kwa nini Watanzania tunapenda SHORT CUTS.

Mbeu

Member
Jan 22, 2011
35
0
Hivi karibuni hapa arusha mtaa wa sakina (white rose) Kuna mradi mkubwa wa maji umeanzishwa hawa jamaa (Mafundi) wa AUWASA wamekuwa wakitapeli watu ili wawafungie maji chapu! chapu! wengi wamelizwa. kiaminika wengine wametoa mpaka laki nne ili wapate maji Waziri unaye husika na hili swala naomba ulifuatilie kwa ukaribu sana maana wafanyakazi wako hawana ethics wamejaa ulafi usio na mipaka, embu jamani wapandishieni mishahara njaa imezidi. wakazi wa mtaa wa Sakina(white rose) tunashindwa kuelewa haya mambo ni ya Kifisadi au ni haki ya kila raia kupata huduma. wengi wa wakazi wa hapa mtaani hawajaenda shule, kwa hiyo hawajui haki zao za msingi. alafu kuna jamaa fulani wameunganishiwa maji bila kufuata taratibu, hawa mita hawaja jaza hata form za maombi ya tawi la maji.
 
Back
Top Bottom