Kwa tamko hili la Uingereza Haya sasa ni Matusi...Hebu soma ilivyokuwa

Consigliere

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
12,037
24,595
Kwa kauli na msimamo uliotolewa na Uingereza kwa hakika wametuabisha au tumejiaibisha.
Wametupa misaada kutulemaza na sisi tukalemaa na kujikuta tumekuwa mateja wa misaada, tukaacha kufanya production nchini, tukaingia mikataba ya hovyo yenye kupoteza rasilimali zetu nk.

Baada ya kuona dozi imetukolea na kuacha ni vigumu kwasababu ya uteja wetu, Wamewaita Viongozi wetu huko Australia nao wakafunga safari kwa mbwembwe wengine wakiambatana na wake zao, wengine vimada (Si unajua tena Miafrika Ndivyo Tulivyo) na ujumbe mzito mzito wa kila aina.
Mkutano ulipoanza Jamaa wakainuka na kusema jamani tumewasaidieni sana na kuanzia sasa atakayetaka msaada wetu ni lazima tuhalalishe ushoga kwanza , lakini jamaa wameonyesha kumaanisha walichokiongea na wanataka taratibu za kuanza kuhalalisha hako kamchezo zianze mapema.
Haya ni matusi ya viwango vya uwenda wazimu japo tumejitakia, kwa hali hii na tulipofikia sijui muna maoni gani hebu tushauriane.

Je tuna maoni gani juu ya hii kampeni ya Kampeni hii ya waingereza.

NIMEAMUA KUPUNGUZA MAKALI YA LUGHA KAMA WENGI WALIVYOPENDEKEZA ILI TWENDE SAWA
.
 
Mtoa mada, naomba mjadala huu uutambulishe kwa kutumia lugha ya kawaida ili tuweze kuchangia. Mambo ya suruali sijui nini, wengine hatuelewi au tunaona jukwaa halitutoshi hivyo tupite twende kwingine.

Ahsante.
 
Mtoa mada, naomba mjadala huu uutambulishe kwa kutumia lugha ya kawaida ili tuweze kuchangia. Mambo ya suruali sijui nini, wengine hatuelewi au tunaona jukwaa halitutoshi hivyo tupite twende kwingine.

Ahsante.
Nimefungua maneno yaliyopo kwenye mabano, ndiyo yameleta maana yenye ukali huo.
Ni makali lakini tukiyajadili katika ukali wake itakuwa vizuri zaidi, kama tutayavalisha nguo kama walivyofanya waingereza huenda tusiyape uzito stahiki.
Naomba tu uvumilie mkubwa kwani hata lile tamko ni kali sana
 
Mmmm hili suala ni la kuamuliwa Bungeni kwa wawakilishi wetu!!
 
Nimefungua maneno yaliyopo kwenye mabano, ndiyo yameleta maana yenye ukali huo.
Ni makali lakini tukiyajadili katika ukali wake itakuwa vizuri zaidi, kama tutayavalisha nguo kama walivyofanya waingereza huenda tusiyape uzito stahiki.
Naomba tu uvumilie mkubwa kwani hata lile tamko ni kali sana

Ufahamu kwamba wewe hupaswi kuendeleza ukali wa maneno ya waingereza kwa kuwa wewe si mwakilishi wao hapa. Unatakiwa utumie lugha inayoelewka katika forum ili kuwapa watu habari na nafasi ya kuchangia hoja. Vinginevyo useme hii mada ni kwa watu wa aina fulani tu. La sivyo havyo mambo ya lugha za suruari na matuzi mengine hayafungui mjadala. Uelewe kwamba si watu wote wanajua undani wa yaliyoongelewa katika ule mkutano. Isitoshe unachokiona wewe ni suruari mwingine anaweza akawa na tafisir tofauti na yako, na tukapata mawazo muafaka yanayotoka kwa watu wa umri, fani, itikadi, uelewa na mitazamo mbali mbali. Lakini kama unaona hicho ndicho ulichokitaka, kwa heri.
 
Kwa nini msiseme 'hasa hao waingereza wamesema nini?
wekeni link basi tusome wenyewe
 
nilidhani ni mimi tu ambaye nipo njia panda kumbe wengi tu lugha hapa gongana!
 
Mmh ama kweli shetan hana muda wa kupoteza, anafanya kila mbinu, sijui ndo mpinga kristo anajongea eeh Mungu tusaidie.
 
Nimekubaliana na pendekezo la kuyaondoa maneno makli kama baadhi walivyopendekeza, lakini muundo wa uwasilishaji utabaki vile vile ili kuendana na maana ya ya Forum (Chit-Chat) na ndiyo maana sikuipeleka kwenye forum ya siasa
 
Kama Uingereza wametulazimisha tuanzishe taratibu za Ushoga basi, MPINGA KRISTO yupo karibu!
 
Mr.Gay Cameron keep your England and we will keep our respected country(God bless Tanzania) Nalog off
 
its time we stand for our dignity and our moral being. We can not bow to everything, let us die poor but not sell our soul and everything we believe in.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom