Kwa nini watanzania tunatabia hii?

Kwa nini watanzania tunatabia hii?

Bra-joe

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
1,850
Reaction score
1,449
Habari Jf? Kupenda visivyo vyetu. Hii ni tabia ya watanzania wengi. Mifano: watu wengi wanashabikia mashindano ya mpira wa nje kuliko ya hapa Tz, mwanamke/mwanaume hata akiwa mbaya vipi akioa/olewa watu wengine watamtaka, akija mgeni kutoka nje ya nchi atashobokewa kuliko raia, tukiona kitu kimeandikwa kimetengenezwa Tz tunakitilia mashaka au hatukitaki kabisaa, mtu kuhudumia au kutoa penzi zaidi nje ya ndoa/mahusiano kuliko kwa mwenza wake. Tubadilikeni jamani! Vyetu ndiyo mpango mzima.
 
Kaa mkao wa kurushiwa mawe lolz.. Mie simooooo!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
:rockon: Vitu vya nje hasa ulalya ulaya vitamu/vizuri.....:rockon:
Kama wanawake wanapenda mawigi na manywele, mikucha bandia kuliko asili tufanyeje.....!:rockon:
 
mmmmmh kila mtu ana uhuru wa kuchagua anachikitaka bhana ilimradi tu usivunje sheria,kosa ni kwa wale wanaovuka mipaka 'CHOICE IS MINE'
 
Habari Jf? Kupenda visivyo vyetu. Hii ni tabia ya watanzania wengi. Mifano: watu wengi wanashabikia mashindano ya mpira wa nje kuliko ya hapa Tz, mwanamke/mwanaume hata akiwa mbaya vipi akioa/olewa watu wengine watamtaka, akija mgeni kutoka nje ya nchi atashobokewa kuliko raia, tukiona kitu kimeandikwa kimetengenezwa Tz tunakitilia mashaka au hatukitaki kabisaa, mtu kuhudumia au kutoa penzi zaidi nje ya ndoa/mahusiano kuliko kwa mwenza wake. Tubadilikeni jamani! Vyetu ndiyo mpango mzima.

Ni kweli Bra-joe. Hii tabia ya kushobokea vitu vya nje na kuponda vya kitanzania nimeiona kwa watz
wengi. Hata kwenye sherehe zetu (ubatizo, send-off, harusi nk) utamsikia mc anasema:"Bibi harusi
kang'ara ama hajang'ara? Yaan mtoto mashallah utafikiri katoka ulaya yaani alivyopendeza" Hapa maana yake vitu
vizuri vinatoka ulaya! Sijui ni kwa sababu ya kutaliwa pengine ndo maana tuna hii kasumba. Halafu hii
kasumba inatukuzwa sana na viongozi wetu (wanasiasa) kiasi cha kutishia uchumi wetu. Transformer nzuri sio
ile inayotengenezwa TANELEC ila ni ile ya India au uingereza.Mtu akiwa na hamu ya kunywa juice anaacha
machungwa fresh ya usambaa, anaingia supermarket kununua pakiti ya juice kutoka Dubai!Mtu akiambiwa hii bidhaa
imetengenezwa Tanzania anasita kununua na kwenda kutafuta bidhaa hiyo mahali pengine. Tuna kasumba
ya ajabu sana wajemeni!

Kama kuna wakunitupia jiwe anitupie tu ila anieleze kwa nini kiongozi mmoja alihitaji msaada wa makachero wa nje ilhali sisi tunao?
 
Tunaushamba na ulimbukeni, ukianzisha kitu mtz kinapondwa na wateja utakosa acha kianzishwe na mzungu hata kama bomu basi wateja kibao. Mie dukani kwangu nimemtafuta mzungu koko mmoja ndiye anaye uza, nauzaje?
 
Sio vibaya kulinganisha vitu vya ndani na vinavyotoka nje ya nchi,lakini pia uwezi kulazimisha mtu apende vitu kutoka ndani atakama ni vibovu eti ni kwakuwa ni vyatanzania,njia mojawapo ya kuondoa ili tatizo nikuwana vitu vizuri na madhubuti kwani hapo ndo tunaweza kujisikia vizuri kupenda vitu vya ndani.Chaguo analo mtu mwenyewe atakama akichagua kisichokufurahisha wewe
 
mmmmmh kila mtu ana uhuru wa kuchagua anachikitaka bhana ilimradi tu usivunje sheria,kosa ni kwa wale wanaovuka mipaka 'CHOICE IS MINE'

Asnam, hujawahi kupendwa/kumpenda mume wa mtu?
 
Tunaushamba na ulimbukeni, ukianzisha kitu mtz kinapondwa na wateja utakosa acha kianzishwe na mzungu hata kama bomu basi wateja kibao. Mie dukani kwangu nimemtafuta mzungu koko mmoja ndiye anaye uza, nauzaje?

Nata umenikumbusha, nataka kufungua hospitali halafu nitafute wazungu machafuchafu wawe madokta labda nitapiga hela kama wewe.
 
Sio vibaya kulinganisha vitu vya ndani na vinavyotoka nje ya nchi,lakini pia uwezi kulazimisha mtu apende vitu kutoka ndani atakama ni vibovu eti ni kwakuwa ni vyatanzania,njia mojawapo ya kuondoa ili tatizo nikuwana vitu vizuri na madhubuti kwani hapo ndo tunaweza kujisikia vizuri kupenda vitu vya ndani.Chaguo analo mtu mwenyewe atakama akichagua kisichokufurahisha wewe

je kwa wale wasiopenda wenza wao au kushobokea mtu kisa tu katoka nje ya Tz? Unasemaje?
 
Una akili wewe!!! Hakuna dhambi yoyote ile kwa Watanzania kupenda kitu ambacho si cha Kitanzania. Kama kuna kitu cha Kitanzania kiko bomba Watanzania watakifagilia. Mbona misosi yetu inafurahiwa sana na Wabongo hata wengi walio nje ya nchi wanakula misosi ya Kibongo na kuagiza kila mara au kubeba kila wanaposafiri toka bongo kurudi kwenye maskani yao? Kitu kama bomu basi hakuna sababu ya kukifagilia kwa sababu ni cha kwetu tu.

mmmmmh kila mtu ana uhuru wa kuchagua anachikitaka bhana ilimradi tu usivunje sheria,kosa ni kwa wale wanaovuka mipaka 'CHOICE IS MINE'
 
Bongo kila kitu feki... Mpaka baadhi ya wanawake ni fekero!!!!!!!
 
Nata umenikumbusha, nataka kufungua hospitali halafu nitafute wazungu machafuchafu wawe madokta labda nitapiga hela kama wewe.
Sasa wewe Bra-joe unatafuta murder cases, hayo ya hospital yanataka watabibu haswa, waliosomea, duka simple bana!
 
Last edited by a moderator:
Sasa wewe Bra-joe unatafuta murder cases, hayo ya hospital yanataka watabibu haswa, waliosomea, duka simple bana!

hapo si itakuwa imemechi, dokta bandia na madawa bandia, au ujasikia yale mambo ya ARVs na wale wanaotumia dozi 3 tofauti za malaria lakini hawaponi? Tupunguze kupenda vya nje, siku 1 watatuletea sumu.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom