Mwenzenu sijui ni ushamba, sijawahi kukubali matumizi ya hili neno...Zamani nilifikiri linatumika kwa wasichana ambao hawajaolewa na wapo below 30 hivi kumbe hata wake za watu nao ni mademu? Na Bibi wa miaka 60 naye ni demu? Siku nyingine mtawaita Mama zetu (na wenu pia) Mademu, lol!! Samahanini kwa ushamba wangu nilikuwa natafuta pa kutolea hili donge na leo hatimaye nimepata nafasi hapa. Back to the topic..Huyo Shemeji yako (Mke wa Mwanaume mwenzio) au "demu" kama ulivyomwita alikufuata au wewe ndio ulimfuata? Mimi nikija kamata mtu ananiibia Mke lazima nimfanyie castration ili asiendelee kutamani wake za watu. Brother "do unto others as thy wanteth others to do unto you" Full stop!