Uchaguzi 2020 Kwa ubabaishaji huu wa CHADEMA hawapaswi kupewa madaraka

Sep 1, 2020
86
41
KWA UBABAISHAJI HUU WA CHADEMA HAWAPASWI KUPEWA MADARAKA

Ndani ya CHADEMA kumekuwa na malalamiko na madukuduku ya muda mrefu sana ya wanachama na viongozi mbalimbali kuhusu namna mambo mbalimbali yanavyoendeshwa ndani ya Chama hicho. Mpaka sasa kumekuwa na giza zito la hofu baada ya Chama hicho kugeuka kuwa kikundi cha watu wachache wenye mamlaka na nguvu ya kuamua jambo lolote ndani ya Chama na kila anayejaribu kuhoji amekuwa akikumbwa na majanga na matatizo makubwa sana kama tulivyoona yaliyowapata akina Chacha Wangwe, Slaa na wengine wengi walioumizwa na wanaoendelea kuumizwa kwa sababu ya kuhoji mifumo flan flan isiyoenda sawa.

Leo Chadema wanakuja wanasema wanataka tuwape madaraka wakati hawajajibu na kuwaeleza Watanzania yanakoenda mabillion ya ruzuku ya Serikali kwenye Chama hicho. Licha ya Chadema kuwa Chama kikuu cha Upinzani na kinachopata ruzuku kubwa ya Serikali lakini mpaka Leo Chama hiko kimekuwa ombaomba kinachotanga kila uchao kuchangisha michango kwa Watanzania. Wapi mabillion ya ruzuku yanaenda? Tunawaaminije kuwapa madaraka makubwa namna hii kwa tabia zenu hizi?

Leo tunaelekea Uchaguzi mkuu halafu Chadema wanataka tuwape nchi kwa ufisadi na janja janja hii wanayoifanya kwenye mali ndogondogo tu za Chama hizi? Je kesho tuwape nchi hawatauza migodi yetu kwa vipande vya shilingi hawa.

Wapi hela za makato ya wabunge zinaenda? Chadema katika kuhakikisha kinajiendesha kimekuwa na utaratibu wa kuwakata wabunge wake mamillion ya fedha kutoka kwenye mishahara yao. Wabunge wa majimbo hukatwa laki 5 kila mwezi na wale wa Viti maalum hukatwa Million 1 na nusu. Licha ya Mabillion hayo ya makato ya wabunge kuingia kwenye akaunti za Chama lakini mpaka leo haieleweki wala hakuna anayejua zinakoenda fedha hizo au walau kujua kiasi, matumizi wala baki ya fedha hizo. Wabunge wachache wanaong'aka na kuhoji jambo hilo wamekuwa wakiishia kuitwa vibaraka wa CCM, wasaliti na kufukuzwa kwenye Chama. Hawa ndo tuwape madaraka?

Leo Chadema wanataka tuwape nchi kwa usafi gani na wameanza lini? Kama Mamillion tu haya ya Wabunge yanawatoa roho na imani, Je kesho na keshokutwa tukiwapa migodi yetu, hifadhi zetu, mazao yetu na nchi yetu yote hii iliyobarikiwa kila kitu itakuwaje? Hawatauza kulekule wanakotumikia kila uchao. Chadema tusidanganyane.

Na Je fedha za wahisani nazo? Mana hazijulikani na wala hazitangazwi. Kama Chadema wanavyojinasibu kuwa na marafiki wengi nje ya nchi tulitegemea wawe wakweli na waeleze urafiki wao huo uko kwenye nini na wanafaidika ama wanapata nini. Mpaka Leo hakuna anayejua. Kama hela wanapata ni ngapi na ziko wapi? Hawa ndo tuwape nchi? Mmmh!!!

Michango ya wanachama inaenda wapi? Wanachama wa Chadema na Watanzania wote wanapaswa kujiuliza maswali mengi sana kwa hawa wenzetu wanaojinasibu kuwa wanataka madaraka. Kila siku tunaona wakichangisha fedha kwenye mikutano na shughuli zao lakini sijui kama yupo anayejua fedha hizo zinaishia wapi?

Hatusikii idadi yake wala mwishoni kuambiwa zimetumikaje na kama ziliisha au zimebakije kama zilibaki. Mbona hao wanaowaponda tunasikia wakisema kuhusu fedha za michango kutoka kwa wanachama wake. Sasa hawa Chadema wanaficha nini na kama wanaficha zinaenda wapi na kwa nani?

