Kwa Uamuzi Huu wa CCM!, CCM Sasa ni Chama Cha Hovyo Hovyo!. Kukitegemea 2015 ni Majanga!.

Pasco unajuaje kuwa hawakusomewa makosa yao kikamilifu na wao kujitetea. Kumbuka waliitwa kuhojiwa na wao walipotoka walijidai wamekwenda kunywa kahawa na kushauriana, Kasoro Mh Membe. Waulize taratibu watakuelezea kwa uwazi kilichojiri.
 
Eeee bwana hee umekuwa mkali mno. Pamoja na kwamba nakubaliana na hoja zako lakini umekuwa mkali mno, duh! Lazima una mtu wako katika hawa, sio bure walai!
 
Pasco
Nanukuu sehem ya maelezo yako point namba4
"Huku sio kutendea haki wale ambao hawako kwenye harakati, at the expenses za wenye harakati!"
Mwisho wa kunukuu.

Swali, hivi hao ambao hawako kwenye harakati ni akina nani?

Umewezaje kutambua hilo?

Help tafadhali.

Sent from my iPhone using JamiiForums app.
 
Last edited by a moderator:
Hiyo ni hadaa tu ya ccm , hamna maamuzi ya maana hapo. Kampeni zilishaanza kitambo sana , toka Jamaa yako ajiuzulu uwaziri mkuu alinzalianzisha , sasa leo hii wanakurupuka nini kutoa maamuzi yasiyokuwa na tija?
 
Kilichofanywa na ccm ni mwendelezo wa unafiki wao wa kuwahadaa watz kwamba wamechukua hatua ilhali hakuna kitu wanachofanya. Hivi EL nategemea kugombea nafasi gani ndani ya miezi 12 kuanzia jana!!!? Total hipocrite!

Hili ni karipio la CCM kwa wana CCM wake sio Serikali, wewe inakuhusu nini mpaka ujifanye Kusikitika? Au ndo upo kwenye kundi la mliotunza Kadi za Chama ili ziwasaidieni mbele ya Safari? Hata Bosi wako apewa Option ya kugombea Urais kupitia CCM au Hiko cham chake alichopo basi angechagua CCM kwa kuwa anajua CCM ilihitaji sera na historia ya utendaji kupata Viti 24 wakati wao walihitaji kila kata moja kupata Chopa ili kujihakikishia ushindi.
 
Pasco ie mleta mada ni kchumia tumbo, njaa. Bwana wake amepigwa stop...hapa ni taifa kwanza pesa baadae

Mkuu ingekuwa Pasco ameleta mada ya kuiponda CHADEMA nina hakika hungemwita mchumia tumbo.... Vijana wanasiasa wametufanya mazuzu kushabikia vyama CCM CHADEMA CUF NCCR na tunaacha kupigania mambo muhimu ya kitaifa na kubaki na ushabiki wa vyama... THE BIG SHOW alishalisema hapa not long ago!!
 
Last edited by a moderator:
Wanabodi,

Nimesoma maamuzi ya CC ya CCM kuhusu wanaotuhumiwa kuanza harakati za kuusaka urais wa 2015.

Uamuzi wenyewe ni huu

  1. Kwa maoni yangu, maamuzi haya ni ya kipuuzi kupita maeleza!. Uamuzi huu unakiiza Chama cha Mapinduzi, katika listi ya vyama vya hovyo kabisa kupata kutokea!.
  2. Kwa vile wahusika ni wanachama wa Chama cha Mapinduzi, na wamevurumishiwa tuhuma mbalimbali za harakati za kuusaka urais, kufikia kiwango cha chama kuitisha kamati ya maadili kuwahoji, kabla ya kufikia hizi stages, ilibidi chama kipate tuhuma specific, hivyo walipoitwa kila mmoja alipaswa kusomewa tuhuma zake specific zikionyesha amevunja kanuni ipi, au kipengele kipi!, ndipo ajieleze!.
  3. Baada ya kupokea tuhuma na maelezo ya majibu, ilipaswa chama kijiridhishe na ushahidi kuhusu kukiukwa kwa tuhuma hizo na ndipo watoe adhabu!.
  4. Tamko hili la CCM ni just a "blanket sweeping statement!", lisilo na any specific kosa, hakuna kanuni iliyofunjwa, na hukumu ni too general, as if its a bunch of thugs, wakati watuhumiwa ni individuals na kila mmoja ame play role yake on his own, kuwaweka wote kwenye tenga moja, na kuwahukumu adhabu moja bila mchanganuo wa makosa yao, hiyo inaitwa hukumu ya "pakacha la samaki", akioza mmoja, wote wameoza!, huku sio kutendea haki wale ambao hawako kwenye harakati, at the expenses za wenye harakati!.
  5. Hata kama ni kweli, kuna watu wameanza harakati za chini chini, jee kuna yoyote aliyetangaza rasmi, expressly kuwa anautaka urais?, iweje CCM i act kwenye maneno ya kutajwa tajwa tuu!. Huu ni uthibitisho CCM ni chama cha majungu, fitna na zengwe, ambapi inayafanyia kazi majungu, fitna na zengwe, na kutoa maamuzi ya kimajungu majungu, kuwafanyia fitna na kutaka kuwapiga zengwe tuu baadhi ya wanaotajwa!.
  6. Naomba kuuliza tena, hivi kuna kosa lolote, mwana CCM yoyote, kuutamani urais?!.
  7. Hivi kuna kosa lolote, mwana CCM yoyote, kutangaza nia ya kuwania urais, wakati utakapowadia ili kutoa fursa kwa wana CCM kumpima?!.
  8. Jee lengo la adhabu hii ni kuwazuia watu wenye uchungu na umasikini wa Tanzania, kuwazuia wasihamasishe maendeleo na moyo wa kujitolea ili wasije wakaonesha huko ni kuusaka urais!.
  9. Niliwahi kusema CCM imechokwa, CCM imeozwa kwa rushwa left, right, from top to down on its roots, yaani imeoza hadi kwenye shina!, inanuka uvundo wa rushwa na vitendo vya ufisadi vilivyokithiri mwanzo mwisho!. Leo inapata wapi, ujasiri wa kuupiga mkwala mbuzi kama huu?.
  10. Uamuzi huu, ni kiashiria cha CCM kuendelea kujiona ni chama dola, hivyo kinatishia nyau ili wale wenye malengo mazuri na taifa hili, wakate tamaa, wanywee na kuwa watumwa wa CCM!
Natoa wito kwa wale wote wenye nia njema na taifa hili, waliochoshwa na umasikini wa Watanzania, walipuuze kabisa tamko hili la CCM, na kuendelea na harakati zao za kuwaletea maendeleo Watanzania, kwa sababu kwa uchaguzi wa 2015, kama daftari la kudumu la kupiga kura litaboreshwa, CCM sio determinant ya rais wa Tanzania, 2015, hivyo nawashauri wandeleze juhudi zao kwa kasi zaidi, ili hata CCM ikiamua kuwatimua kwenye hilo lichama lao rushwa kunuka!, Watanzania wanajua 2015, wanataka nini, wanataka rais gani, mwenye uwezo gani, na kukubalika kwa kiasi gani, akifukuzwa CCM, hata akisimama kama mgombea wa kujitegemea!, tutamchagua tuu!.

CCM iache tisha toto, na kuwatishia nyau watu wakubwa wazima!, na kwa mwendo huu wa CCM, na Chadema ni dhoofu bin taaban!, kwa 2015 mbona itakuwa Majanga?!.

Wasalaam.

Pasco.
NB. Pasco wa jf, sio mwanachama wa chama chochote cha siasa, ila supporter mkubwa wa kupigania Tanzania kupata rais mwenye uwezo ile 2015 kuepuka majanga ambayo tumeishakumbana nayo!.
Mkuu wangu Pasco, mbona kama umedondoka jukwaani ukiwa na jazba? Kwani katiba ya CCM inasemaje linapokuja suala la wanachama wake kufanya vitendo vinavyoashiria kampeni za mapema? Umeona hapo kwenye RED? Unaweza ku-connect dots hapo? Manake hapo kwenye RED ni kama umetaja jina la mtu na kwamba hasira zako ndipo zilipojikita...ni hisia zangu tu!!
 
Last edited by a moderator:
Mleta maada hivi unajua sheria na katiba ya chama cha mapinduzi(CCM)? kwa sababu hujui ndo maana umeandika hayo unayowaza, unajua nn maana ya chama cha siasa? nadhani umesahau kuwa kila chama kna mwenendo wake na lengo kuu la kila chama ni kushika dola na si kila lengo la mwanachama ni kushika dola.... jiulize n kushka nini? lakn mwisho umesema we si mwanachama wa chama chochote, lakn inaonesha dhahili huipend ccm ila nadhan unawapenda baadhi ya wana ccm na kuna chama unakipenda zaid ya ccm, au wanachama wake. Hvyo we ni mwanasiasa.
CCM NI CHAMA MAKINI AMBACHO KIKO MAKINI NDO MAANA KILICHUKUA UAMUZI HUO.
 
