Kwa upole naomba kuuliza

Kwa upole naomba kuuliza

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,116
Reaction score
34,960
Kuna kiongozi mmoja wa ngazi ya juu ya kanisa, ametangaza kustaafu, kulitumikia kanisa akidai kuwa umri wake umeenda, ana miaka 85.

leo hii, asubuhi, kuna kiongozi mmoja wa ki-afrika, anadai kuomba kuongezewa kipindi kingine cha uongozi, amesema bado ananguvu za kuongoza umri wake ni miaka 89.

naomba maoni yenu
 
Waafrica hatujaweza kutengeneza pension schemes za kuweza kuwashawishi viongozi wetu kwamba wakistaafu watakuwa salama kipesa. (Yaani viongozi wa kiafrica wanaogopa sana njaa).

Pili ni tatizo la kutenda uovu wakiwa madarakani - kwa viongozi wengi wamekuwa waovu na wanaogopa sana kulipizwa visasi na wale watakaochukua madaraka. Kwa hiyo njia salama ni kung'ang'ania madarakani.

Tatu, ni wengi wa viongozi kutokuwa na akili - haiwaingii akilini kuwa kuna maisha nje ya uongozi.(wengi hawajui wakistaafu watafanya nini). Hivyo uongozi ni ajira na ni starehe pia.
 
Mkuu.
Huyo mu-afrika hawezi pata huo uongozi. FYI kwa miaka mingi sana makaldinali walikuwa wanakitaka hicho cheo, lakini huyu Pope Benedict amajifunza kuwa hicho cheo wanaostaili ni waItaly and not otherwize.
Kila kitu kina misingi yake, watu waache kukurupuka, wasifikiri uPope ni sawa na kuchagua rais...
 
Kwani wewe kauli zao umezichukua kama niza kweli?. Hivi unajua kilichoko nyuma ya pazia?.
Hujui kama walikufunga mdomo na hawapendi uwe kimbele mbele pale waliposema, Ya Kaizari mwachie Kaizari na Ya Mungu mwachie Mungu.
Ya wanasiasa waachie wanasiasa na ya kanisa liachie kanisa. DESINO.
 
Mkuu.
Huyo mu-afrika hawezi pata huo uongozi. FYI kwa miaka mingi sana makaldinali walikuwa wanakitaka hicho cheo, lakini huyu Pope Benedict amajifunza kuwa hicho cheo wanaostaili ni waItaly and not otherwize.
Kila kitu kina misingi yake, watu waache kukurupuka, wasifikiri uPope ni sawa na kuchagua rais...

Mkuu umemuelewa mtoa mada?
 
The born politician wants nothing but power, believes in nothng but power. All his energies are concentrated on a thing that will enable him to become a leader.
 
Mugabe alihakikisha Banana anapotea kabisa,hii ndio sababu kubwa inayomkwaza,
 
Kuna kiongozi mmoja wa ngazi ya juu ya kanisa, ametangaza kustaafu, kulitumikia kanisa akidai kuwa umri wake umeenda, ana miaka 85.

leo hii, asubuhi, kuna kiongozi mmoja wa ki-afrika, anadai kuomba kuongezewa kipindi kingine cha uongozi, amesema bado ananguvu za kuongoza umri wake ni miaka 89.

naomba maoni yenu

Mkuu, kitalaam sioni tatizo hapa. Umri unaweza kuwa sawa lakini kukawa na utofauti mkubwa sana katika uwezo wa mwili kufanya kazi. Uwezo wa mtu kufanya kazi ni function ya vitu vingi not only age.
 
unaweza kuwa na umri mkubwa huku kwetu Afrika lakini unanguvu na akili yako inatenda ya umri wa miaka 30-50. si wajua ngo'mbe hazeeki maini...?
 
Waafrica hatujaweza kutengeneza pension schemes za kuweza kuwashawishi viongozi wetu kwamba wakistaafu watakuwa salama kipesa. (Yaani viongozi wa kiafrica wanaogopa sana njaa).

Pili ni tatizo la kutenda uovu wakiwa madarakani - kwa viongozi wengi wamekuwa waovu na wanaogopa sana kulipizwa visasi na wale watakaochukua madaraka. Kwa hiyo njia salama ni kung'ang'ania madarakani.

Tatu, ni wengi wa viongozi kutokuwa na akili - haiwaingii akilini kuwa kuna maisha nje ya uongozi.(wengi hawajui wakistaafu watafanya nini). Hivyo uongozi ni ajira na ni starehe pia.
Ndugu tetere,
Natofautiana kidogo nawe,katika kipengere kwamba Pension scheme inachangia. Hapana. Ni ubinafsi na umangimeza uliopindukia. Hebu ona "Zee" kama Robert Mugabe? Kina Mubarak Hussein (kabla hajafurumushwa)? Hapa kwetu wapo tele humo maofisini wanapeana mikataba ya baada ya kustaafu.. and mind you,most of them wapo sawa kifedha. Ni Uhuni tuu. Ni culture ya ubinafsi uliopindukia,kudhani uongozi (utawala)/ Mamlaka ni stahili yake pekee,hata bila ku-deliver. Benedict xvi ameona changamoto za kukua kwa Idara anayoiongoza zimekuwa nyingi na zinahitaji Afya ya Akili na nguvu.
 
Last edited by a moderator:
Mugabe anataka kufia jukwaani? Loh! Aache hizo.
 
Back
Top Bottom