Kwa ujinga/uelewa mdogo wa waafrika, udikteta utatusaidia kuleta maendeleo haraka kuliko demokrasia

Pro Magufuli Wa 47

Senior Member
Mar 5, 2016
188
58
Nakumbuka miaka ya 1980's nilipokuwa shuleni, mwalimu wetu wa siasa/uraia (sijui kama bado lipo) alitufundisha maana fupi ya Demokrasia kama "serikali ya watu" ukidadavua utakuta Kumbe:

"Ni mfumo wa siasa unaotegemea watu, kupanga na kuamua jinsi ya kujitawala kwa misingi ya uhuru na haki, kulingana na mazingira na kwa ridhaa ya watu"

Je, Demokrasia yetu ni yetu? Au ya kuazima?

Demokrasia lazima iendane na mazingira, mabadiliko yanayotokea, na watu wenyewe.
Ujinga ni pale Waafrica tunapojaribu kulazimisha aina ya Demokrasia ya Wamarekani au wafaransa ifanye kazi kwenye jamii zetu.

Mwisho wa siku unakuta kila jambo haliendi, migogoro isiyokwisha, maandamano, na upotezaji mkubwa wa muda

Hatupaswi kuiga kila kitu toka kwa wazungu, Kama wao Democrasia yao wameifanya kuwa flexible kutokana na mazingira au nyakati zao.

Kwanini sisi tusibadirike hata kama tutapigiwa kelele na wao?
Why should Africa listen to the hypocritical criticism of its three-term leaders? | Eric Joyce
1-Hapo unaona jinsi sisi tunavyopigiwa kelele kujiongezea miaka ya kukaa madarakani wakat mataifa makubwa mengi e.g Germany wamefanya kitu kama hicho na bado mataifa yao yanasonga mbele.

2-Pitia kwenye social network za waTanzania uone jinsi wanavyotukanana na kudhararishana kutwa Hadi aibu, wakati kuna mengi tungeweza kufanya kupitia huko.

3-Tazama Mahakama zetu zilivyobize pindisha sheria zinavyopindishwa wakati Viongozi wetu ni kweli wameshiriki kwenye vitendo vya ubadhirifu.

4-Tazama ghalama zinazotumika kufadhili vyama vya siasa au maridhiano ya kisiasa.
Ona pesa zinazotumika kupooza wabunge hata kama jambo ni jema au muda unaotumika Bungeni kupitisha mipango ya serikali au kubishana siasa.

5- Tazama Wazungu wanavyotumia vyombo vyao kama ICC kinafiki kwa kubagua nani ahukumiwe nani asihukumiwe, kupindisha sheria, kutoa au kutokutoa hukumu kutegemea mahusiano yao na nchi zenyewe au kiongozi wenyewe.
Mfano:Kenyatta na Rutto juzi.

6- Na mwisho na kibaya zaidi ni UJINGA mkuu tulionao Watanzania wa kushobokea Viongozi Mafisadi kwa kuangalia itikati, Imani, ukabila au hata ukanda na sio kutanguliza Maslahi ya nchi.
Matokeo yake ni Viongoz kuendelea kutuchezea akili kwa kujua fika wana Wajinga watawaunga mkono na kuwatetea.

Tumeona ya kina Chenge kutandikiwa kanga, Lowassa kutakaswa na kuwa malaika, Dau kutetewa kisa alituchangia kujenga Msikiti na ujinga mwingine mwingi.
Kwa demokrasia ya US hatutaweza chomoka, ni Lazima tupike ya kwetu ama kutumia Udikteta wa kwetu ili nchi isonge kama China.

Na itafika wakati Demokrasia ya 100% itatufaa lakini si leo.
Mwl Mjema
 
Maendeleo hayaletwi na Demokrasia yanaletwa na kufanya kazi .Shida ya Afrika ni maendeleo , je ww unafanya kazi ? hilo ndo swali la msingi mengine ni porojo
 
Tungejifunza kwanza kwa hao wazungu kwa waliyoyapitia hadi kufika pale walipo.
 
Ukiwapa demokrasia wapumbavu na malofa huwezi kuyaona maendeleo!!! Watalazimisha mawazo yao mafupi kwa kutojua kuwa ni mafupi, yaheshimiwe, yakikataliwa, utasikia, oh fulani, dikteta!!! Hapa kazi tu ndg!!
 
Back
Top Bottom