Kwa ujinga huu ni ndoto Tanzania kuwa 'Super Power' kwenye ukanda wa EAC

Siasa zetu za ndani zimetupumbaza hadi zimeanza kuvuka mipaka, ni ujinga.

Kwa kitendo hiki CCM wamefaidika nini kwa vile nafasi bado ni za Chadema na inawezekana wakarudishwa wale wale wakaongezewa mwanamke mmoja tu CCM wakalazimishwa kuchagua wawili kati ya watatu.
CCM wanatuangusha sana mkuu.
 
Hapa solution chadema tujipange kuongea viti bungeni.haya makondoo ya ccm yanatumia vibaya wingi wao pale mjengoni.
 
CCM hawaangalii uwezo wa mtu katika kutetea maslahi ya taifa kwa mwanaume inaangaliwa pesa ( rushwa) na mwanamke inaangaliwa chupi baaas
 
No wonder kwanini Tanzania tunaendelea kuburuzwa na kutengwa kwenye EAC, kama tutaendelea kupeleka wawakilishi EALA kwa mihemko ya kisiasa, yaani unampeleka Fancy kutetea taifa kufanya lobbying mbele ya wanasheria nguli kutoka Kenya, Uganda unawaacha wanasheria wazoefu kina Taslima, Macha kwa vile tu ni wapinzani, unamwacha memba mzoefu Zainabu Kawawa? Unamwacha Wenje kwa vile tu chama chake hakikuleta mwanamke? Unamwacha Makongoro aliyefanya lobbying hadi bomba la mafuta toka Uganda likapita Tanzania? Kweli?

Kwenye suala la ku serve national interests wanaCCM wenzetu hebu tuwe serious kidogo tuondoe uvyama, kule hawaendi kuwakilisha CCM wala Chadema wanakwenda kuwakilisha nchi.

Wenzetu huko Wakenya kwa mfano when comes issue ya kutetea nchi yao wako very serious and strong wanaleta competent representatives ndio maana labda wana maendeleo kutuzidi, sidhani kwenye bunge kama hili huwa wanaleta vitoto vitoto vya kuuza sura kama tunavyofanya sisi, that is why may be Kenya is becoming the super power among member states of the community, wengine tutabaki kulialia tu Kenya wanautumia mlima Kilimanjaro wanachukua watalii wetu kumbe tatizo ni sisi hatuna watu wa ku-defend our national interests. Tubadilike.
Tanzania tulikuwa na bahati ya kumpata Rais wa kwanza (Baba wa taifa) aliyefanya kazi kama Rais wa nchi na kazi ya ziada ya kufundisha wananchi wake mambo mbalimbali. Lakini kwa bahati mbaya uwezo wa uelewa wa wananchi wake haukuwa mzuri, hivyo hawakuweza kumuelewa baba wa Taifa. Matokeo yake ni kuwa wa watu wenye aina fulani ya ujinga, woga, unafiki, ubinafsi, watu wa kupenda kupata upendeleo kwa njia za kujikomba, kujipendekeza na kumbelembele sana. Hapo ndipo tulipokwama kama Taifa. Kiuhalisia hatuna tofauti kati ya wasomi na wasiosoma, wote tunafanana kimawazo na kimatendo. Matokeo yake ni haya tunayoyaona kila kukicha na kituko chake na umasikini ukituandama kila mahali
 
Life is not all about laws guys
Ndg kusema CDM wameambulia zero inaonyesha ni kiasi gani hujui hata wao wabunge wa EAC wanatakiwa wangapi na wanapatikana vipi. piga ua bado nafasi ya wawakilishi toka CDM lazima wawe wawili. Uhakika wagombea wa CDM walionekana wako competent kuliko wengine wote, cha kushangaza wale wabunge wanaenda kutetea maslahi ya TZ hakuna haja ya kuingiza hizi siasa za majitaka. Nimeona uwezo mdogo sana wa baadhi ya wabunge wa EAC waliopita yaani itakuwa ni aibu huko, huyo Nkuhi na Habib Mnyaa uwezo wao mdogo hata kwa kujieleza tu unagundua hawawezi kupambana.
 
Ndio mkuu, wabunge wa CCM wangekuwa na mantiki kama kina Macha na Wenje wangekuwa wanakwenda kufanya kampeni ya Chadema lakini wanakwenda kutetea mlima Kilimanjaro usitumike hovyo, kulinda heshima ya Mtanzania awe Chadema au CCM, kutetea aridhi isitumiwe hovyo na wageni. Sasa unapopeleka mtu ambaye hata kujieleza hawezi unamkomoa nani.
Nia nzuri utetezi dhaifu.
 
CCM hawaangalii uwezo wa mtu katika kutetea maslahi ya taifa kwa mwanaume inaangaliwa pesa ( rushwa) na mwanamke inaangaliwa chupi baaas
Nahisi kutakuwa na matatizo mahali fulani, haiwezi kueleweka ikiwa kuna wabunge wengi tu wa CCM bungeni lakini Mhe Rais haoni kama wana sifa za kutosha na kumlazimu kuteuwa wengine ili wamsaidie ambao wengi amewapa uwaziri katika wizara mbalimbali.
 
Siasa zetu za ndani zimetupumbaza hadi zimeanza kuvuka mipaka, ni ujinga.

Kwa kitendo hiki CCM wamefaidika nini kwa vile nafasi bado ni za Chadema na inawezekana wakarudishwa wale wale wakaongezewa mwanamke mmoja tu CCM wakalazimishwa kuchagua wawili kati ya watatu.
Kwa nn hawakuleta watatu toka mwanzo, demokrasia imechukua mkondo wake wa kulaumiwa ni mbowe
 
Kwa nn hawakuleta watatu toka mwanzo, demokrasia imechukua mkondo wake wa kulaumiwa ni mbowe
Demokrasia kwa vyama vyenye itikadi tofauti?! Bunge kazi yao ni kupeleka majina Eala ndio mana viti vikagawiwa kichama...wanachofanya ccm ni uhuni na UBASHITE
 
Mlishangiria Ubinafsi
mkaona kama ACT itapata si chama cha Tanzania
leo mmeanza kulialia
hahaha nabado
mtulie dawa iwaingie

Dawa ya moto ni moto
Safi sana wabunge
Chadema wameambulia ZERO
Wewe kweli nyumbu unashangilia nn?Wa hovyo ww bado upigwe bei Na mkeo Tu maana uwaza kwa makalio
 
Akili ndogo za kina Prof Maji Mafupi,Bwege, zinapongoza akili kubwa za kina Masha na wenje unategemea nini?
 
Natamani ifike mahali utaratibu wa kuwapata hawa Wabunge ubadilishwe, siasa zikae pembeni maana when it comes to jambo lolote likitumika bunge letu huwa ni vituko, hata mchakato wa Katiba mpya uliharibika baada yakuwafanya Wabunge kuwa sehemu yake, wapo wataalam na wazoefu haswa wanaoacha kutumika kwa sababu tu hawana vyama
 
Back
Top Bottom