Kwa vijana walioko Sekondari

Rebeca 83

JF-Expert Member
Jun 4, 2016
14,840
31,583
/Hello JF,

Nimeupitia huu uzi Kozi gani umesoma ambayo huwezi kumshauri mtu mwingine aisome?

Tatizo la ajira limekua changamoto kwa wengi, courses hazijawa kuwa za faida kwa wasomi wengi....na wengi kuona wamepoteza muda huko University/College..

Mimi nashauri kuwe na hata kipindi cha nusu saa kwa week ambacho kitakua incorporated kwenye curriculum ya A-Level students, Katika kipindi kuwe na discussions za employment ONLY.

Kila shule kuwe na Independent Advisor ambae kazi yake ni kufanya research wapi pana opportunities za kazi na hivyo kudiscuss na wanafunzi options walizonazo.....kwa mfano wale wanaosoma mchepuo wa science, advisor atadiscuss na wanafunzi options walizonazo..sio kung'ang'ania Medicine na Engineering peke yake :cool::oops:...

Michepuo mingine hivyo hivyo, wanafunzi wasaidiwe ku explore their interests, identify skills gap, what to expect on chosen career path,and how to match those interests/skills and job descriptions/requiremenrs…..,in this way mwanafunzi kabla ya kuingia Chuo anajua exactly what he/ she wants, what to expect on the course and what will the degree take him/her.

I am sure this will solve the misery among our graduates and save millions of wasted money on courses ambazo hazina matokeo chanya!

Sijui kama website kama hii ipo,lakini ningependa kuona kitu kama hiki.. 👉👉👉Prospects.ac.uk
 
Tuna changamoto za kisera pia kwenye nchi yetu. Leo unaweza kusema programs fulani zina soko zuri la ajira lakini hapo hapo serikali ikabadili sera na ukumbuke mtu ashachukua degree ya icho kitu hawezi tena kurudi chuo kusoma kitu kingine ili aendane na sera ya serikali ya wakati huo.

Mfano: Miaka ya nyuma ualimu ulikua na ajira ya uhakika kwa arts&science ila kwa awamu hii ni sawa tu programs zingine; kwamba unaweza kusoma na bado usipate ajira. Miaka ya 2012-2015 serikali ilidhamiria kuinua sekta ya mafuta na gesi na ikaonekana ni fursa nzuri sana kwa vijana wa kitanzania; wengi sana walienda kusoma iyo program kwa level ya diploma; degree na Masters.

Toka mwaka 2016 ule mradi ulisimama (BG) na hadi leo hatima yake haijulikani; sasa utawaaambia nini walosomea vitu ivyo tena adi ngazi ya Master's? Warudi chuo wakasome tena program nyingine inayolipa kwenye soko la ajira?

Mimi nadhani mfumo wetu wa elimu ubadilishwe ili umjengee uwezo wa kujitegemea muhitimu bila kutegemea sana ajira za serikali. Lakini pia vijana wajengewe uwezo wa kuweza kuajirika kimataifa kwenye sekta zote zikiwamo hizo ulizotaja hapo juu.

Haiwezekani mtu ni Masters/PhD graduate hawezi kujiajiri na kuajiri wengine; hizi tafiti tunazofanya chuo ni za namna gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Education is better than money . discuss?
Always research about employment vary with time , political influance
kwa sababu hatuna vipaumbele vya taifa Mana kila kiongozi anakuja na ndoto zake za usiku kuongoza taifa.


Sent using Jamii Forums mobile app


I agree it varies,but kwa researcher makini will be able to predict future trends..upepo unaelekea wapi...this is ongoing /daily process.. ..
 
Ndio maana huwa naona ni unafiki kudai democrasia,wakati mambo ya msingi na ya wazi kabisa hatujishughulishi nayo kisa hayana kick za kisiasa.
 
Hapo ukiangalia vizuri elimu ya advance ( A- level) naona imepoteza dira kabisa yani , unasoma miaka miwili na hamna professional yoyote unayopata kadri miaka inavyoenda advance inaweza poteza wateja .
Wakati kuna watu wamemaliza form four kaenda kusoma certificate or diploma then degree . These graduates are more marketable in employment market because they have a lot of option to use. Tofauti na wanaopita A- level then degree.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Heavy Metal,
Mkuu post yako nimekuelewa sana, tuna tatizo la kisera,ila hii topic haijalenga tu kwa advisor kuwaambia kazi hii inalipa sana kazi hii hailipi sana,no, as a researcher unatakiwa umpe mtoto options lakini unampa Evidence ili mwenyewe afanye informed choice, Ajira sio malipo peke yake, kuna vitu vingi ikiwemo prestige/reputation ya unapofanyia kazi etc...ndio maana kuna wengine wanafanya kazi labda benki ya Barclays,utakuta wanalipwa ujira mdogo ila wameridhika na kipato chao kidogo wanachopata kwenye kampuni ya jina kubwa...anyway back to the topic tukipata researcher wa kweli akawekwa shuleni lazima a foresee mambo mengi ikiwepo mabadiliko kwenye soko la ajira,

kwa mfano hao waliosoma petroleum engineering, wangeweza kuwa guided kabla hawajachukua hio course probably wangechukua kitu kingine, in addition its easy to predict that any project will have duration of a certain period and have certain number of workers needed,so huyo kijana aliyechukua Petroleum Engineering angeweza ku calculate mwenyewe chances za kupata hio ajira,kama ni slim angeweza kutafuta alternative course badala ya kuchukua Petroleum,

ni mtoto tu kuambiwa ukweli on what to expect...unamwambia Petroleum sio permanent job, na inahitaji watu wachache ..he/she will understand...sio mwandishi mzuri ila natumaini umenielewa
 
Freedom is the mother of innovation.

Kwanza binafsi sishauri kuwekwe nguvu kubwa kwenye suala la watu KUAJIRIWA.

Hakuna kitu kizuri na kinacholeta furaha ya kweli kama kuunda kitu kutoka mwanzo mpaka unakiona kinaleta impact kwenye jamii.

Tatizo kubwa la nchi hii ni WATAWALA.

Yaani kuna kundi la watu wako madarakani, ilimradi wao wanakula na watoto wao hivyo hawaoni umuhimu wowote wa kurekebisha chochote kisichowapa faida.

Leo hata kublog tu au kumiliki YouTube Chanel ni kosa nchi hii.

Hivyo badala kwanza kutoa mawazo ni vizuri kwanza tukatambua hakuna mtu wa KUSIKILIZA.
 
Freedom is the mother of innovation.

Kwanza binafsi sishauri kuwekwe nguvu kubwa kwenye suala la watu KUAJIRIWA.

Hakuna kitu kizuri na kinacholeta furaha ya kweli kama kuunda kitu kutoka mwanzo mpaka unakiona kinaleta impact kwenye jamii.

Tatizo kubwa la nchi hii ni WATAWALA.

Yaani kuna kundi la watu wako madarakani, ilimradi wao wanakula na watoto wao hivyo hawaoni umuhimu wowote wa kurekebisha chochote kisichowapa faida.

Leo hata kublog tu au kumiliki YouTube Chanel ni kosa nchi hii.

Hivyo badala kwanza kutoa mawazo ni vizuri kwanza tukatambua hakuna mtu wa KUSIKILIZA.

Nimekuelewa mkuu...

hasa hapo uliposema hakuna wa kusikiliza...

JamiiForums ipo for 15 years...

Watu kila siku wanatoa ushauri kwa serikali humu..

lakini HAKUNA kinachofanyika

Mambo mengi nadhani yapo kwenye kabati ya JF,which is sad
 
Mkuu post yako nimekuelewa sana, tuna tatizo la kisera,ila hii topic haijalenga tu kwa advisor kuwaambia kazi hii inalipa sana kazi hii hailipi sana,no, as a researcher unatakiwa umpe mtoto options lakini unampa Evidence ili mwenyewe afanye informed choice, Ajira sio malipo peke yake,kuna vitu vingi ikiwemo prestige/reputation ya unapofanyia kazi etc...ndio maana kuna wengine wanafanya kazi labda benki ya Barclays,utakuta wanalipwa ujira mdogo ila wameridhika na kipato chao kidogo wanachopata kwenye kampuni ya jina kubwa...anyway back to the topic tukipata researcher wa kweli akawekwa shuleni lazima a foresee mambo mengi ikiwepo mabadiliko kwenye soko la ajira,kwa mfano hao waliosoma petroleum engineering, wangeweza kuwa guided kabla hawajachukua hio course probably wangechukua kitu kingine, in addition its easy to predict that any project will have duration of a certain period and have certain number of workers needed,so huyo kijana aliyechukua Petroleum Engineering angeweza ku calculate mwenyewe chances za kupata hio ajira,kama ni slim angeweza kutafuta alternative course badala ya kuchukua Petroleum,ni mtoto tu kuambiwa ukweli on what to expect...unamwambia Petroleum sio permanent job, na inahitaji watu wachache ..he/she will understand...sio mwandishi mzuri ila natumaini umenielewa
Nimekuelewa vizuri sana mkuu;
Lakini nani anaetakiwa kuyaandaa hayo na kuyatekeleza? Maana mzazi anapompeleka mtoto shule anakaa na kusubiri mtoto amalize form six aende chuo then agraduate apate kazi basi. Wazazi wangapi wana upeo wa kusoma alama za nyakati na kuwaandaa kisaikolojia watoto wao toka wakiwa sekondari? Tunarudi shuleni na vyuoni sasa; sera yetu ya elimu inasemaje? Hawa wanaofanya hizi tunaita education policy; education calculum development &review hadi huku mwisho kwenye syllabus wote wanaangalia upepo wa nchi unaendaje kwa kipindi hiko. Education researchers wapo wengi sana lakini je sera yetu ya elimu ni ipi ili tuwape nafasi ya kutoa mchango wao. Anyways sijui kama nimetoka nje ya mada, utanirekebisha. Ahsante

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pia suala la kupangiwa kozi ya kusoma bila wewe kupenda huwa sio nzuri.Mtu unakuwa unapenda kozi A au B lakin wao wanakuchagua kwenye kozi F ambayo uliweka tu ili kufidia gape lililoachwa kujaza vyuo au mchepuo.Pia kuna kuna wanafunzi wanapass masomo yote halafubunapangiwa PCM wakati yeye alitaka asome EGM na shule kama haina mchepuo wa EGM huwezi kuhama hivyi utasoma kozi ambayo huipendi sana.

Kwa hiyo hata advance kwa wale wanaofaulu masomo mengi o-levo wapangiwe shule nyingi zenye michepuo tofauti kisha waconfirm shule wanazotaka na michepuo ikijaa basi wanaangalia shule nyingine waliyopangiwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi unajua katika jamii zetu hasa wazazi wanaamini elimu bora lazima mwanafunzi apitie A-Level? Kwamba mwanafunzi akitoka O-Level akaenda moja kwa moja vyuo vya ufundi wao wanaamini uwezo wake ni mdogo ndo maana hajaenda A-Level? Lakini unajua watu wanaosuffer zaidi wakikosa ajira ni wale walienda moja kwa moja university tokea A-Level kuliko hawa walopitia vyuo vya ufundi? So kwenye point yako ya kwamba researchers wawepo mashuleni kuwaguide wanafunzi kuhusu ajira bado itakua na changamoto maana kwa hali ya sasa wahitimu ni wengi mno na ajira hazitoshi; hata km utamguide akikosa ajira hata iyo unayoona haina mshahara mkubwa bado guidance haitomsaidia maana hatakua na ujuzi wowote wa kujitegemea ya alichosomea ili aajiriwe
Point yangu ni kwamba mitaala ibadilike watu wapewe elimu ya kujitegemea tokea huku chini kabsa mwanafunzi ajengwe kua mbunifu ili kuja kua na uwezo wa kujiajiri mwenyewe hata kama atakosa ajira rasmi. Wizara ya Elimu kupitia COSTECH wanaendesha mashindano ya kutambua bunifu mbalimbali za kiteknolojia zinazoweza kutatua changamoto kwenye sekta mbalimbali kama kilimo, afya; maji; na mengine mengi. Ukiangalia washiriki wengi wanatoka vyuo vya ufundi na mtaani na sana bunifu nzuri ambazo zikiendelezwa zitawatoa kibiashara na of course wanapewa pesa za kuendeleza bunifu zao ziende kwenye ubiasharishaji


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Point inakuja;
Hiki wanachokifanya leo COSTECH ndo kilikua kinafanyika miaka ya nyuma kwenye shule za ufundi km MUSOMA TECH; DAR TECH; MOSHI TECH; IFUNDA TECH; TANGA TECH na nyingine nyingi. Kwanini huu mfumo waliuua? Ingefaa kama lengo ilikua kujenga vyuo vya ufundi wangejenga vyuo vingine wakaacha hizi shule ziendelee kuzalisha vipaji vije kuendelezwa huku vyuoni
Tatizo ni sera yetu ya elimu haileweki na kama inaeleweka basi haiheshimiwi na kusimamisha vizuri; lakini pia hairekebishwi kuendana na mazingira na mahitaji ya sasa na baadae
Ahsante

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamani nimependa sana hi maada kwa sababu imekua kichwani kwangu kwa muda mrefu sasa ninaongelea elimu katika mchepuo wa sayansi. Kwa mm naweza kusema A level imekamilika coz mtu akisoma pcm it means amelenga maswala ya engineering lakini ubovu unaanzia hapa kutokana wanafunzi wengi wanaona Kama ni mapito ya kufika chuo lakini sio hivyo science ni nature ambayo umewezesha watu kufanya invention ya vitu mbalimbali ko mpaka tunaweza tukasema form six anaweza akafanya kitu sindio kwa sababu anaelewa nature mfano anaulewa wa electromagnetism kwenye motor electricity kwenye vyombo vya umeme ko mm nadhani kabla hujamwambia mtu aende kusoma nn ili apate ajira mweleze kwanza hayo anayoyataka kuyasoma kuhusu engineering yametoka wapi? Je hao waliyo yaanzisha walikuwa Wawapi? Je uchumi wao unaendana na sisi? Coz naweza kusema 80% ya technology imevumbuliwa marekani Sasa je sisi tunao copy hayo maarifa tunauchumi wa kutosha kumuiga. kwa sababu wao wamevumbua maarifa kwenye frame reference ya uchumi wao wenyewe so na sisi tunabidi kuunda technology zinazoenda na uchumi wetu wenyewe ili kizazi kijacho kiweze kuona tuliyo yafanya sio tulio ya soma.
 
Kingine mbwana niwatu walio tutangulia yaani naweza kusema vijana wasasa hatuna msingi waliochangia walio tangulia utakuta mzazi was 80's alisoma vizuri kipindi hicho na kupata kazi baadala kuanzia mfumo wowote au company yeye anaishia kutafuta hawala hilo swala ni lakutoka kwa mababu na maswala mengine. Lakini kama tukiangalia wenzetu nje Kama vile tunapo muona Jeff bezos kwamba aliacha ya kazi ya msharaha mnono a kuanzisha company yake na baada ya ameajili watu wengi zaidi marekani. Mm nadhani wazee wetu wangefanya hivi tusengekuwa kuwa tunaangaika kazi na ss tukifanya Kama huyu jamaa watoto wetu hawata teseka
 
Tuna changamoto za kisera pia kwenye nchi yetu. Leo unaweza kusema programs fulani zina soko zuri la ajira lakini hapo hapo serikali ikabadili sera na ukumbuke mtu ashachukua degree ya icho kitu hawezi tena kurudi chuo kusoma kitu kingine ili aendane na sera ya serikali ya wakati huo.

Mfano: Miaka ya nyuma ualimu ulikua na ajira ya uhakika kwa arts&science ila kwa awamu hii ni sawa tu programs zingine; kwamba unaweza kusoma na bado usipate ajira. Miaka ya 2012-2015 serikali ilidhamiria kuinua sekta ya mafuta na gesi na ikaonekana ni fursa nzuri sana kwa vijana wa kitanzania; wengi sana walienda kusoma iyo program kwa level ya diploma; degree na Masters.

Toka mwaka 2016 ule mradi ulisimama (BG) na hadi leo hatima yake haijulikani; sasa utawaaambia nini walosomea vitu ivyo tena adi ngazi ya Master's? Warudi chuo wakasome tena program nyingine inayolipa kwenye soko la ajira?

Mimi nadhani mfumo wetu wa elimu ubadilishwe ili umjengee uwezo wa kujitegemea muhitimu bila kutegemea sana ajira za serikali. Lakini pia vijana wajengewe uwezo wa kuweza kuajirika kimataifa kwenye sekta zote zikiwamo hizo ulizotaja hapo juu.

Haiwezekani mtu ni Masters/PhD graduate hawezi kujiajiri na kuajiri wengine; hizi tafiti tunazofanya chuo ni za namna gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
"Haiwezekani mtu ni Masters/PhD graduate hawezi kujiajiri na kuajiri wengine; hizi tafiti tunazofanya chuo ni za namna gani?"

Mkuu umeongea jambo la msingi sana. Kweli kuna sehemu tunakosea siyo siri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Freedom is the mother of innovation.

Kwanza binafsi sishauri kuwekwe nguvu kubwa kwenye suala la watu KUAJIRIWA.

Hakuna kitu kizuri na kinacholeta furaha ya kweli kama kuunda kitu kutoka mwanzo mpaka unakiona kinaleta impact kwenye jamii.

Tatizo kubwa la nchi hii ni WATAWALA.

Yaani kuna kundi la watu wako madarakani, ilimradi wao wanakula na watoto wao hivyo hawaoni umuhimu wowote wa kurekebisha chochote kisichowapa faida.

Leo hata kublog tu au kumiliki YouTube Chanel ni kosa nchi hii.

Hivyo badala kwanza kutoa mawazo ni vizuri kwanza tukatambua hakuna mtu wa KUSIKILIZA.
"Freedom is the mother of innovation."

Umemaliza mkuu, tatizo ni utayari wa kulipia gharama za kutafuta huo uhuru ndo shughuli ilipo hapo, siyo rahisi ndo maana wengi wanakimbilia kuajiriwa na wachache kuweza kumudu na kuanzisha shughuli zao.

Penye nia Pana njia, yeyote anaweza kufanya, naamini.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom