Ndugu waziri wa Utalii, boresheni utalii kwa kufanya mambo yafuatayo

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
10,005
2,000
Ndugu Waziri,

Takwimu zinaonyesha kuwa katika mambo yanayochangia pato kubwa la nchi yetu ni utalii. Kwa hiyo hii ni sekta inayopaswa kuchukuliwa serious sana na kuwekeza kwa nguvu zote ili pato la nchi liweze kuongezeka.

Kwa hiyo ndugu Waziri huu ni muda muafaka wa ubunifu na kuja na vyanzo vingi vya utalii. Tunahitaji kwenda beyond ya ile kutegemea tu vyanz vya utalii vya mbuga za wanyama, na ule wa mandhari kama kule Zanzibar na Mlima Kilimanjaro

Ndugu Waziri tunahitaji kufanya yafuatayo.

1.Utalii wa Kiutamaduni
Nchi yetu ina makabila 120, ndani ya makabila haya watu wana utamaduni mbalimbali, nyimbo, dawa, mavazi, nyumba, malezi ya watoto, chakula etc. Ninatambua kuwa kabila la kimasai limekuwa ni nembo ya nchi katika utalii wa kiutamaduni, Je Wizara kwa nini isione kuwa ni muhimu sasa kupanua wigo wa Utalii wa Kiutamaduni, Kwa kuinvolve na Makabila mbalimbali, Yaani Watalii waweze kwenda let say Kagera kuona utamaduni wa Wahaya, au Waende Mbeya wakaone utamaduni wa Wasafwa, Wanyakyusa, Wakavae mabazi yao, Wakacheze ngoma zao, Wakale chakula chao etc. Hii itasaidia Watalii waende sehemu nyingi zaidi nchini na kila watakapokwenda lazima kutakuwa na faida maana watatumia pesa

2. Wizara ije na mpango wa Utalii wa Kilimo
Sisi Tanzania tuna eneo kubwa sana, tunaweza kutenga maeneo kadha wa kadha tukasema kuwa haya maeneo ni kwa ajili ya utalii wa Kilimo. Huko Ulaya, Marekani etc, kuna watu wana hela nyingi tu wanatafuta shughuli za kufanya kujikeep busy.

Unaweza kuanzisha utalii wa Kilimo wa kuwaleta watu waje kwenye maeneo hayo Walime, Just for fun, Watu hao wataenjoy ile kujikeep busy, wataenjoy process nzima ya kushughulika, na ili uweze kuwavutia zaidi unaweza kuattach hilo suala na Charity, yaani kwa mkulima atakayevuna anaweza kutoa mazao yake kana Charity mashuleni au nyumba za watoto yatima, Au akiamua kuuza na kupata hela nayo ni sawa tu na tutamtoza kodi pia.

Waziri changamkia hii kitu, Tangaza utalii wa hivi huko nje kisha Uone kama watu hawajaamua Kuja Kuenjoy utalii wa "kujikeep busy" hapa nchini hasa kipindi cha Winter huko.

3. Peleka Utalii wa nchi hukohuko nje
Ndugu Waziri, Tunao uwezo wa Kuchagua nchi kadha wa kadha za Kistratejia na kufungua replica za mambo yetu yaliyoko Tanzania, Tuweke Tanzania food house humo, watu wale ugali, Makande, Ndizi Bukoba, Mlenda, Mahindi choma, Viazi vya kuchoma etc.
Weka kikundi cha ngoma za asili kwa ajili ya intertainment kila wiki au kila mwezi, Maduka ya nguo za asili etc. Kwenye hili unaweza kushirikisha watu binafsi katika mtindo wa PPP

4. Kuna vivutio vingine vingi nchini bado havijafunguliwa
Kuna maziwa madogodogo kama vile Ikimba huko Kagera, Kuna milima kama vile Uluguru, Usambara, Udzungwa, kuna visiwa vidogovidogo kwenye maziwa yetu na bahari zetu.
Siyo kila mtu anataka kupanda au anaweza kupanda mlima kilimanjaro, wengine wana interest ya kupanda milima ya size ya kati, Huu ni muda muafaka kwa Wizara kutafuta milima kadhaa na kuiwezesha miundo mbinu ya kuweza kuipanda. Huko China, kuna milima wameijengea ngazi vizuri sana kufuatisha njia ya kuipanda kuanzia chini hadi juu, Huu ni muda muafaka kwa wizara kufanya kitu kama hicho kwa baadhi ya milima nchini.
Pia kwenye Maziwa yetu wizara ianzishe utalii wa Kuvua samaki, Diving n. k. Hili linawezekana, Ni suala la wizara kujipanga na kushirikisha sekta binafsi. Kwenye visiwa vidogo vidogo chochea investors waje waweke vivutio huko, wajenge mahoteli etc. Bado kuna visiwa vingi vidogovidogo hatujaviexploit kabisa

