ngoshwe
JF-Expert Member
- Mar 31, 2009
- 4,131
- 931
Kila hatua ya kukua kwa mwanadamu inaendana na kukutana au kutokutana na mambo fulani katika hii dunia. Ukizaliwa, siku ya kwanza (hujitambui kabisa) lakini watu watakuja kukuona na kujaribu kukufananisha na wale ambao tayari wapo duniani nk .nk Lakini huwezi kuwatambua hao.
ukifikia umri wa kujitambua , utaweza kuwatambua kwanza na kuwatofautisha tabia, sura, sauti na jinsia wale waliokuleta duniani (baba na mama yako) kama wao pamoja. Baadae utajitambua wewe mwenyewe kisaikolojia (jinsia yako, rangi, tabia, vitu unavyopenda na usivyopenda, unavyojua na usivyojua nk nk).. Baadae utajitambua zaidi, ndipo utaanza kujitofautisha wewe na wengine, hapo utachagua marafiki na maadui, raha na tabu nk nk., Ni katika kipindi cha kujua jema na baya pia, binadamu huwa ana hangaika kupata yote mema, utataka mzazi wema, utaomba uwe na rafiki mwema, utataka upate mke au mume mwema,uwe na watoto wema, upate kazi njema na mshahara wa kukuweka sehemu "njema", ule, unywe na ulale vyema, uonekane kwenye jamii kuwa wewe upo njema na unatenda yaliyo mema siku zote!
Hata hivyo, inaonekana kuwa tabia za wanaume mara nyingi huwa zinatofautiana na za wanawake tokea utoto.....hisia za kufanya yaliyo mema siku zote kwa wanawake ni kubwa zaidi kuliko wanaume, na wanawake hisia hizo zimejengwa na huruma, mapenzi na pengine hofu nyingi za kukosea, kwani kukosea kwao inakuwa ni sawa na kutenda dhambi kubwa....na kuwa wanawake huwa wanaweza kutunza siri kubwa moyoni, na pengine hata ile inayomuua. Cha kushangaza, kwa upande mwingine, hao hao wanawake ndio wanaonekana kuwa wavujisha siri kwa kiwango kikubwa sana katika jamii kuliko hata wanaume....
Je, kwa nini ipo hivi?