Ndugu Zangu,
MAGAZETI, Redio na Runinga zimeripoti, jana na leo; Freeman Mbowe amemtosa John Shibuda kwenye Baraza Kivuli la Mawaziri.
Tafsiri yangu, Mzee John Shibuda, Mbunge wa Maswa Magharibi kwa tiketi ya CHADEMA ( CCM?) hana wakati mzuri ndani ya CHADEMA. Kule kwao kwa asili CCM alifanyiwa fitna. Jina lake likaenguliwa kwenye kura za maoni.
Na Mzee wa watu alikuwa juu kwenye kura za maoni. Lakin,i CCM tunawajua, wakafanya Vitu vyao! Wakamnyima kivuli cha kisiasa. Shibuda, Msukuma anayewazidi Wasukuma wote kwa Kiswahili fasaha akaachwa na chama chake aungue juani!
Masikini Mzee Shibuda, kada mahiri asiyekana wala kuidharau asili yake kiitikadi, alichanganyikiwa. Akakata shauri kuvuka bahari. Akaenda Unguja kuomba ushauri kwa watani zake, Waswahili wa Unguja. Msukuma wa watu akarudi bara.
Breki ya kwanza ikawa Kinondoni, Makao Makuu ya CHADEMA- Chama Cha Demokrasia Na Maendeleo. Na jana akaambiwa laivu- Hata CHADEMA hakuna kivuli!
Mwenyekiti Mbowe amem-freeze Shibuda. Inasemwa magazetini, kuwa Shibuda ameonekana kuwa na mitazamo tofauti dhidi ya chama chake cha sasa. ( Mwananchi, Februari 15, 2011)
Na ugomvi si ulianzia tangu Bagamoyo, au? Iliandikwa wakati ule, kuwa kulikuwa na kushikana mashati kati ya Kijana Ezekiel Wenje na Mzee John Shibuda. Kijana Wenje alimshutumu Mzee wake kwa uroho wa minofu! Ndio maana, wakati wenzake wamesusa, yeye akavaa shati lake jeupe na kwenda Ikulu ya Chamwino; kula nyama, kunywa na kucheza mduara kwenye sherehe ya Jakaya, Rais wa nchi.
Waandishi wakamfuata Shibuda kumwuliza kulikoni kushikana mashati na Wenje. Tukamsikia Mzee Shibuda akitamka; Nitakwenda kumshtaki Wenje kwa Wazee wa Mwanza!
Hata pale kuna tulioingiwa mashaka; hivi CHADEMA hakuna Wazee?
Na leo imeripotiwa, kuwa vijana wa CHADEMA vyuo vikuu mkoani Dodoma wamepanga leo waende ofisi za Bunge kumzuia Mzee Shibuda asiingie Bungeni, kisa? Msaliti!
Si Shibuda alitamka juma la jana pale Bungeni, kuwa vijana wa sasa wanahitaji mwongozo mzuri zaidi wa malezi na kwamba yeye atabaki na maadili aliyojifunza ndani ya CCM. Na hakuwa mchoyo, Mzee Shibuda akasema atayapeleka CHADEMA!
Hapo ndipo alipokosea mtani wangu, Msukuma wa watu Shibuda, Ya CCM kuyapeleka CHADEMA! Vijana wa CHADEMA wamemjia juu kama moshi wa kifuu. Wanasema; Yeye anataka kuleta malezi aliyoyapata CCM alete CHADEMA, malezi ya CCM ayalete CHADEMA! Hapa hatutaki na sisi tutaandama Jumanne ( leo) kwenda kumzuia Shibuda asiingie Bungeni. Alitamka kijana Toju, Mwenyekiti wa tawi la Miyuji, Dodoma.
Wabunge Lema na Mdee walikuwapo . Lema akatamka, kuwa suala hilo liko ndani ya uwezo wa viongozi wa chama chao. Mdee akasema hakuna haja ya kumfutilia mbunge huyo ( Shibuda). Kama hukumu atahukumiwa na jamii husika. ( Mwananchi, Februari, 15, 2011).
Yote haya yanaacha maswali. Moja nalojiuliza, hivi kwanini vyama vyetu vya siasa vinapata tabu sana kumvumilia mwanachama mwenye fikra au mtazamo tofauti na wezake. Kwa nini muono tofauti uwe sawa na usaliti? Tumeyaona ndani ya CCM, na sasa CHADEMA.
Nini kifanyike kuimarisha Intra- Party Democracy ndani ya vyama vyetu hivi? Nimechokoza mjadala.
Maggid
Iringa,
Februari 15, 2011
mjengwa
.............Mzee John Shibuda, Mbunge wa Maswa Magharibi kwa tiketi ya CHADEMA ( CCM?) hana wakati mzuri ndani ya CHADEMA. Kule ' kwao' kwa asili CCM alifanyiwa fitna. Jina lake likaenguliwa kwenye kura za maoni.
Na Mzee wa watu alikuwa juu kwenye kura za maoni. Lakin,i CCM tunawajua, wakafanya ' Vitu vyao!' Wakamnyima kivuli cha kisiasa. Shibuda, Msukuma anayewazidi Wasukuma wote kwa Kiswahili fasaha akaachwa na chama chake aungue juani!............
Ndugu Zangu,
...Yote haya yanaacha maswali. Moja nalojiuliza, hivi kwanini vyama vyetu vya siasa vinapata tabu sana kumvumilia mwanachama mwenye fikra au mtazamo tofauti na wezake. Kwa nini muono tofauti uwe sawa na usaliti? Tumeyaona ndani ya CCM, na sasa CHADEMA.......
Maggid
Iringa,
Februari 15, 2011
mjengwa
Msukuma anayewazidi Wasukuma wote kwa Kiswahili fasaha
.............Mzee John Shibuda, Mbunge wa Maswa Magharibi kwa tiketi ya CHADEMA ( CCM?) hana wakati mzuri ndani ya CHADEMA. Kule ' kwao' kwa asili CCM alifanyiwa fitna. Jina lake likaenguliwa kwenye kura za maoni.
Na Mzee wa watu alikuwa juu kwenye kura za maoni. Lakini CCM tunawajua, wakafanya 'Vitu vyao!' Wakamnyima kivuli cha kisiasa. Shibuda, Msukuma anayewazidi Wasukuma wote kwa Kiswahili fasaha akaachwa na chama chake aungue juani!...........
Maggid,
Naomba kwa kuweka rekodi sawa: Shibuda alishindwa (hakuenguliwa) kwenye kura za maoni na Ndg Robert Kisena ingawa kuna madai kwamba rushwa ilitumika kwa kiwango cha juu sana hasa ukizingatia hakuwa chaguo la Chama Mkoa hata Taifa.
Tukirudi kwenye mjadala wa Intra-Party Democracy nadhani ni mjadala mpana kwa sababu bado hatujaelewa hata demokrasia yenyewe nini.
Wapo wanaosema sauti ya wengi ndio democrasia na sio kuwasilikiza wachache.
Wengine wanaamini democrasia ni uhuru wa kusema chochote tu bila kujali kina madhara gani kwa wengine. Mtu anayeadhibiwa au kukosa uongozi kwenye chama anakihama huku akisema hakuna demokrasia ndani ya chama ila akipandishwa cheo ndani ya chama ndo demokrasia (hapa namkumbuka M/kiti wa BAWACHA).
Kwa mtazamo wangu mfumo unaotawala siasa zetu ni kitu tofauti kabisa na kinachoitwa demokrasia kama ambavyo nyumbani kwako Majid au kwangu kusivyo na demokrasia - iite Intra-Family Democracy.
SHIBUDA CITATION
Kwa mtazamo wangu si sahihi waandishi kusema "Shibuda atoswa" au "Mbowe ammwaga Shibuda".
Kwa nini waandishi wanataka ionekane kwamba ilikuwa ni lazima Shibuda kuwa waziri kivuli?? Kabla hajahamia Chadema hakupata kuwa waziri hivyo nafasi yake ilikuwa sawa na wabunge wengine wa upinzani.
Uzoefu wa kuwa Bungeni haumaanishi anakuwa bora kuliko wageni kama Mnyika au Lisu.
Kwa silka Shibuda ni mwongeaji na ni vema watu wakamkubali kwa namna alivyo bila kuongeza tafsiri kwamba ni mamluki.
Inawezekana kweli kwamba Chadema wana namna yao ya kuendesha mambo lakini ukisilimu haimanishi kwamba tayari utaijua Quran yote. Kinachotakiwa ni kutambua haiba zetu ili itupe nafasi ya kufanya kazi pamoja au kurekebishana.
Mimi bado sioni kwa nini watu wadhani Shibuda hana kivuli Chadema kwa vile tu alipishana na Wenje au Toju (M/kiti wa Tawi Vs Mbunge??). Kwa upande mwingine sioni kama kuna tatizo kwenye majibu ya Lema au Mdee (kama hivyo ndivyo walisema).
Kwa msingi wa hoja hii,
Je tutumie mabishano ya Shibuda na Wenje kama kigezo cha lack of Intra-Party Democracy?
Kwa Shibuda kukosa uwaziri-kivuli ni dalili ya kukosekana kwa Intra-Party Democracy??
Lakini pia Demokrasia ni nini kabla hatujadadavua demokrasia ndani ya Vhama???
Yote haya yanaacha maswali. Moja nalojiuliza, hivi kwanini vyama vyetu vya siasa vinapata tabu sana kumvumilia mwanachama mwenye fikra au mtazamo tofauti na wezake. Kwa nini muono tofauti uwe sawa na usaliti?

Tafsiri yangu, Mzee John Shibuda, Mbunge wa Maswa Magharibi kwa tiketi ya CHADEMA ( CCM?) hana wakati mzuri ndani ya CHADEMA. Kule ' kwao' kwa asili CCM alifanyiwa fitna. Jina lake likaenguliwa kwenye kura za maoni.
Na Mzee wa watu alikuwa juu kwenye kura za maoni. Lakin,i CCM tunawajua, wakafanya ' Vitu vyao!' Wakamnyima kivuli cha kisiasa. Shibuda, Msukuma anayewazidi Wasukuma wote kwa Kiswahili fasaha akaachwa na chama chake aungue juani!
Masikini Mzee Shibuda, kada mahiri asiyekana wala kuidharau asili yake kiitikadi, alichanganyikiwa. Akakata shauri kuvuka bahari. Akaenda Unguja kuomba ushauri kwa watani zake, Waswahili wa Unguja. Msukuma wa watu akarudi bara.
Breki ya kwanza ikawa Kinondoni, Makao Makuu ya CHADEMA- Chama Cha Demokrasia Na Maendeleo. Na jana akaambiwa laivu- Hata CHADEMA hakuna kivuli!
Mwenyekiti Mbowe amem-freeze Shibuda. Inasemwa magazetini, kuwa Shibuda ameonekana kuwa na mitazamo tofauti dhidi ya chama chake cha sasa. ( Mwananchi, Februari 15, 2011)
Na ugomvi si ulianzia tangu Bagamoyo, au? Iliandikwa wakati ule, kuwa kulikuwa na kushikana mashati kati ya Kijana Ezekiel Wenje na Mzee John Shibuda. Kijana Wenje alimshutumu Mzee wake kwa uroho wa minofu! Ndio maana, wakati wenzake wamesusa, yeye akavaa shati lake jeupe na kwenda Ikulu ya Chamwino; kula nyama, kunywa na kucheza mduara kwenye sherehe ya Jakaya, Rais wa nchi.
Waandishi wakamfuata Shibuda kumwuliza kulikoni kushikana mashati na Wenje. Tukamsikia Mzee Shibuda akitamka; Nitakwenda kumshtaki Wenje kwa Wazee wa Mwanza!
Hata pale kuna tulioingiwa mashaka; hivi CHADEMA hakuna Wazee?
Na leo imeripotiwa, kuwa vijana wa CHADEMA vyuo vikuu mkoani Dodoma wamepanga leo waende ofisi za Bunge kumzuia Mzee Shibuda asiingie Bungeni, kisa? Msaliti!
Si Shibuda alitamka juma la jana pale Bungeni, kuwa vijana wa sasa wanahitaji mwongozo mzuri zaidi wa malezi na kwamba yeye atabaki na maadili aliyojifunza ndani ya CCM. Na hakuwa mchoyo, Mzee Shibuda akasema atayapeleka CHADEMA!
Hapo ndipo alipokosea mtani wangu, Msukuma wa watu Shibuda, Ya CCM kuyapeleka CHADEMA! Vijana wa CHADEMA wamemjia juu kama moshi wa kifuu. Wanasema; " Yeye anataka kuleta malezi aliyoyapata CCM alete CHADEMA, malezi ya CCM ayalete CHADEMA! Hapa hatutaki na sisi tutaandama Jumanne ( leo) kwenda kumzuia Shibuda asiingie Bungeni". Alitamka kijana Toju, Mwenyekiti wa tawi la Miyuji, Dodoma.
Wabunge Lema na Mdee walikuwapo . Lema akatamka, kuwa suala hilo liko ndani ya uwezo wa viongozi wa chama chao. Mdee akasema hakuna haja ya kumfutilia mbunge huyo ( Shibuda). Kama hukumu atahukumiwa na jamii husika. ( Mwananchi, Februari, 15, 2011).
Yote haya yanaacha maswali. Moja nalojiuliza, hivi kwanini vyama vyetu vya siasa vinapata tabu sana kumvumilia mwanachama mwenye fikra au mtazamo tofauti na wezake. Kwa nini muono tofauti uwe sawa na usaliti? Tumeyaona ndani ya CCM, na sasa CHADEMA.
Nini kifanyike kuimarisha Intra- Party Democracy ndani ya vyama vyetu hivi? Nimechokoza mjadala.
Maggid
Iringa,
Februari 15, 2011http://mjengwa.blogspot.com
CHADEMA washamshutikia Shibuda kuwa ni mercenary aka mamluki kama wewe unavyoji "shibudadua" kwenye masuala, au siyo?