5. Utalii wa Udugu, Utalii wa mtu kwa mtu
Wapo watu huko nje wangependa kuexperience maisha ya Waafrika, Yaani aje aishi na familia ya kiafrika kwa muda fulani kisha aondoke, inaweza kuwa wiki, mwezi au hata miezi. Wizara ijipange ione namna gani inaweza kufanikisha hili, ikiwemo kutunga sera na utaratibu wa kuwezesha hili. Kuna Wazee na watu wa nakamu huko nje ya nchi wako wana hela lakini wako lonely, wamengibe wana depression, wengine wanapenda tu adventure ba kujaribu mambo mbalimbali, wengine wanapebda kuconnect tu na watu wa background na utamaduni tofauti. Hili linawezekana, tuumize kichwa namna gani ya kufanya utalii huu

6. Utalii wa Kihistoria
Nchi yetu imepitia mambo mengi kabla ya ukoloni, tangu enzi za ukoloni na mpaka sasa. Huu ni mysa muafaka kwa Wizara ya Utalii kufanya mradi wa kukusanya taarifa za kutosha za tawala na Chiefdom zetu kabla ya ukoloni, Waweke kumbukumbu vizuri, hii itakuwa chachu kwa watalii wanaopenda kujua masuala ya historia, Pia Makaburi ya viongozi wetu wa Kitaifa pia ni chanzo kikubwa cha Utalii., Serikali itunge sheria kuwa Makaburi ya viongozi wakubwa pia ni nyara za serikali, hii ni kwa sababu makaburi hayo ni ishara ya historia ya nchi hii kwa miaka yote ambayo kiongozi huyo amehudumu nchini. Na pia site hizo za Makaburi zitakuwa ni kivutio kikubwa sana cha utalii.

Ndugu Waziri, Wizara iwe bunifu, isiendeshe utalii wa kimazoea.
Huu ni myda muafaka wa kuunda task force iende ikajifunze wenzetu wana vivutio gani na wameviendeleza vipi, ili na sisi tuje tuboreshe vya kwetu hapa nchini.

Pia ili kuwezesha hayo, ushirikiano baina ya serikali na sekta binafsi ni muhimu sana, kwa hiyo tazameni namna gani mnaweza kuwezesha hilo!

KAZI IENDELEE
 

kisu

JF-Expert Member
Mar 31, 2009
908
500
Pia ili kuvutia watalii wa kigeni kwa wingi, tozo ziwe sawa au zizidi kidogo (percent 10) ya tozo kwa wananch, faida itapatikana kwenye matumizi mengine ya mtalii kama hoteli, usafiri ndege/mabasi nk.
 

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
10,005
2,000
Pia ili kuvutia watalii wa kigeni kwa wingi, tozo ziwe sawa au zizidi kidogo (percent 10) ya tozo kwa wananch, faida itapatikana kwenye matumizi mengine ya mtalii kama hoteli, usafiri ndege/mabasi nk.
Hii sikubaliani na wewe.
Tozo wanazotozwa watalii wanazimudu, Kumleta mtalii kutoka nje aje alipe pesa sawa na mwananchi wa ndani ni kujipunja maana Wale wana Mihela wanaweza kuafford, Kwanza hizi tozo tunazowatoza wao wanaona ni peanuts. tunahitaji hizo pesa zao ili tuendeshe nchi.

Mwananchi ana haki ya kupewa punguzo kubwa kwa sababu kwanza vyanzo vya utalii ni mali yake na pia uchumi wetu ni mdogo kipato cha raia wengi si muafaka kuwatoza pesa ndefu
 

kirikou1

JF-Expert Member
Nov 8, 2016
4,273
2,000
Wadau wa utalii wawe sehemu ya kuishauri wizara kwa sababu wao ndio ground players
Kama ramaphosa alivyomchukua MO
 

kisu

JF-Expert Member
Mar 31, 2009
908
500
Hii sikubaliani na wewe.
Tozo wanazotozwa watalii wanazimudu, Kumleta mtalii kutoka nje aje alipe pesa sawa na mwananchi wa ndani ni kujipunja maana Wale wana Mihela wanaweza kuafford, Kwanza hizi tozo tunazowatoza wao wanaona ni peanuts. tunahitaji hizo pesa zao ili tuendeshe nchi.

Mwananchi ana haki ya kupewa punguzo kubwa kwa sababu kwanza vyanzo vya utalii ni mali yake na pia uchumi wetu ni mdogo kipato cha raia wengi si muafaka kuwatoza pesa ndefu
Kama tozo kwa wageni wanaona ni peanuts basi fanyeni tozo kwa mgeni shilingi milioni 10, na wazawa shilingi 10
 

Godo

JF-Expert Member
Apr 11, 2017
325
500
Nyarandu arudishwe jamaa ni mbunifu sana na wizara ilimkaa vilivyo kipindi chake watalii walikuwa wanamiminika haswa naona saizi hiyo wizara imepoa sana.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom