maramia
JF-Expert Member
- Jul 17, 2015
- 2,030
- 1,345
Nina wasi wasi mkubwa suala hili la uteuzi wa viongozi likiachwa likaendelea kama linavyoonekana litaipeleka nchi hii pabaya sana.
Kwa mfano, kuteuliwa kwa maDAS kwa namna walivyoteuliwa ni hatari sana tena zaidi ya hatari, watu wanateuliwa halafu ndiyo vinaitishwa vyeti kuona cv zao, kweli Rais anaweza kuteua watendaji wa serikali kwa kuangalia utendaji wa kisiasa?
Naomba wanasheria wetu waliangalie suala hili kama halikukiuka misingi ya utawala bora au kukiuka katiba?
Nijuavyo mimi ofisi ya DAS ni ya kiutawala zaidi inayosimamia sheria na taratibu za utumishi katika wilaya, kwa hiyo isingefaa wakateuliwa wapiga debe wa chama katika chaguzi kwa kazi kama hiyo, kazi ambayo tangu huko nyuma imekuwa ikihitaji elimu ya utawala ya kiwango cha juu toka toka vyuo kama Mzumbe n.k
Inawezekana huu ni mkakati wa mapema wa mheshimiwa Rais kuanza kujipanga mapema kwa uchaguzi wa 2020 akizingatia msemo wa mwisho wa uchaguzi mmoja ndiyo mwanzo wa uchaguzi mwingine.
Naamini pia kwamba uteuzi huu haukuzingatia uwezo wala tija kwa taifa uliojikita zaidi katika ushabiki wa kichama ambao haukufanywa kisayansi na menejimenti ya utumishi na kama umefanywa ni kwa njia ya shinikizo fulani la chama ili kujipanga.
Hivi kama mambo yatafanywa kwa namna hii hawa wasomi wetu wenye vyeti na taaluma zao za utawala na uongozi lakini wenye itikadi tofauti tofauti za vyama watafanya kazi gani?
Nasema hivyo kwa sababu kwa mujibu wa ufukunyuku wangu maDAS wote walioteuliwa ni makada na wakereketwa wa CCM.
Hali hii inatoa picha kwamba tusipoangalia huko mbele tuendako tunaweza kujikuta hata waalimu, waganga, askari n.k wanaajiriwa kwa vigezo vya uanachama wa vyama vya siasa ili kujihakikishia uhakika wa ushindi katika chaguzi nyingine zijazo.
SIASA NI UJANJA NA USHINDI NI MIKAKATI.