Kwa teuzi hizi zinazofanywa na Mhe.Rais, nani atabisha kwa hoja kuwa Upinzani umewapika viongozi wengi? CCM ilikwama wapi?

Petro E. Mselewa

Verified Member
Joined
Dec 27, 2012
Messages
9,158
Points
2,000

Petro E. Mselewa

Verified Member
Joined Dec 27, 2012
9,158 2,000
Natazama kwa hicho la tatu kitendo cha wanasiasa mbalimbali wa upinzani kuhamia CCM. Naona ni kama bahati iliyomfikia Mhe Rais na hata CCM anayoiongoza katika kuwapata wateule wake.

Tangu mwaka 2015, Mhe Rais na CCM kwa ujumla wake umepata wateule kwenye nafasi mbalimbali za kiuongozi na katika kutimiza matakwa na dhima ya kuunda Serikali. Hadi sasa waliokuwa Wapinzani wameteuliwa kwenye nafasi mbalimbali.

Kuna Manaibu Mawaziri (Waitara na Shonza); Katibu Mkuu wa Wizara (Profesa Mshiriki Kitila Mkumbo); Balozi(Dr. Slaa); Mkuu wa Mkoa(Mama Mghwira); Katibu Tawala wa Mkoa(Kafulila); Wakuu wa Wilaya(Katambi na Mtatiro); MaDAS (mfano Mtela Mwampamba) na kadhalika.

Kwangu mimi huo ni ushahidi kuwa Upinzani uliwaandaa, kuwalea na kuwapika wahusika hao na kuwapa sifa za kiuongozi. Ndiyo maana Mhe Rais na CCM kwa ujumla wameridhika nao na kuwakabidhi nafasi hizo za kiuongozi. Mimi siwaiti Wasaliti wa upinzani ni fursa iliyopatikana kwa CCM ambayo 'haikuwa na watu kama hao'.

CCM wamekwama wapi katika kupika vijana na kuwakomaza kuwa na sina za kiuongozi kama hao waliotoka Upinzani? CCM ilikwama wapi kuwa na watu wazima kwenye sifa na kaliba hizo ili kuonwa na kuaminiwa na Mhe Rais? Kimsingi, sifa ziende kwa Upinzani, jiko lenye kuivisha wengi!
 
VAPS

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2012
Messages
2,971
Points
2,000

VAPS

JF-Expert Member
Joined Jul 10, 2012
2,971 2,000
Tuna mfumo wa hovyo sana wa teuzi katika taifa letu.Miongoni mwa mapungufu ya katiba yetu ni maamlaka yaliyopitiliza ya Rais. Tuna mifano mingi ya mazingira ya teuzi na kutenguliwa ni ya uzalilishaji sana. Mfano DC mteule sidhani alipaswa kupitia njia ile haramu. Basi tu njaa na ufinyu wa kufikiri.
 
sheiza

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2010
Messages
4,364
Points
2,000

sheiza

JF-Expert Member
Joined Sep 29, 2010
4,364 2,000
Hao upinzani ni asilimia ngapi ya walioteuliwa na magufuli nje ya wana ccm?
We inawezekana ukawaona ni upinzani ila kwa Magufuli ni watanzania na wanaenda kufanya kazi ya watanzania. Unaonekana kama mtu mzima ila mihemko ya kisiasa inadumaza ubongo wako.
 
Petro E. Mselewa

Verified Member
Joined
Dec 27, 2012
Messages
9,158
Points
2,000

Petro E. Mselewa

Verified Member
Joined Dec 27, 2012
9,158 2,000
Hao upinzani ni asilimia ngapi ya walioteuliwa na magufuli nje ya wana ccm?
We inawezekana ukawaona ni upinzani ila kwa Magufuli ni watanzania na wanaenda kufanya kazi ya watanzania. Unaonekana kama mtu mzima ila mihemko ya kisiasa inadumaza ubongo wako.
Kwanini wote wasingetokana na CCM?
 
YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2015
Messages
19,320
Points
2,000

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined Aug 9, 2015
19,320 2,000
Lets wait and see 2020.
True Katika chama kisichosomeka duniani CCM Ni namba Moja.CCM hakuna political scientist hata mmoja awezaye kukijua vizur.CCM Ina Ina circle nyingi ndani ya inner Circle nyingi kuliko utando wa buibui.Upinzani walijua wamepata Lowasa na wazingu wakaimba Lowasa ,Lowasa kilichotokea hawaamini Hadi sasa.2020 haiko mbali it is just around the corner you will know who is who in CCM .CCM nyerere aliisuka ikasukika ni vyama vitatu tu duniani vilivyosukwa vikasukika Ni CCM ,chama Cha China na Cha Korea ya kaskazini.Hivi inner circles zake ziko nyingi mno na zinajua kutunza Siri.Dont worry 2020 is coming
 
KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2019
Messages
898
Points
1,000

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Joined Apr 10, 2019
898 1,000
kwa teuzi hizo bado ni chache sana kusema upinzani ulipika/ unapika viongozi bora kuliko CCM. wote waliopewa vyeo waliongoka na kutubu kuwa CCM ndio penyewe na kuacha njia zao mbaya ambayo ni upinzani kwa maana hiyo wakawa ni wanaCCM hivyo inatoa picha ni kwa namna gani CCM ya Magufuli inaaminika hadi kwa wapinzani.

wanarudi CCM baada ya kukimbia upinzani ambako wengine walikuwa hawana amani ya moyo( rejea mama Mngwira) na wengine baada ya kuona upinzani umekosa dira( rejea balozi dk.Slaa) na wengine wengi. huo ni ushahidi tosha kwamba CCM ina hazina kubwa ya viongozi ila uongozi ni kipawa ambacho Mungu anajalia watu wake hivyo ni suala la muda na wakati.
 
DiasporaUSA

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2016
Messages
18,555
Points
2,000

DiasporaUSA

JF-Expert Member
Joined Aug 27, 2016
18,555 2,000
Hao hawajapikwa na upinzani. Hao ni mamluki walioandaliwa na CCM kuwarubuni wananchi kwa kujifanya watetezi wa wananchi walipokuwa upinzani. Wanapewa nafasi za uteuzi kama zawadi ya kazi waliyoifanya.
 
Freddie Matuja

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2018
Messages
560
Points
1,000

Freddie Matuja

JF-Expert Member
Joined Jul 21, 2018
560 1,000
Natazama kwa hicho la tatu kitendo cha wanasiasa mbalimbali wa upinzani kuhamia CCM. Naona ni kama bahati iliyomfikia Mhe Rais na hata CCM anayoiongoza katika kuwapata wateule wake.

Tangu mwaka 2015, Mhe Rais na CCM kwa ujumla wake umepata wateule kwenye nafasi mbalimbali za kiuongozi na katika kutimiza matakwa na dhima ya kuunda Serikali. Hadi sasa waliokuwa Wapinzani wameteuliwa kwenye nafasi mbalimbali.

Kuna Manaibu Mawaziri (Waitara na Shonza); Katibu Mkuu wa Wizara (Profesa Mshiriki Kitila Mkumbo); Balozi(Dr. Slaa); Mkuu wa Mkoa(Mama Mghwira); Katibu Tawala wa Mkoa(Kafulila); Wakuu wa Wilaya(Katambi na Mtatiro); MaDAS (mfano Mtela Mwampamba) na kadhalika.

Kwangu mimi huo ni ushahidi kuwa Upinzani uliwaandaa, kuwalea na kuwapika wahusika hao na kuwapa sifa za kiuongozi. Ndiyo maana Mhe Rais na CCM kwa ujumla wameridhika nao na kuwakabidhi nafasi hizo za kiuongozi. Mimi siwaiti Wasaliti wa upinzani ni fursa iliyopatikana kwa CCM ambayo 'haikuwa na watu kama hao'.

CCM wamekwama wapi katika kupika vijana na kuwakomaza kuwa na sina za kiuongozi kama hao waliotoka Upinzani? CCM ilikwama wapi kuwa na watu wazima kwenye sifa na kaliba hizo ili kuonwa na kuaminiwa na Mhe Rais? Kimsingi, sifa ziende kwa Upinzani, jiko lenye kuivisha wengi!
Wateule toka upinzani ni Watanzania na wana equal chance kama Watanzania wengine kuteuliwa maadam wana sifa.

Watanzania wenzetu hao toka vyama pinzani ni wachache in number vs wateule waliotoka CCM.

Hata marais waliopita walifanya kazi na watu toka Upinzani, kama JK alimpa Wasira Uwaziri na alitokea NCCR. Dr. Shein nae anafanya kazi na Wapinzania. JK aliwahi kumpa Dan Makanga U-DC

CDM nao waliwahi kuwapa watu toka CCM kuingia kamati kuu moja kwa moja. Lowasa, Nyalandu, Mpendazoe, Sumaye, Waitara ailitoka Ukatibu UVCCM mkoa wa Tanga na kuingia kamati kuu moja kwa moja.
 
X-bar

Senior Member
Joined
Mar 20, 2019
Messages
190
Points
250

X-bar

Senior Member
Joined Mar 20, 2019
190 250
Hukupaswa kutumia jicho la tatu kutambua mtazamo wa Magufuli juu ya makada wa upinzani. Bali ilikupasa kutumia kumbukumbu ya kauli alizowahi kuzitoa kuhusu wapinzani. Labda nikusaidie kidogo.

Kwanza ikumbukwe kuwa aliwahi kumshangaa Shain kwa nini ameteua wapinzani kushika nafasi za uongozi katika serikali anayoiongoza. Lakini akahapa yeye katika serikali yake "nyoka hawezi kulamba unga" yaani hatateua wapinzani kuwa kuingia serikalini.

Pili, Magufuli amepiga marufuku harakati za siasa hadi wakati wa kampeni za chaguzi zinazofuata.

Tatu, kuzuia siasa peke yake Magufuli aliona haitoshi kwa vile kuna jukwaa mbadala ambalo wapinzani wangeweza kulitumia kufanya siasa ambalo ni Bunge. Alichofanya Maguguli ni kumuagiza Ndugai afukuze waropokaji (wapinzani) ili wakija kuropoka nje ya Bunge yeye mwenyewe a-deal nao. Lakini zaidi alichofanya ni kuzuia matangazo mubashara ya Mikutano ya Bunge.

Hapa ndugu yangu najaribu kukumbusha hulka na mtazamo wa Magufuli juu ya wapinzani ili ikusaidie kutambua endapo teuzi anazotoa kwa makada wa upinzani ni kutokana na "kuwakubali" kuwa ni watu mahili zaidi kuliko wenzie wa CCM au la. Ukweli ni kwamba, Magufuli hapendi wakosoaji (wapinzani).

Labda unaweza kuhoji kama hawapendi wapinzani kwanini anawaingiza serikalini? Jibu ni moja tu; ni UOGA. Kwavile hapendi upinzani, anatamani wanasiasa wote wawe upande wake na ili abaki na amani ya kisiasa. Hata hivyo hakuna mwanasiasa aliyetayari kwenda upande wake burebure. Namaanisha hakuna mpinzani anaweza kukubali kuitwa msaliti kwa kujitoa upinzani na kisha abaki mwanachama wa CCM wa kawaida. Kwa hiyo teuzi za Magufuli kwa makada wa upinzani ndo "Bei" pekee ya kuvutia wapinzani wawe upande wake. Na hii ni fursa kwa wanasiasa ambao wako kimaslahi binafsi.

Hata hivyo mbinu hii ni ya kuteua wapinzani dhidi ya wanna ccm asilia inaweza ku-backfire kwasababu wanaccm asilia inaonekana hawako tayari kuwa chini ya wateule ambao hapo awali "waliwapa taabu sana" kutetea serikali ya chama Chao. Matokeo yake wanaccm asilia wanaweza kugeuka.
 
Forum statistics

Threads 1,355,632
Members 518,708
Posts 33,114,450
Top