christopher mlewa
Member
- Oct 22, 2018
- 15
- 39
Poleni kwa majukumu.
Ndugu zangu hapa katikati kuanzia miaka ya 2010 limeibuka wimbi la waandishi wa habari pamoja na vyombo vyao vya habari ambavyo vimekua ni zaidi ya janga kabisa.
Kwanza kabisa waandishi hawa ni weupe kichwani kiasi kwamba hadi wanatia aibu, mfano kuna radio na waandishi wake niliskia wanachambua migogoro ya mashariki ya kati daaaah aise nilijiskia aibu mimi, hakuna wanachojua hadi unashangaa wamefikaje hapo?
Sawa wanafika hapo si kwa sababu ya uwezo ila vyeti vya kuhonga vyuoni kwao na "connection" za hapa na pale sasa mbona hata maadili tu ya utangazaji hawa watu hawana?
Oooh ebu ona kuna siku namsikia "Babalevo" pale Wasafi Fm anasema "siku hizi Diamond hamzagamui zuchu vizuri, duuh on mic kabisa.
Halafu wamekua wakiuliza wananchi watoe majawabu badala ya wao wawatafutie majawabu, kwenye "MediaPlatforms" zao wanajaza maswali kwa wasomaji badala ya kuwapa majibu ya kipi ni kipi, kwa mfano mwandishi wa habari anauliza wasomaji wake ni sifa zipi mwenyekiti wa mtaa anatakiwa kuwa nazo? haaaa hapa mwandishi angekuja na jawabu lake tu ili asaidie umma.
Kiukweli ukitoka kutazama Al jazeera, BBC, CNN au CGTN halafu ukaminya rimoti bahati mbaya basi jiandae kwenda kushuhudia vituko vya akina Mwijaku na Zembwela huko TBC, CHANNEL 10, STAR TV, WASAFI TV AU CROWN, kama jana pale Crown Tv karibia masaa mawili walikua live kutuonesha birthday ya mwenzao (AIBU).
Siku hizi hadi Salim Kikeke ambaye alikua ndo hazina pekee iliyobaki nae anaanza kuiga hawa walio weupe kichwani, TUFANYAJE KUIOKOA HII TASNIA YA HABARI?
ASANTENI