Ccm haiwezi kuwavumilia wachuuzi wa madaraka.wanaonunua madaraka na uongozi kwa fedha zao

Bali itawasaidia kung'aa zaidi kwa kujifanya kuwatishia. Sasa tungojee kidogo, watakapo amka itakuwa tishio kuonesha ni nani bingwa wa kuzigawa.
Hata mtapetape vipi, EL atawatoa jasho mpaka mchanganyikiwe. 2015 hicho chama kitajimaliza chenyewe kwani kwenye nomination peke yake wajumbe watakuwa mamilionea kama sio matrilionea. Hawataangalia sura ya mtu bali uzito wa bahasha. Mliikata kuwa sio takrima, mkaleta harambee sasa mmeikataa sijui mtaiita "Miwani" au?
Nasema, bila rushwa ccm hakuna kura. Hawajui lugha nyingine yeyote, bali kununua kadi za wapiga kura tu. Ndio zenu hizo
 
Lowassa akiguswa lazima Pasco wa JF povu limtoke.. hahahaaaa mtajijua na LiCCM lenu kama ulivyosema CCM is not a determinant kwenye urais 2015, Daftari likiboreshwa CCM kwaheri...
 
Ccm haiwezi kuwavumilia wachuuzi wa madaraka.wanaonunua madaraka na uongozi kwa fedha zao

Hahahahahahaaa Eti eheeee, sasa Mbona mlisema mtawavua gamba mmeshindwa sasa mnatoa Maonyo makali na makaripio makali tu.. hahahaa CCM mmekwisha kabisa na Lowassa ndo anakwenda kuwamalizia.. CCM ndo imejenga utamaduni wa kuchuuza madaraka sasa kwanini wanachama wake wasifuate utamaduni huo wa uchuuzwaji wa madaraka ndani ya chama chenu.
 
Papa wanatishiwa kwa chelewa.

Ila Pasco haya mambo ya siasa inabidi ujiandae sana kifikra, kama dogo tu hivi umechafukwa namna hii, vipi vikianza vikao vya chama vya kukata jina la silver hair??
Hii ni zaidi ya bahasha ya kaki aisee.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu wangu Pasco, mbona kama umedondoka jukwaani ukiwa na jazba? Kwani katiba ya CCM inasemaje linapokuja suala la wanachama wake kufanya vitendo vinavyoashiria kampeni za mapema? Umeona hapo kwenye RED? Unaweza ku-connect dots hapo? Manake hapo kwenye RED ni kama umetaja jina la mtu na kwamba hasira zako ndipo zilipojikita...ni hisia zangu tu!!

Hahahaha Viongozi wa dini watatoa matamko, Maonyo na Makaripio makali kwa CCM, kwa kuwatakia njaa kuelekea uchaguzi mkuu..
 
Wanabodi,

Nimesoma maamuzi ya CC ya CCM kuhusu wanaotuhumiwa kuanza harakati za kuusaka urais wa 2015.

