Kwa sababu hatutaki kujifunza... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa sababu hatutaki kujifunza...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwanamageuko, Jan 5, 2011.

 1. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #1
  Jan 5, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,294
  Trophy Points: 280
  Wanasiasa wachache wenye maslahi yao wataendelea kuwatumia wapumbavu wachache ili kutimiza malengo yao ya kijinga, ninawaambia pamoja na kujiambia mwenyewe hapa ndugu zangu:

  TUSIMWAMINI MWANASIASA YEYOTE AWAE HATA KAMA NI NDUGU AMA MZAZI WETU.

  Kila mmoja anapigania ama kulinda maslahi yake, uchafu mtupu. (leo watu wanashawishiwa kuandamana huku na kule bila kuwapo malengo maalum)

  Wenzenu huko duniani wanajua wakiandamana matokeo yakiwa tofauti watafanya nini? Leo Mtanzania anaandamana achilia mbali pasi ya kusafiria NAULI yenyewe hana, Akiumia hana bima itakayomlipa wala hana hata shekeli ya kununulia dawa, na mwisho wa yote atakwenda kutibiwa kwenye hospitali ya serikali anayoipinga! Akifika kule ataulizwa hati ya polisi namba tatu (PF.3) hapo ndio atasindikizwa na pingu kurudi hospitali kama majibu yake hayakujitosheleza. (mhanga wa maandamano - tungelimuita mhanga wa demokrasia) Na pia tujiulize tena "Je katika kuandamana kwetu magari na nyumba zinazopigwa mawe huwa zimefanya makosa gani?"

  Gari la bwana Materu ambae si shabiki wa siasa na haki tunayoidai vinahusiana nini hata aadhibiwe?
  Je ni kwanini Mpitanjia ambaye hayuko katika maandamano apigwe na polisi kwa kuhusishwa ya yasiomhusu?

  Tunahitaji mabadiliko makubwa ya kifikra na pia tunahitaji tujiongezee busara katika maamuzi yetu, je Tanzania tuitakayo ama ijayo itakuwa ya kutotii mamlaka na utawala wa kisheria? (tuwe wakweli na tusimamie ukweli huo) Kama ni kuutafuta madaraka, umaarufu juu ya vilema na maiti za Watanzania wenzetu haya na iwe...

  Yawezekana kabisa ikawa kweli tunayoyataka hatuwezi kuyapata bila shinikizo, lakini pia tuangalie sarafu yetu upande wa pili nani ataathirika zaidi na shinikizo hilo WAO au SISI?

  Siioni picha njema hata kidogo. Wapo wanaodhani kwamba yanayofanyika ni sahihi (narudia tena - Wahanga wa matokeo ya upinzani wa serikali si wahusika pekee bali wengi wao ni walio nje ya wakusudiwa)

  Hivyo basi kabla hatujafanya tunayotaka kufanya; Tuwafikirie watoto wetu na wazee wetu kwanza waliomo majumbani.

  Tufikirie mbali zaidi ya hapo ndugu zanguni, ili tuijenge Tanzania tuitakayo. Tanzania yenye neema, demokrasia ya kweli na amani. Na hayo yote hayawezi kupatikana bila kuwa na KATIBA inayoruhusu. Lakini kabla ya katiba kupatikana tungelipaswa kuwa wapole vinginevyo tutakula virungu vya kutosha na wapo watakaokufa pia bila kujulikana.

  Narudia tena ndugu zangu watanzania...

  TUTAHITAJI MAPINDUZI YA KIFIKRA KWANZA, NA TUNAPASWA KUJUA TUNATAKA NINI KWA TANZANIA IJAYO.

  :angry:
   
 2. e

  emma 26 Senior Member

  #2
  Jan 5, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 108
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kweli
   
Loading...