Kwa nini watu wanalia?

Naskia machozi ni expression ya feelings kwa asilimia 99 na asilimia 1 inayobaki ni maji..
 
haka nako ni kashule, unaweza kudadavua?
Mkuu kuna siku nilikuwa nalia asa rafki yangu niliyekuwa naye akaenda dukani kuninunulia kitambaa akanipa af hakuniambia chochote akaniacha had nikanyamwaza mwnyw ndo akanipa hako kamsemo. Hata hivyo alisema mtu akilia unamwacha coz 99% ni hisia hivyo akinyamaza anajiskia nafuu (Anakuwa ameushusha mzigo) Baada ya hapo unaweza kuongea naye kwa kumpa moyo na vitu kama hivyo.
 
Nasikia kulia ni njia mojawapo ya kutoa sumu mwilini!! Niacheni nilie kwa raha zangu!
 
Inategemea unalia katika mazingira gani,tushashuhudia watu wakifurahi kupitiliza wanalia,nakubaliana na wadau tu kwamba ni kweli machozi huja baada ya hisia!
 
Jamani mimi the more I become strong the lesser I cry
 
na kucheka pia unaongeza dakika za kuishi, watu wengi wenye vidonda vya tumbo inasemekana mingoni mwa sababu ni hasira hovyo kusababisha nyongo kuunguza kongosho
Nasikia kulia ni njia mojawapo ya kutoa sumu mwilini!! Niacheni nilie kwa raha zangu!
 

MadameX,

Getting strong physically or emotionally?
najumuisha strong physically na kulia ni emotionally ..............nahisi hiki ni aina ya kilio cha furaha........wengine wakitaka kupigana hasira zinapanda sana na anahisi kupaa wengi wa hawa huishia kulia........huyu huenda analia hata kwenye box
 
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda ameangua kilio bungeni kuonyesha uchungu alio nao
dhidi ya vitendo vya mauaji ya kikatili ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino),
hivyo kuyeyusha hoja ya wabunge wa upinzani waliokuwa wamepania kumbana, ili
ajiuzulu kwa madai kwamba, alitoa amri ya kuua wauaji ambayo ni kinyume na
katiba ya nchi.
Hali hiyo ilitokea jana bungeni, wakati Pinda akielezea
yaliyomfanya atoe kauli hiyo tata kikatiba na misingi ya haki za
binadamu.
Pinda alisema alipokuwa katika ziara katika mikoa ya Kanda ya Ziwa,
alipata taarifa za kusikitisha kuhusu mauji ya albino na mara kesho yake habari
zikatoka kwenye vyombo vya habari kwamba, albino mwinge kauawa.
"Jamani
jamani taarifa za matukio hayo kibinadamu zinatia uchungu sana na kumfanya mtu
ashindwe kujizuia….," mara akaanza kutokwa machozi na kukatisha maelezo yake
akatoa miwani na kujifuta huku wabunge wakiwa kimya.
Waziri Mkuu alisema hayo
baada ya Kiongozi wa Kambi ya Upinzani bungeni, Hamad Rashid Mohamed, kumtaka
atoe ufafanuzi kuhusu kauli aliyoitoa hivi karibuni akiwa katika ziara Kanda ya
Ziwa, kuwaruhusu wananchi kuwaua watu watakaokutwa wakimchinja albino.
Hamadi
alisema katiba ya nchi inamlinda mtu kupewa nafasi ya kujitetea, hivyo akamtaka
waziri afafanue maana ya kauli yake, kwa kuwa ni kinyume na taratibu ambazo nchi
imejiwekea katika kuhakikisha haki inapatikana.
Pinda alisema mtu anaposikia
au kusoma taarifa za mauaji ya albino, hawezi kupata hisia juu ya mateso
wanayoyapata, sawa na anayewasikiliza watu walionusurika kufa au walioshuhudia
vitendo hivyo vikitendeka.
"Mimi walinihadithia, aah! Samahani," alisema kwa
masikitiko Pinda huku akiwataka radhi wabunge kwa kushindwa kuendelea kueleza
kwa jinsi alivyoguswa na matukio hayo. Mara akaanza kububujikwa na machozi na
baada ya sekunde kama 15, alichukua kitambaa chake akajifuta.
Aliendelea
kuelezea jinsi maalbino wanavyouawa kikatili, akisema wengi walikufa kwa
kushindwa kupata huduma mapema ya kuzuia damu baada ya ama kukatwa mikono ama
miguu na majitu hayo katili yenye imani potofu kwamba, viungo hivyo vinaweza
kumpatia mtu utajiri.
Alisema alielezwa kuwa, wauaji wanachokifanya ni
kumshambulia albino na kumkata kiungo wanachokitaka kwa kutojali hali
wanayomuacha nayo kama ni mateso, kufa au kupona hivyo alipatwa na uchungu kiasi
cha kujikuta anatamka kuwa, watu wanaokutwa wakitenda hayo nao wanapaswa
kuadhibiwa papo hapo.
Alifafanua kuwa wakati akiwa kwenye ziara hiyo
iliyokuwa maalumu kwa ajili ya kukemea na kupanga mikakati ya kukabaliana na
vitendo hivyo, idadi ya maalbino waliouawa walikuwa 30 na baada ya kukemea
vitendo hivyo, ghafla akapewa ripoti ya kuuawa wengine wawili, jambo ambalo
lilizidi kumuudhi na kumchanganya.
Waziri Pinda aliwaomba radhi watu
walioudhika kutokana na matamshi na pia akimuomba Mungu amsamehe iwapo
amewakosea.
"Kama mnaona kile nilichofanya ni makosa naomba mnivumilie.
Naomba Mungu anisamehe kama nimewakosea," aliomba Waziri Mkuu na kuongeza kuwa
serikali imechukizwa sana na mauaji hayo ya kikatili.
Alisema Tanzania
imekuwa ikiheshimika sana katika jumuiya ya kimataifa, lakini mauaji ya albino
na ya vikongwe katika eneo hilo yameitia doa.
Alielezea pia kuhuzunishwa
zaidi na tamko la Bunge la Jumuiya ya Ulaya (EU) la kulaani mauaji hayo, kana
kwamba wao wanaguswa sana na suala hilo kuliko Serikali ya Tanzania.
Hata
hivyo, alisema kuwa katika ziara hiyo, ambayo iliwahusisha pia baadhi ya
mawaziri, wabunge, viongozi wa polisi, viongozi wa dini na kisiasa, waliahidi
kushirikiana kuhakikisha kuwa wanakabiliana na kulimaliza tatizo.
Isitoshe
alisema aliwataka viongozi wa vijiji kurejesha ulinzi wa jadi, maarufu kama
sungusungu ili kukabiliana na wauaji.
Pinda alisema kuwa serikali ipo tayari
kupokea maoni kutoka kwa watu mbalimbali, yanayoweza kusaidia kupata mbinu ya
kukomesha kabisa mauaji hayo, ili kuiokoa jamii hiyo ya albino.
Alisema
katika kumbukumbu za serikali, hadi mwishoni mwa mwaka jana vikongwe 2,866
walikuwa wameuawa kwa imani potofu kuwa ni wachawi.
Alisema serikali
imeliagiza jeshi la polisi kutumia maarifa yake, hata kama itabidi kutumia
gharama kubwa, ili kuwatia mbaroni watu wote wanaojihusisha na mauaji
hayo.
Wapinzani pia walimtaka Pinda atoe maelezo yanayodaiwa kuwa yalitolewa
na Rais Jakaya Kikwete kisiwani Pemba kwamba, aliwashangaa wakazi wa eneo hilo
kuwachagua watu ambao hawawezi kuunda serikali na ambao watachukua muda mrefu
kupata nafasi hiyo.
Pinda alisema anapata taabu kujibu swali hilo, kwa sababu
hawezi kuyatolea maelezo mambo yaliyozungumzwa na bosi wake na wala hajui kama
ni kweli rais alisema kama vyombo vya habari vilivyoripoti.
Mbunge wa Konde,
Dk Ali Tarab Ali (CUF) alimtaka Pinda aeleze kama kitendo cha Rais Kikwete
kutumia magari ya serikali kisiwani Pemba na kuonekana akifanya shughuli za
chama ni matumizi mabaya ya fedha za serikali.
Pinda alimjibu akisema kuwa,
ni vigumu rais kutofautisha vyombo vya usafiri anavyovitumia wakati akifanya
ziara za kisiasa ama za kiserikali na kutoa mfano kwamba, hata rais wa Marekani
hutumia ndege aina ya Air Force one bila kuchagua kuwa ni shughuli ya kisiasa au
kiserikali.
Wakati hayo yakitokea bungeni, baadhi ya viongozi wa dini nchini,
wamemtaka Waziri Pinda kukiri kosa, kufuta kauli yake na kuomba radhi kwa
mamlaka za kisheria, Bunge na Wananchi.
Akizungumza na Mwananchi jijini Dar
es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislaam,
Sheikh Ramadhan Sanze alisema Pinda alifanya kosa la kiufundi kwa kuwa yeye ni
mtendaji mkuu wa serikali, hivyo hakupaswa kusema jambo linalopingana na msimamo
wa serikali, sheria na katiba ya nchi.
"Kwa vile kauli hiyo haijaleta madhara
mpaka sasa Waziri Mkuu ana uchochoro wa kupita ili kujisafisha. Cha msingi ni
kukiri kosa, kufuta kauli yake na kuomba radhi kwa mamlaka za kisheria, Bunge na
Wananchi" alishauri Sheikh Sanze.
Alisema, hajafuatilia vizuri kuhusu hoja za
kambi ya upinzani bungeni na kwamba, kujiuzulu inaweza isiwe suluhisho la tatizo
hilo kwa kuwa, hata kama atajiuzulu kauli haitafutika na tatizo litabaki
palepale.
"Nchi hii haina dini na kwa hiyo haingozwi na sheria za dini bali
inaongozwa na sheria za nchi, kwa hiyo Pinda alipaswa kuangalia sheria ya nchi
kwanza kabla ya kutoa agizo lake," alisema Sheikh Sanze.
Alifafanua kuwa,
Waziri Pinda ametengeneza mazingira ya uchafuzi na uchochezi, kutokana na kauli
yake hiyo kwani baadhi ya watu wanaweza kuitumia vibaya kwa kumuua mtu kwa
sababu ya chuki tu baina yao.
Alisema, athari ya kauli kama hizo zinaweza
kusababisha migogoro kati ya dini na dini nyingine, kabila moja na jingine au
dhehebu moja na jingine kama wananchi watautumia wito huo.
Alisema vita dhidi
ya mauaji ya albino imekuwa ikitumika kisiasa zaidi kuliko kitaalamu na kuongeza
kuwa, mamlaka husika ziliangalie tatizo hilo kitaalamu badala ya kuliacha
likitumika kisiasa.
Naye Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania,
Valentino Mokiwa alisema kauli ya Pinda ya kutaka aliyeua albino auawe si sahihi
kwa sababu mtu akimuua aliyeua ni muuaji na ana kosa kisheria.
Mauaji ya
albino yamekuwa yakitikisa nchi na hasa katika eneo la Kanda ya Ziwa, licha ya
juhudi mbalimbali zilizofanywa na serikali kupitia jeshi la polisi, mashirika ya
kutetea haki za binadamu, vyama vya walemavu na watu
binafsi.
Source:Mwananchi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…