S.M.P2503
JF-Expert Member
- Nov 25, 2008
- 2,088
- 3,665
Mbunge anasema na au anakana kwamba yeye si Raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania “Mtanzania”.
Sasa Humo Bungeni anafanya nini?
Hatuna Nchi inayoitwa Zanzibar wala nchi ya Tanganyika. Tuna Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, “ Tanzania”
Sasa kama yeye ni Mzanzibar na hatuna nchi hiyo, humo ndani kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anafanya nini? Kiti cha Speaker kingefaa kimtoe nje pale pale kwa kauli yake mwenyewe kwamba hapokei taarifa ya yeye ni raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kiti cha Speaker mumepwaya sana maana, Hatuna dual nationality, tuna Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mtu anasema na anakana kwamba yeye sio Raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ( Principle of legal estoppel), sasa kwa nini aendelee kuwemo humo Bungeni?
Hatuna dual nationality, hakuna raia wa Burundi, Rwanda au nchi ya “Zanzibar” anayeweza kuwemo Humo Bungeni.
Ni Raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pekee anayeweza kukaa humo, vinginevyo ni magumashi tu, bila chenga chenga na mkosi ni Mkosi tu- Haijalishi unatokea wapi.
Povu ruksa bila Matusi.