Kwa sasa channel zote za taarifa ya habari nchini hazina mvuto kama habari za mitandaoni

toroka uje mjini

JF-Expert Member
Mar 29, 2017
1,584
2,111
Hivi inakuwaje lakini nikiangalia taarifa za habari kuanzia channel10, Star TV, ITV, Azam TV na TBC zinakua hazina mvuto kama taarifa au matukio, au habari kama za mitandaoni? Hususani MITANDAO ya SIMU kupitia JF, FB, Twiiter, Insta na mengineyo.
 
Mimi siku hizi naangalia aljazera,cnn fox news na zinginezo.taarifa za habari za hapa bongo hazina mpya.unasikia sijui ziara ya kushtukiza ya waziri,mara sijui bunge yaan No mvuto at all so tunaweka bando ili kuangalia page ya mange kafichua nini
 
Kwenye tv unapata habari za masaa mengi yaliyopita wakati kwenye mitandao unapata taarifa dakika chache baada ya tukio.
 
Home hata cable niliitoa kabxaa mambo yote medias za mitandaoni kupitia sim tu..
Ndo maana hata ITV walishajishtukia Kua hawana tena bao ktk TV wakaamua kutangaza Kua kama una smatfon ingia play store utakuta ITV na utaona kila.kitu MUBASHARA
 
Kwenye tv habari nyingi wanahariri ili kuendana na maadili ya uandishi wa habari kitu ambacho hupunguza radha ya habari
 
Hivi inakuaje lkn nkiangalia taarifa za habari kuanzia.channel10 ,Star TV,ITV,Azam TV,na TBC.
Zinakua Hazina mvuto kama taarifa au matukio,au habari kama za mitandaoni?
Hususan MITANDAO ya SIMU kupitia JF,FB,Twiiter,Insta na mengineyo
Ni kwa vile habari itakayosomwa usiku wewe unakuwa umeshaipata na pengine hata kushiriki mjadala wake
 
Hivi inakuaje lkn nkiangalia taarifa za habari kuanzia.channel10 ,Star TV,ITV,Azam TV,na TBC.
Zinakua Hazina mvuto kama taarifa au matukio,au habari kama za mitandaoni?
Hususan MITANDAO ya SIMU kupitia JF,FB,Twiiter,Insta na mengineyo
Kwasababu habari zinazotangazwa huko ni za mitandaoni, mitandao siku hizi ndio inayoendesha TV na Magazeti
 
vitalis msungost: 20556535 said:
Habari za mjini zinamhusu makonda,sasa waliapa kuto kuandika habari zake. So bora huku tunazipata mubashara tena mpaka video
Huyu mwizi wa vyeti?.Bashite ni aibu kubwa Dar kuongozwa na Kilaza
 
kuangalia habari za kitaifa siku hizi naona kama kupoteza muda, habari nyepesi nyepesi.
 
Kwa sababu umenunua simu hivi karibuni. Habari za kwenye tv zina mvuto wake mitandao isikudanganye
 
Ni kweli muda mrefu uko cm TV ni summary ya habari ambazo zote unazijua
 
Back
Top Bottom