Kwa ranks za Polisi, ni kazi gani kubwa zaidi ya u-IGP?

ubuntuX

JF-Expert Member
Aug 18, 2014
1,762
2,000
Jana ilitangazwa kutenguliwa kwa uteuzi wa mkuu wa polisi Tanzania, Ernest Mangu na ikaelezwa kuwa atapangiwa kazi na majukumu mengine.

Kwa mtu aliyeshika nafasi ya IGP hii ndio nafasi ya juu kabisa ndani ya jeshi la polisi, hivyo Kumtoa Mangu hapo inategemewa apangiwe majukumu mapya na ya juu zaidi ya IGP.

Je, ni kazi gani ndani na nje ya jeshi la polisi inaendana na mkulu huyu aliyepumzishwa huku akiwa bado ana nguvu na hali ya kuitumikia taifa?
 
tamuuuuu

JF-Expert Member
Mar 10, 2014
13,940
2,000
Labda ukurugenzi wa mashtaka but hajasoma sheria,ss akipewa ukuu wa mkoa si ameshuka!labda ubalozi.

Tume huru idaiwe mapema ccm itoke vinginevyo watanzania mtapata tabu sana
 
MTOCHORO

JF-Expert Member
Dec 18, 2016
3,265
2,000
Sarakikiya alitolewa kwenye CDF akiwa kijana na akapangiwa majukumu mengine sasa IGP ishindikane nini
 
ng'adi lawi

JF-Expert Member
Sep 27, 2014
2,955
2,000
Hak
Jana ilitangazwa kutenguliwa kwa uteuzi wa mkuu wa polisi Tanzania, Ernest Mangu na ikaelezwa kuwa atapangiwa kazi na majukumu mengine.

Kwa mtu aliyeshika nafasi ya IGP hii ndio nafasi ya juu kabisa ndani ya jeshi la polisi, hivyo Kumtoa Mangu hapo inategemewa apangiwe majukumu mapya na ya juu zaidi ya IGP.

Je, ni kazi gani ndani na nje ya jeshi la polisi inaendana na mkulu huyu aliyepumzishwa huku akiwa bado ana nguvu na hali ya kuitumikia taifa?
Hakuna na kamanda Mangu sasa itabidi astaafu jeshi na rais anaweza kumpa kazi ya kisiasa.
 
Kikarara78

JF-Expert Member
Nov 18, 2010
1,493
2,000
Boss Mr swax Swali zuri sana, kumbuka Jeshi la Polisi lipo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani. Pia kuna Wizara ya Ulinzi. Nje ya hapo kuna Ubalozi au Teuzi za Rais.

Jana ilitangazwa kutenguliwa kwa uteuzi wa mkuu wa polisi Tanzania, Ernest Mangu na ikaelezwa kuwa atapangiwa kazi na majukumu mengine.

Kwa mtu aliyeshika nafasi ya IGP hii ndio nafasi ya juu kabisa ndani ya jeshi la polisi, hivyo Kumtoa Mangu hapo inategemewa apangiwe majukumu mapya na ya juu zaidi ya IGP.

Je, ni kazi gani ndani na nje ya jeshi la polisi inaendana na mkulu huyu aliyepumzishwa huku akiwa bado ana nguvu na hali ya kuitumikia taifa?
 
mkorinto

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
16,299
2,000
Kwa mfumo wa polisi ulivyo,huyo ni mkubwa kuliko IGP wa sasa,hawezi akaendelea kuvaa uniform na kuripoti kazini.atasubiri kazi nyingine nyumbani kwake mpaka itakapokuja.

Na haitakuwa ndani ya polisi,huko taasisi zingine za serikali.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom