Kwa nini wanawake wapo hivi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini wanawake wapo hivi?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by ngoshwe, Feb 1, 2010.

 1. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #1
  Feb 1, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,089
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Kila hatua ya kukua kwa mwanadamu inaendana na kukutana au kutokutana na mambo fulani katika hii dunia. Ukizaliwa, siku ya kwanza (hujitambui kabisa) lakini watu watakuja kukuona na kujaribu kukufananisha na wale ambao tayari wapo duniani nk .nk Lakini huwezi kuwatambua hao.

  ukifikia umri wa kujitambua , utaweza kuwatambua kwanza na kuwatofautisha tabia, sura, sauti na jinsia wale waliokuleta duniani (baba na mama yako) kama wao pamoja. Baadae utajitambua wewe mwenyewe kisaikolojia (jinsia yako, rangi, tabia, vitu unavyopenda na usivyopenda, unavyojua na usivyojua nk nk).. Baadae utajitambua zaidi, ndipo utaanza kujitofautisha wewe na wengine, hapo utachagua marafiki na maadui, raha na tabu nk nk., Ni katika kipindi cha kujua jema na baya pia, binadamu huwa ana hangaika kupata yote mema, utataka mzazi wema, utaomba uwe na rafiki mwema, utataka upate mke au mume mwema,uwe na watoto wema, upate kazi njema na mshahara wa kukuweka sehemu "njema", ule, unywe na ulale vyema, uonekane kwenye jamii kuwa wewe upo njema na unatenda yaliyo mema siku zote!

  Hata hivyo, inaonekana kuwa tabia za wanaume mara nyingi huwa zinatofautiana na za wanawake tokea utoto.....hisia za kufanya yaliyo mema siku zote kwa wanawake ni kubwa zaidi kuliko wanaume, na wanawake hisia hizo zimejengwa na huruma, mapenzi na pengine hofu nyingi za kukosea, kwani kukosea kwao inakuwa ni sawa na kutenda dhambi kubwa....na kuwa wanawake huwa wanaweza kutunza siri kubwa moyoni, na pengine hata ile inayomuua. Cha kushangaza, kwa upande mwingine, hao hao wanawake ndio wanaonekana kuwa wavujisha siri kwa kiwango kikubwa sana katika jamii kuliko hata wanaume....


  Je, kwa nini ipo hivi?
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Feb 1, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 80,463
  Likes Received: 117,261
  Trophy Points: 280
  Kuna haja ya kutoa mifano hai ili kusupport hitimisho lako, vinginevyo litakuwa halina mvuto. Kwa maoni yangu hata wanaume nao kwa namna moja au nyingine wanavujisha siri hivyo sijui ni vigezo gani ulivyotumia na kuhitimisha kwamba Wanawake ndiyo wanaovujisha sana siri kuliko wanaume.
   
 3. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #3
  Feb 1, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,089
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  [​IMG]


  sitakwenda kwenda mbali sana,

  Take this few.

  1. Eva vs Satan.
  1. Delila vs Samson,
  2. Clinton vs Monica,
  3. Tigger wod vs Rachel Uchitel, Jamie Grubbs, Kalika Moquin, Jamie Jungers, Mindy Lawton, Cori Rist,Holly Sampson,Holly Sampson,Loredana Jolie,Julie Postle,Theresa Rogers.
  4. Peter Robinson vs his wife
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...