DR HAYA LAND
JF-Expert Member
- Dec 26, 2017
- 31,636
- 81,533
Kwa Tanzania tuna misikiti Mingi na makanisa mengi Sana .
Na ukiangalia idadi ya watu wanaosali bado ni Chache Sana .
Ikiwa tutaangalia mahitaji hasa ya jamii tunaweza kubadilisha matumizi ya hizo pesa.
Mfano wafadhili ambao hujitolea kujenga misikiti na makanisa , jaribuni kufikiri hilo kuwa tunaweza kujenga Visima Vya maji , tunaweza kujenga maktaba , Shule na kusapoti huduma za Afya.
Unaweza kukuta eneo lina misikiti Kumi Ila eneo hilo hilo halina hata kisima kimoja cha Maji ambacho watu wanachota bure.
Au unasikia taasisi imejenga kanisa lenye thamani ya B-Kadhaa Ila eneo hilo hilo halina huduma za kijamii .
Kwa sasa tufanye mambo kwa kuangalia Vipaumbele.
Miaka ya nyuma nilikuwa nikienda msikitini wanaosali hawafiki 05 Ahsubui .
Ila utaona watu wanachangisha kujenga msikiti Mwingine.
Je kwanini wasichangishe kujenga kisima cha Maji , kumbuka kuna familia masikini na duni ambazo haziwezi hata kuoga kwa kukosa maji hapa nazungumzia maeneo ambayo maji yanauzwa.