Uamuzi wenyewe ni huu

  1. Kwa maoni yangu, maamuzi haya ni ya kipuuzi kupita maeleza!. Uamuzi huu unakiiza Chama cha Mapinduzi, katika listi ya vyama vya hovyo kabisa kupata kutokea!.
  2. Kwa vile wahusika ni wanachama wa Chama cha Mapinduzi, na wamevurumishiwa tuhuma mbalimbali za harakati za kuusaka urais, kufikia kiwango cha chama kuitisha kamati ya maadili kuwahoji, kabla ya kufikia hizi stages, ilibidi chama kipate tuhuma specific, hivyo walipoitwa kila mmoja alipaswa kusomewa tuhuma zake specific zikionyesha amevunja kanuni ipi, au kipengele kipi!, ndipo ajieleze!.
  3. Baada ya kupokea tuhuma na maelezo ya majibu, ilipaswa chama kijiridhishe na ushahidi kuhusu kukiukwa kwa tuhuma hizo na ndipo watoe adhabu!.
  4. Tamko hili la CCM ni just a "blanket sweeping statement!", lisilo na any specific kosa, hakuna kanuni iliyofunjwa, na hukumu ni too general, as if its a bunch of thugs, wakati watuhumiwa ni individuals na kila mmoja ame play role yake on his own, kuwaweka wote kwenye tenga moja, na kuwahukumu adhabu moja bila mchanganuo wa makosa yao, hiyo inaitwa hukumu ya "pakacha la samaki", akioza mmoja, wote wameoza!, huku sio kutendea haki wale ambao hawako kwenye harakati, at the expenses za wenye harakati!.
  5. Hata kama ni kweli, kuna watu wameanza harakati za chini chini, jee kuna yoyote aliyetangaza rasmi, expressly kuwa anautaka urais?, iweje CCM i act kwenye maneno ya kutajwa tajwa tuu!. Huu ni uthibitisho CCM ni chama cha majungu, fitna na zengwe, ambapi inayafanyia kazi majungu, fitna na zengwe, na kutoa maamuzi ya kimajungu majungu, kuwafanyia fitna na kutaka kuwapiga zengwe tuu baadhi ya wanaotajwa!.
  6. Naomba kuuliza tena, hivi kuna kosa lolote, mwana CCM yoyote, kuutamani urais?!.
  7. Hivi kuna kosa lolote, mwana CCM yoyote, kutangaza nia ya kuwania urais, wakati utakapowadia ili kutoa fursa kwa wana CCM kumpima?!.
  8. Jee lengo la adhabu hii ni kuwazuia watu wenye uchungu na umasikini wa Tanzania, kuwazuia wasihamasishe maendeleo na moyo wa kujitolea ili wasije wakaonesha huko ni kuusaka urais!.
  9. Niliwahi kusema CCM imechokwa, CCM imeozwa kwa rushwa left, right, from top to down on its roots, yaani imeoza hadi kwenye shina!, inanuka uvundo wa rushwa na vitendo vya ufisadi vilivyokithiri mwanzo mwisho!. Leo inapata wapi, ujasiri wa kuupiga mkwala mbuzi kama huu?.
  10. Uamuzi huu, ni kiashiria cha CCM kuendelea kujiona ni chama dola, hivyo kinatishia nyau ili wale wenye malengo mazuri na taifa hili, wakate tamaa, wanywee na kuwa watumwa wa CCM!
Natoa wito kwa wale wote wenye nia njema na taifa hili, waliochoshwa na umasikini wa Watanzania, walipuuze kabisa tamko hili la CCM, na kuendelea na harakati zao za kuwaletea maendeleo Watanzania, kwa sababu kwa uchaguzi wa 2015, kama daftari la kudumu la kupiga kura litaboreshwa, CCM sio determinant ya rais wa Tanzania, 2015, hivyo nawashauri wandeleze juhudi zao kwa kasi zaidi, ili hata CCM ikiamua kuwatimua kwenye hilo lichama lao rushwa kunuka!, Watanzania wanajua 2015, wanataka nini, wanataka rais gani, mwenye uwezo gani, na kukubalika kwa kiasi gani, akifukuzwa CCM, hata akisimama kama mgombea wa kujitegemea!, tutamchagua tuu!.

CCM iache tisha toto, na kuwatishia nyau watu wakubwa wazima!, na kwa mwendo huu wa CCM, na Chadema ni dhoofu bin taaban!, kwa 2015 mbona itakuwa Majanga?!.

Wasalaam.

Pasco.
NB. Pasco wa jf, sio mwanachama wa chama chochote cha siasa, ila supporter mkubwa wa kupigania Tanzania kupata rais mwenye uwezo ile 2015 kuepuka majanga ambayo tumeishakumbana nayo!.

Mkuu Pasco hapo kwenye RED sijakuelewa ulitaka kusema nini? Maana umekitaja Chadema hapo na sioni kinahusikaje na hii habari ya wanaCCM.
 
Last edited by a moderator:
Ukisoma maelezo ya mleta mada utajua wazi kuwaamevurugwa na anamtumikia mtu,hayuko huru

Wewe unamtumikia Nani? Mbona unajificha huku ukitokwa mapovu?
Acheni unafki. Mliwaita mafisadi mkataka wajivue Hanna, Wakagoma!! Wapo walioitwa mizigo, Wanatanua kwa raha zao , Leo eti wanapewa karipio.. Mtu amevunja Kanuni why asivuliwe uwanachama na kutimuliwa? CC inogopa nini?
 
Back
Top Bottom