Watanzania tuamke. Tuepuke wajanja wanaotaka nchi yetu kwa mikate yao wenyewe.

Kijana Mzalendo.
 
Sasa uko kwenye kamati kuu mpaka ujue mapato na matumizi?Au wewe ni mjumbe wa mkutano mkuu?Au CAG anasemaje?
Hebu tuletee basi na mchanganuo wa mabilioni ya ruzuku wanayopata CCM!
 
KWA UBABAISHAJI HUU WA CHADEMA HAWAPASWI KUPEWA MADARAKA

Ndani ya Chadema kumekuwa na malalamiko na madukuduku ya muda mrefu sana ya wanachama na viongozi mbalimbali kuhusu namna mambo mbalimbali yanavyoendeshwa ndani ya Chama hicho. Mpaka sasa kumekuwa na giza zito la hofu baada ya Chama hicho kugeuka kuwa kikundi cha watu wachache wenye mamlaka na nguvu ya kuamua jambo lolote ndani ya Chama na kila anayejaribu kuhoji amekuwa akikumbwa na majanga na matatizo makubwa sana kama tulivyoona yaliyowapata akina Chacha Wangwe, Slaa na wengine wengi walioumizwa na wanaoendelea kuumizwa kwa sababu ya kuhoji mifumo flan flan isiyoenda sawa.

Leo Chadema wanakuja wanasema wanataka tuwape madaraka wakati hawajajibu na kuwaeleza Watanzania yanakoenda mabillion ya ruzuku ya Serikali kwenye Chama hicho. Licha ya Chadema kuwa Chama kikuu cha Upinzani na kinachopata ruzuku kubwa ya Serikali lakini mpaka Leo Chama hiko kimekuwa ombaomba kinachotanga kila uchao kuchangisha michango kwa Watanzania. Wapi mabillion ya ruzuku yanaenda? Tunawaaminije kuwapa madaraka makubwa namna hii kwa tabia zenu hizi?

Leo tunaelekea Uchaguzi mkuu halafu Chadema wanataka tuwape nchi kwa ufisadi na janja janja hii wanayoifanya kwenye mali ndogondogo tu za Chama hizi? Je kesho tuwape nchi hawatauza migodi yetu kwa vipande vya shilingi hawa.

Wapi hela za makato ya wabunge zinaenda? Chadema katika kuhakikisha kinajiendesha kimekuwa na utaratibu wa kuwakata wabunge wake mamillion ya fedha kutoka kwenye mishahara yao. Wabunge wa majimbo hukatwa laki 5 kila mwezi na wale wa Viti maalum hukatwa Million 1 na nusu. Licha ya Mabillion hayo ya makato ya wabunge kuingia kwenye akaunti za Chama lakini mpaka leo haieleweki wala hakuna anayejua zinakoenda fedha hizo au walau kujua kiasi, matumizi wala baki ya fedha hizo. Wabunge wachache wanaong'aka na kuhoji jambo hilo wamekuwa wakiishia kuitwa vibaraka wa CCM, wasaliti na kufukuzwa kwenye Chama. Hawa ndo tuwape madaraka?

Leo Chadema wanataka tuwape nchi kwa usafi gani na wameanza lini? Kama Mamillion tu haya ya Wabunge yanawatoa roho na imani, Je kesho na keshokutwa tukiwapa migodi yetu, hifadhi zetu, mazao yetu na nchi yetu yote hii iliyobarikiwa kila kitu itakuwaje? Hawatauza kulekule wanakotumikia kila uchao. Chadema tusidanganyane.

Na Je fedha za wahisani nazo? Mana hazijulikani na wala hazitangazwi. Kama Chadema wanavyojinasibu kuwa na marafiki wengi nje ya nchi tulitegemea wawe wakweli na waeleze urafiki wao huo uko kwenye nini na wanafaidika ama wanapata nini. Mpaka Leo hakuna anayejua. Kama hela wanapata ni ngapi na ziko wapi? Hawa ndo tuwape nchi? Mmmh!!!

Michango ya wanachama inaenda wapi? Wanachama wa Chadema na Watanzania wote wanapaswa kujiuliza maswali mengi sana kwa hawa wenzetu wanaojinasibu kuwa wanataka madaraka. Kila siku tunaona wakichangisha fedha kwenye mikutano na shughuli zao lakini sijui kama yupo anayejua fedha hizo zinaishia wapi? Hatusikii idadi yake wala mwishoni kuambiwa zimetumikaje na kama ziliisha au zimebakije kama zilibaki. Mbona hao wanaowaponda tunasikia wakisema kuhusu fedha za michango kutoka kwa wanachama wake. Sasa hawa Chadema wanaficha nini na kama wanaficha zinaenda wapi na kwa nani?

Watanzania tuamke. Tuepuke wajanja wanaotaka nchi yetu kwa mikate yao wenyewe.

Kijana Mzalendo.
 
Mmeambukizana ujinga uko kwaiyo ukiwa CCM tu ndiyo MZALENDO?

futeni vyama vyote vya upinzani sasa mbaki pekeyenu wazalendo.
 
Ila kuna vingine vinafikirisha iwapo unataka kweli. Jana nilikua naangalia mahojiano ya mh.Lissu kuna ujumbe nikapata kwamba Chadema kwa nafasi kama hii ya Uraisi na akipata Uraisi kwa katiba yao anatakiwa awe anaripoti kwa mwenyekiti wake wa chama juu ya mienendo yake kwake. Sasa hii ni kama kijana umeoa alaf unakaa kwenu nyumba moja na wazazi wako hapo lazima uulizwe unarudi mida gani?, Unajiona umekua eh?
 
Wanapokea Ruzuku,

Wanachangisha wabunge kila mwezi,

Wanachangisha wananchi kwenye mikutano yao,

Wanaomba fedha toka kwa mabeberu.

Lakini bado hawana hata makao makuu yao.

Ofisi za Kanda zipo hoi.

Chadema kuna mashine ya kutafuna fedha,

Pale kuna ubadhirifu mkubwa sana ndio maana uongozi wa juu ni watu wale wale kwa muda mrefu ili kuficha madudu yao, mtu nje ya mtandao wao hawezi kuwa sehemu ya uongozi.

Chama kimejaa ufisadi.
 
Hawapo serious na kutaka kuiongoza tanzania kabisa
 
Ila kuna vingine vinafikirisha iwapo unataka kweli. Jana nilikua naangalia mahojiano ya mh.Lissu kuna ujumbe nikapata kwamba Chadema kwa nafasi kama hii ya Uraisi na akipata Uraisi kwa katiba yao anatakiwa awe anaripoti kwa mwenyekiti wake wa chama juu ya mienendo yake kwake. Sasa hii ni kama kijana umeoa alaf unakaa kwenu nyumba moja na wazazi wako hapo lazima uulizwe unarudi mida gani?, Unajiona umekua eh?
Amini nakwambia kam ikitokea lissu kashinda ataeongoza serekali ni mbowe na sio lissu.
ingawa lissu kushinda hayo ni maajabu yasiyoweza kutokea
 
Umetumia nguvu nyingi kuandika kupinga chama ambacho ruzuku yake haifiki Hata Milion 300 kwa mwezi, vs chama ambacho kina serikali

Maneno yote hayo unaongelea chama ambacho kwa miaka 5 kipo gizani, kimya kabisa vs chama ambacho kwa miaka 5 kinaongea tu sera zake

Mpaka hapo means ccm mna hofu kubwa sana na chama ambacho mbele za watu mnakiita dhaifu
 
Ila kuna vingine vinafikirisha iwapo unataka kweli. Jana nilikua naangalia mahojiano ya mh.Lissu kuna ujumbe nikapata kwamba Chadema kwa nafasi kama hii ya Uraisi na akipata Uraisi kwa katiba yao anatakiwa awe anaripoti kwa mwenyekiti wake wa chama juu ya mienendo yake kwake. Sasa hii ni kama kijana umeoa alaf unakaa kwenu nyumba moja na wazazi wako hapo lazima uulizwe unarudi mida gani?, Unajiona umekua eh?
Hahahhaa......waendelee kuwaburuza wenzao kwenye chama ila sio wa tanzania
 
Kama wanataka kuongoza nchi wajenge kwanza Chama chao,Nchi haiwezi kuendeshwa kihuni kama chama chao
Yaani ukiwaangalia tu unasema hapa tunaenda kupigwa.

Matapeli huwa wanakuwa na hulka ya kujieleza sanaaa,

Basi jamaa nao wako hivyo hivyo maneno meeengi mpaka mtu unashtukia kuwa hapa hakuna usalama kabisa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom