Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,895
- 20,392
Wadau, amani iwe kwenu.
Kumeibuka mjadala mzito kwenye mitandao ya kijamii baada ya Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete kumuomba Rais Magufuli kuwafikiria, kuwapongeza na kuwawezesha vijana 46 waliokuwa mitandaoni kukitetea chama. Naamini kuwa Kikwete alikuwa na dhamira njema ya kutambua mchango wa kila mmoja wetu alioutoa wakato wa mapambano ya kutwaa Dola. Naamini pia kuwa chama kilikuwa na mikakati imara ya kuhakikisha kuwa inashinda uchaguzi huo na miongoni mwa mikakati hiyo ni kuwa na vijana wa kushinda kwenye mitandao baada ya kubaini kuwa media zote zimenunuliwa na mafisadi.
Pamoja na hayo, binafsi naamini kuwa vijana hao 46 wapo chini ya chama. Kwa maana nyingine ni kwamba Mwenyekiti wa CCM ndiye anayewajibika kuwapongeza vijana hao na kuweka mikakati ya kuwawezesha ili wajipange upya kwa ajili ya 2020. Hata hivyo, hakika najisikia huzuni kubwa sana kuona Mwenyekiti wangu akitamka maneno hayo hadharani. Mikakati hiyo ilikuwa ya kichama na kitendo cha kutamka hadharani maana yake ni kwamba unadisclose mbinu za ushindi ambazo hazikupaswa kuwafikia maadui.
Nakubaliana na Maneno yako Mwenyekiti wangu kuwa Mwisho wa uchaguzi wa 2015 ni mwanzo wa uchaguzi wa 2020. Pia naamini kuwa mbinu zilizosaidia ushindi wa 2015 hazitatumika uchaguzi wa 2020 kwa vile CCM ina mbinu zaidi ya 200. Hata hivyo, wajibu wa kukitetea chama ni wa kila mwanachama. Inashangaza kuona Mwenyekiti ukiwaona vijana 46 tu ndio wanaostahili kupongezwa ilhali wapo vijana wengi hususan Wasanii ambao waliacha kazi zao na kuzunguka nchi nzima kukitetea chama mpaka wengine wakapachikwa majina mabaya yakiwemo WASALITI, WAPINGA MABADILIKO, WANATUMIKA KAMA CONDOM nk. Hawa umechukua hatua gani ya kuwapongeza?
Kutokana na kauli hiyo ya Kikwete na jinsi mjadala unavyoenda humu JF, hakika ninapata wasiwasi juu ya dhamira ya Januari Makamba. Ni vema tukajua hao vijana 46 aliwapataje? Je aliwaahidi nini? Mchango wao ulikuwaje mpaka Mwenyekiti wa Chama ashinikizwe kumuomba Rais awatambue vijana hao? Je wakati wa kuwaajiri vijana hao mlitangaza uwepo wa nafasi hizo kwenye Media? Kama mlifanya kimya kimya, iweje sasa mambo hayo yawe hadharani? Kuna tatizo gani limejitokeza?
Mambo haya ya kupongezana na kukwezana ndiyo yaliyowaponza Wapinzani. Mathalan, kule CHADEMA, kuna vijana kama akina Yeriko Nyerere, Michael Aweda, Marehemu Mohamed Mtoi, Henry Kilewo, Ben Saanane nk ambao walijifanya watetezi wakubwa wa chama kumbe walikuwa na malengo yao. Matokeo yake, waliojitokea kwa dhati kama akina Nusrat Hanje wamejikuta wakitupwa hata kwenye nafasi za viti maalum. Hizo ndo siasa za upinzani. CCM tunaamini kuwa kujitolea kwa ajili ya chama ni wajibu wa kila mwanachama na si mtu anafanya hivyo ili apate chochote au awe mtu fulani baada ya ushindi. Kama dhamira ya hao vijana ilikuwa wale shavu, hakika hawafai kuwa Makomredi. Watu wa aina hiyo ni rahisi kurubunika kama ilivyotokea kwa akina MUSSA ALLAN, MINYOO, FUNZA, MAMNDENYI, ASSADSYRIA3 na wengineo ambao wa sasa wamegeuka kuwa wapambe wa upinzani baada ya kununuliwa na fisadi Lowasa.
Narudia tena kusema kuwa kama dhamira ya vijana hao ni kutaka wapongezwe na hatimaye wateuliwe kuwa watu fulani au waajiriwe Serikalini, hakika hawafai kuwa wana CCM. Wafia chama tupo na tupo wengi sasa kuliko ilivyokuwa huko nyuma. Tunafanya kazi 24 Hours na hatulipwi ujira wowote. Tunafanya hivyo kwa mapenzi yetu huku tukiamini kuwa ushindi wa CCM ndiyo faraja yetu. Kama ni lazima wapongezwe, basi nakuomba Mwenyekiti wangu timiza wajibu wako kwa vile utaendelea kuwa Menyekiti wa chama chetu hadi 2017