Kwa Nini Watoto Wamebaguliwa Vitambulisho Vya Taifa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa Nini Watoto Wamebaguliwa Vitambulisho Vya Taifa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Plato, Aug 22, 2012.

 1. Plato

  Plato JF-Expert Member

  #1
  Aug 22, 2012
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 421
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 33
  Mwenyekiti naomba ufafanuzi,katika kuandikisha watu watakaopoata vitambulisho vya taifa Dar na nchini kote,tumeambiwa ni wenye miaka 18 na zaidi.sasa najiuliza kuwa wenye miaka 17 kuteremka siyo raia,na au hili zoezi ni kwa ajili ya uchaguzi? maana hilo ndo hutaka miaka 18.je mtu mwenye miaka 17 si mwaka kesho tu atakuwa na miaka 18? so zoezi hili nalo litakuwa mradi wa kudumu?
  Mimi nina wasiwasi kuwa zoezi hili litatumika kisiasa kwa maana ya kuja kusema asiye na kitambulisha cha uraia hawezi kushiriki uchaguzi.maoni yangu haya yanatokana na imani kuwa kama tunavyoona miaka3 mbele kutakuwa na wapiga kura wengi vijana ambao sasa wana miaka 17,16 na 15.yawezekana kabisa baada ya kuandikisha sasa usitokee uandikishaji mwingine.Mimi siamini tena katika programu za serikali hii.tulipoambiwa kusajili simu kulikuwa na mbwembwe kubwa na vitisho.Baadhi yetu hatimaye kwa kujua umuhimu wa kusajili namba za simu lakini tukijua pia usanii wa watawala tulikubali shingo upande.NINI kilitokea? hata baada ya kutangaza mwisho wa kusajili na nyongeza kwisha,hadi leo unaweza kununua line na kuitumia bila kusajili hadi siku kadhaa.hadi leo baada ya usajili watu wanafanya ujangili na kutukana na kutishia wenzao bila serikali wala mamlaka za mawasiliano kufanya chochote.lakini kwa wenye kukumbuka wakati wa uchaguzi mkuu,kampuni fulani waliruhusu namba za wateja wao kutumiwa meseji za kampeni na CCM.sasa mimi nimeota sugu na sifanyi tena programu yoyote ya serikali ya ccm mpaka itapokuja serikali ya chama kingine kitakachorudisha utawala wa sheria.hivyo sitaomba na wala sihitaji kuwa na kitambulisho cha taifa.(kwa sasa kwangu ni aibu kujitambulisha kama mtanzania) kwa wanaonitia hofu eti oooh utakosa visa,paspoti,ajira na haki ya kuchaguliwa,nawajibu kuwa naweza kuishi bila shida bila hayo na kuhusu ajira sioni shida kwani hata sasa sinayo na si kwa sabababu ya vitambulisho vya taifa.Simu ikitokea hizi ninazotumia zikapotea sitahangaika na kuzirudisha.kwa wanaotaka kujua nitafanya nini kuwasiliana? nitatumia komputer (au mnasahau kuwa tumeingia digitali? nayo ni ngonjera nyingine.kwa wasiojua zipo simu zisotumia line.
  Na Kwa hiyo sitashiriki SENSA kwa sababu hizohizo (siyo za kidini.mimi ni mkristo).Nani anaweza kunijibu kuwa ikiwa sensa inaisaidia serikali kupanga mipango yake ni kwa nini baada ya sensa iliyopita miaka kumi kuna watoto wamemaliza shule ya msingi wakafaulu lakini wakakosa nafasi kwa kuwa hakuna madarasa ya sekondari.serikali haikujua kuwa miaka saba baada ya sensa watoto walio dara sa la kwanza wataanza sekondari? serikali bado iseme inatumia takwimu kupanga maendeleo yetu au programu ndiyo shughuli yenyewe ya maendeleo ya vigogo.Kwa kweli NATAMANI KUHAMA NCHI
  Masala Kulangwa
   
 2. RGforever

  RGforever JF-Expert Member

  #2
  Aug 22, 2012
  Joined: Apr 3, 2011
  Messages: 6,165
  Likes Received: 1,890
  Trophy Points: 280
  We umeambiwa Zoezi si la kudumu! Si ataandikishwa akifikia miaka 18.....
   
 3. Bra-joe

  Bra-joe JF-Expert Member

  #3
  Aug 22, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,559
  Likes Received: 510
  Trophy Points: 280
  Wewe ni kilaza wa hali ya juu. Vitambulisho vya taifa ni zoezi la milele, mtanzania yoyote akiwa na miaka 18 au zaidi anaweza kuomba na akapewa. Baada ya muda fulani kila mtanzania atalazimika kuwanacho apende asipende. Matumizi yake ni haya; 1. kujiandikisha elimu zote za juu ni lazima ukionyeshe. 2. Huwezi kusajili mali zako (gari, nyumba, shamba au akaunti ya banki) bila ya kuwa na kitambulisho cha taifa. 3. Kila unapotembelea kunapotolewa huduma za serikali kama uhamiaji, hospitali, mahakamani n.k ni lazima kuonyesha kitambulisho cha taifa kabla hujahudumiwa. 4 ukitaka kuajiliwa au kusajili biashara yoyote kitambulisho cha taifa ni lazima. Je, unaweza kuwa na maisha bora bila ya mambo tajwa hapo juu? Hili siyo swala la kisiasa ni la kitaifa.
   
 4. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #4
  Aug 22, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Ndugu kama vitaanza kutolowa kisheria ni kuanzia 18 years na nchi nyingine ni 15 years.
  mtoto atakuwa na atapewa.

  jiulize kwanza kwanini nchi tajiri kama UK na US hawana vitambulisho vya Taifa bali watumia passports, driver licence katika kupata huduma?
  Jiulize kwanini nchi za Afrika hazitumii vitambulisho hivi ya kielectronic?ila wanatumia vya bar code technology.
  jiulize kwanini NIda ilikwa watoe vitambulisho April lakini wameshindwa kwa kukosa fedha? ni ajabu nchi kutaka kuanzisha vitambulisho vya garama kwa kutegemea fedha za wahisani.
  ndio vitambulisho vya taifa ni muhimu lakini wamekurupuka kutangaza kutoa wakati hawana fedha wala teknolojia ya kuvitumia
  si ajabu ikachukua muda kuwezesha huu mradi wao.time will tell

   
 5. Bra-joe

  Bra-joe JF-Expert Member

  #5
  Aug 22, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,559
  Likes Received: 510
  Trophy Points: 280
  Na wewe pia kilaza. Hao wa marekani na waingereza wanatumia pasipoti au leseni ya udereva kupata huduma kwa sababau walitumia vitambulisho vya taifa (Id card) kufanya maombi ya hizo pasipoti au leseni za udereva, katika pasipot au leseni zao kuna namba ya kitambulisho cha taifa ambayo inashabiiana na namba ya leseni au pasipoti, kwahiyo wakiingiza namba ya leseni au pasipoti pia namba ya kitambulisho cha taifa inaonekana. Leseni au pasipoti vinaweza kutumika kama vitambulisho (ndiyo maana wanaweza kupata huduma ktk ofisi za serikali) lakini huwezi kupata leseni au pasipoti kama huna kitambulisho cha taifa.
   
 6. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #6
  Aug 22, 2012
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Nida wanajua sababu.
   
Loading...