Kwa pamoja tusiache kuliombea Taifa letu

mchungaji7

Senior Member
Feb 2, 2017
187
396
Taifa letu linapita kwenye nyakati ngumu za changamoto mbali mbali, kama wananchi wenye uzalendo tusichoke kuliombea ili Mungu atuepushe na mabalaa.

Tumuombee Rais apewe hekima ili aongoze kwa haki bila kubagua.

Tuliombee Bunge liache kuburuzwa na serikali.

Tuiombee mahakama iamue mambo yote kwa haki.

Amani ya nchi yetu ndiyo amani ya familia..usipuuze omba.
 
Vitu vingine Mungu anaviacha kwa makusudi yake, hatuwezi tukasema Watanzania sio wendawazimu.

Angalia awamu ya mkapa mpaka ya kikwete jinsi pesa za serikaki zilivyokuwa zinaibiwa, angalia maliasili zilivyokuwa zinachezewa.

Kwa utahira wetu bado 2015 tukaiweka ccm hiyo hiyo madarakani. Ona leo hii kiongozi wa nchi anavyotoa kauli za ajabu, vyombo vya habari vinaminywa, serikali haitoi ajira, pesa za wahanga zinaliwa, yaani nchi haijulikani ni wapi inaenda.

Kwa uzezeta wetu 2020 tutaiweka tena madarakani.

Tusimhusishe Mungu na mambo ya kijinga.
 
Kama tusipo muhusisha Mungu tutatendewa mabaya zaidi ya haya, kama Rais katiba imempa madara ya kulevya unadhani kimbilio letu litakuwa wapi kama si kwa Mungu pekee? Tusichoke kuomba
 
Taifa letu linapita kwenye nyakati ngumu za changamoto mbali mbali, kama wananchi wenye uzalendo tusichoke kuliombea ili Mungu atuepushe na mabalaa.

Tumuombee Rais apewe hekima ili aongoze kwa haki bila kubagua.

Tuliombee Bunge liache kuburuzwa na serikali.

Tuiombee mahakama iamue mambo yote kwa haki.

Amani ya nchi yetu ndiyo amani ya familia..usipuuze omba.
Asante kwakutukumbusha mtumishi
 
Vyovyote vile tusiache kumuombea maana maamuzi yake yanaweza liweka taifa pabaya au pazuri
Mchungaji umekosa kazi ya kufanya? shida za kuombea zimekwisha kwenye diary yako? KWani huyu si ndo chaguo la mungu? sasa tunamuomba huyo mungu amfanyie nini chaguo lake?
 
Kama tusipo muhusisha Mungu tutatendewa mabaya zaidi ya haya, kama Rais katiba imempa madara ya kulevya unadhani kimbilio letu litakuwa wapi kama si kwa Mungu pekee? Tusichoke kuomba
Mkishachemsha katika mambo yenu ndo mnamkumbuka mungu wenu, mbona kabla ya yote hamjamuuliza huyo mungu kuwa jamaa anafaa au la?
 
Mchungaji umekosa kazi ya kufanya? shida za kuombea zimekwisha kwenye diary yako? KWani huyu si ndo chaguo la mungu? sasa tunamuomba huyo mungu amfanyie nini chaguo lake?
Mpendwa sijakosa cha kufanya ila hili nalo ni moja ya majukumu yangu tena ni la muhimu kuliko ujuavyo
 
Mkishachemsha katika mambo yenu ndo mnamkumbuka mungu wenu, mbona kabla ya yote hamjamuuliza huyo mungu kuwa jamaa anafaa au la?
Ndugu punguza hasira kisha tafakari Leo hii nchi ikipotea utakuwa wapi? Mungu anahimiza watu wake wasiache kuomba kila Leo, nini mbaya nikumuombea mtu ambaye amepewa dhamana kubwa yenye mustakabari wa maisha yetu?

Maombi ni muhimu nasisitiza tusiache kumuombea Rais wetu Mungu ampe hekima ya kuongoza
 
Ikipotea ni makosa ya dereva wa lori asiye taka kuelekezwa, watapotea walio ndani ya lori tu.
 
Mpendwa sijakosa cha kufanya ila hili nalo ni moja ya majukumu yangu tena ni la muhimu kuliko ujuavyo
Sasa kama ni jukumu lako unatusumbulia nini sisi? kwani nani kwakwambia kuwa na sisi hatuna majukumu yetu mpaka utupe yako? wewe fanya yako utuache na sisi tufanye yetu.
 
Kuna kipindi Wachungaji mlikuwa mnachukua picha zake na kuzimiminia mafuta ya upako, kisha mnabandika mikono juu ya picha na kushusha maombi ya nguvu. Imekuwaje tena???
 
Kuna kipindi Wachungaji mlikuwa mnachukua picha zake na kuzimiminia mafuta ya upako, kisha mnabandika mikono juu ya picha na kushusha maombi ya nguvu. Imekuwaje
 
Back
Top Bottom