream ya siku moja aje aupande.
Nilimsikia kigwangalla anasema eti wanataka kupunguza msongamano wa watalii kaskazini na kuwafanya watembelee sehemu nyingine kutalii.Labda ajue tu watalii si ng'ombe,huwezi kumlazimisha eti aende burigi asiende serengeti kuangalia wildebeest migration au asiende Ngorongoro crater maarufu wanayoishi wanyama na binadamu.Kama hakuna kitu cha utofauti hiyo mbuga ya burigi haitakuwa tofauti na saadani .
 
Business orianted minds tunafahamu kabisa biashara hua haiendi kwa kanuni kama za mzee lakini ngoja tuone itakuaje mbele ya safari tuzidi kumuombea mema,
 
Ngororo Crater ni moja ya maajabu ya dunia, sehemu tambarare isiyo na mwinuko na wanyama wanaishi kwenye natural environment.

Kilimanjaro ni mlima wa pili kwa urefu duniani.

Serengeti ni mbuga yenye uoto wa asili na wingi wa wanyama wanaoishi kwenye mazingira asilia.

Mtalii akinunua ticket anapanda mlima , kuona Crater na kuona Serengeti katika safari moja.

Burigi kuna ajabu gani?
Sanamu la nyelele ,Baba wa taifa la chato
 
Asbh hii, nimemsikia kiongozi mmoja anahoji, "kwa nini Watalii iwe ni Kaskazini tuu na siyo pengine? Akaendelea, mimi nataka nifungue vivutio vingi kwingine ili watalii wapungue kule Kaskazini waende na kwingine ninakotengeneza vivutio kama vya kule."
Mimi sina mtizamo wa kupinga hoja hii, ila kuna hoja nimeshindwa kuzielewa;
1. Mbuga na vivutio vingine kama Mlima Kilimanjaro viliwekwa na nani?
2. Je, watalii kuongezeka Kaskazini, na mapato kuongezeka ni manufaa kwa nani?
3. Kwa utafiti mdogo, watalii hawaendi sehemu kuona jambo moja tuu, hupendelea zaidi kuona vivutio vingi zaidi wakijua viko sehemu moja. Ukiacha mbuga za wanyama, kuna mfano mlima Kilimanjaro ambao ni kivutio kikubwa barani Afrika. Na huu unaweza kuwa ndiyo kivutio namba moja kwa Kaskazini. Hapa itakuwaje uhamisho wake?
4. Kama lengo ni kulazimisha kutawanya watalii hadi kule wasikotosheleza haja zao, ikatoea wamegairi, fidia ya mporomoko wa hayo mapato, nani awajibike?
Kiujumla, nini mashaka na matamko haya, japo nia ya Kiongozi huyu inaweza kuwa njema, ila tujadili hili.
Na dhahabu naye ichukuliwe ikapandwe na kwingine pia ili kuwe na uwiano mzuri wa rasilimali/maliasili.
 
Ngororo Crater ni moja ya maajabu ya dunia, sehemu tambarare isiyo na mwinuko na wanyama wanaishi kwenye natural environment.

Kilimanjaro ni mlima wa pili kwa urefu duniani.

Serengeti ni mbuga yenye uoto wa asili na wingi wa wanyama wanaoishi kwenye mazingira asilia.

Mtalii akinunua ticket anapanda mlima , kuona Crater na kuona Serengeti katika safari moja.

Burigi kuna ajabu gani?
Burigi kuna maajabu mengi, kuna ngedele anacheka kama mtu, kuna chatu wanavusha watu mtoni kuepuka mamba ahaaa!!!
 
Ni sawa. Lakini watalii watakaokuja kuwaona hao ngedere ni lazima wawe ni wale walewale watakaopanda mlima Kilimanjaro? Kuwa, wangezuiwa baadhi kwenda Kilimanjaro ili wagawane mapato kati ya Tanapa ya huko na ile ya kule? Kwa nini kama viongozi wasione kuwa hiyo ni fursa mpya ya kuongeza watalii nchini kwa ujumla wake, na siyo suala la kupunguza sehemu moja kujazia kwingine?
 
Yaani ni sawa na kuuliza kwanini dhahabu iwe kanda ya ziwa tuu na sio Kaskazini..
Yaani wangekuwa na uwezo hata mlima Meru na Kilimanjaro wange upeleka Chato
Mimi nashauri watengeneze huo MLIMA CHATO. Mbona ni rahisi tu? Malori makubwa 1000 na magreda 200 yakichimba na kupakia kwenye hayo malori, eneo kama la kilometa tano za mraba, huo mlima wa udongo na mawe na kokoto utakuwa mrefu sana. MLIMA CHATO OYEEE
 
Ngororo Crater ni moja ya maajabu ya dunia, sehemu tambarare isiyo na mwinuko na wanyama wanaishi kwenye natural environment.

Kilimanjaro ni mlima wa pili kwa urefu duniani.

Serengeti ni mbuga yenye uoto wa asili na wingi wa wanyama wanaoishi kwenye mazingira asilia.

Mtalii akinunua ticket anapanda mlima , kuona Crater na kuona Serengeti katika safari moja.

Burigi kuna ajabu gani?

Unayosema ni kweli lakini sasa hivi kuna msongamano Serengeti unaotishia mpaka uasilia wa hifadhi, hivyo si vibaya watalii wakaona na vivutio vingine nchini kupunguza 'JAM'!
 
Tanzania kuna mbuga nyingi tu sio Serengeti tu lakini huwezi kumpangia mtalii aliyeona documentary ya great migration eti aende mikumi au huko burigi asiende serengeti wakati yeye dream yake ni kuona hiyo adventure ya wildebeest .Ni bora asije kuliko kuzima dream yake na kumpangia pa kwenda .
Tanzania inapokea watalii wasiozidi millioni moja kwa mwaka sasa hiyo Jam mnayosema ni ipi? Hata kukiwa na Jam huwezi kumpangia mtalii pa kwenda bora kutokwenda kama sehemu iko overcrowded
 
Mkuu anayesema hivyo atakuwa mpumbavu hana akili kichwani mwake!
 
Burigi siyo mbuga ya asili. Hiyo ni zoo tu kama walizonazo wazungu huko kwao. Hapa wanyama wamesombwa toka sehemu za mbali kupelekwa Burigi. Na kwenye zoo huwa wanachukua wanyama wanawaweka pamoja. Kwa hiyo hamna sababu yoyote mtalii kupoteza hela kwenda huko Burigi badala ya kwenda kwenye zoo ambazo wanazo na zina wanyama kama hao
 
Kuna nyerere wa bandia. ..

Back
Top Bottom