Kwa nini wanataaluma wetu hukimbilia siasa?

MwanaFalsafa1

MwanaFalsafa1

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2008
Messages
5,566
Likes
29
Points
135
MwanaFalsafa1

MwanaFalsafa1

JF-Expert Member
Joined Feb 26, 2008
5,566 29 135
Kwanza napenda nianze kwa kusema sina neno na kuwa na wanasiasa ambao wamebobea kwenye taaluma zao. Natambua kwamba mtu hasomei siasa kwa hiyo mwanasiasa yoyote kazima atakuwa na taaluma fulani nje ya siasa. Pia natambua madhara ya kuwa na viongozi wengi ambao hawana kisomo kikubwa. Mwisho niseme pia kwamba natambua kwamba siyo wanasiasa wote "wasomi" wana visome halali au vya kueleweka.

Tatizo langu ni kwamba inaelekea Tanzania kuna wimbi la wanataaluma ambao wanaona ni heri kuwa wanasiasa kuliko kufanya kazi walizo somea. Ingekuwa wachache ningeelewa ila sasa inabidi nijiulize kwa nini wengi hukimbilia siasa? Kwenye Bunge letu na hata serikalini kumejaa "madokta" tena wengine wenye specializations lakini bado ukiangalia hospitali zetu tunaambiwa kuna upungufu wa wataalamu.

Kuna watu kama Prof. Lipumba. Mseme utakavyo huyu bwana lakini ni jambo lililo wazi kwamba ni mchumi aliebobea hata kipindi fulani kuwa mshauri wa raisi. Prof. Lipumba kila leo ana gombea uraisi lakini huishia kapa. Kwa nini asifanye kazi inayo husisha taaluma yake baada ya kung'ang'ania siasa?

Mtu kama Prof. Kapuya ina tambulika kabisa kuwa ni mtaalamu wa mifupa. Kwenye nchi iliyo na upungufu wa madaktari bingwa kwa nini huyu bwana hashughuliki na taaluma yake?

Nime taja hawa baadhi siyo kwa ajili ya kuwa single out ila kama kutolea mfano watu ambao nina uhakika na elimu zao. Kwenye siasa leo upo kesho haupo. Kwenye siasa ina tegemea sana na mazingira. Kwa nini wanataaluma hawa washughulike na siasa ambayo ni bahati nasibu kuliko kutumikia taaluma zao?

Mimi naheshimu sana watu kama wakina Prof. Othman Haroun (R.I.P.) na Prof. Shivji. Hawa ni wanataaluma ambao hawaja kimbia taaluma yao. Inapo bidi wanaikosoa serikali ila hawaingii kwenye siasa. Kwa nini na wengine wasifanye hivyo?

Katika nchi yoyote dunia kazi mbali mbali zina hitajika kuendeleza taifa. Siasa siyo mahali pekee kwa kuleta mabadiliko na mageuzi. Tuki kazania siasa na kupuuzia taaluma zetu tuta jikuta tuna geuka nchi ya wanasiasa tupu isiyo na mabadiliko yoyote. Je tatizo ni nini?
 
The Son of Man

The Son of Man

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2010
Messages
12,556
Likes
2,368
Points
280
The Son of Man

The Son of Man

JF-Expert Member
Joined Feb 9, 2010
12,556 2,368 280
Pesa bila jasho mkuu ndo maana wanakwenda huko!
 
N

Nonda

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2010
Messages
13,257
Likes
1,999
Points
280
N

Nonda

JF-Expert Member
Joined Nov 30, 2010
13,257 1,999 280
Mkuu,

Siasa katika nchi yetu imekuwa ni short cut ya kuwa katika kikundi kidogo cha wanaofaidi national cake. Profs wengi, na drs wengi huhenyeka huko vyuoni wakitia, mkono mfuko wanakuta mfuko umetoboka. Wahadhiri wengi inawapasa wawe na vijimradi pembeni vya kuweza kuyamudu maisha.

Ningekutolea mifano hapa lakini wee wacha tu...

Serikali bado haiwathamini ipasavyo wasomi wetu. Wataalamu wetu. Mishahara waipatayo hailingani na hadhi ya kisomo chao na hela wanayoipata haikidhi mahitaji yao;wanapowatizama wanaoingia katika siasa huwa haichukuwi muda huanza kung'aa, kutoka vitumbo, vx, majumba nk kwa hiyo wanaona ,ok!!?? that is the way!
Ndio unawaona wanaongezeka huko. wanakimbilia huko sasa.

Simply, siasa hapa kwetu imekuwa short cut kwa at least mtu kuweza kumudu maisha na kupata lines za kutengeneza mahela.
 
K

Koba

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2007
Messages
6,143
Likes
506
Points
180
K

Koba

JF-Expert Member
Joined Jul 3, 2007
6,143 506 180
its all about the benjamins!
 
MwanaFalsafa1

MwanaFalsafa1

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2008
Messages
5,566
Likes
29
Points
135
MwanaFalsafa1

MwanaFalsafa1

JF-Expert Member
Joined Feb 26, 2008
5,566 29 135
Mkuu Nonda,

Katika nchi yoyote mishahara ya publix sector ni midogo kulinganisha na private sector. Hata kwa nchi kubwa kama Marekani mtu anaye fanya kazi public sector ana lipwa hela ndogo kuliko mtu anae fanya kazi hiyo hiyo kwenye private sector. Ila je kwa nini bado wenzetu wana wafanyakazi wa public sector ambao wapo dedicated na committed? Ni kwa sababu wenzetu wanaichukulia kama public service and they are not in it for the money.

Natambua huku kwetu mishahara ni midogo. Na ndiyo maana kwetu ina hitaji moyo zaidi kufanya baadhi ya hizi shughuli. Ila kinacho nishangaza ni kitu kimoja. Wengi wa hawa wasomi wetu at some point in their academic career iwe kwenye undergaduate, masters au PhD wali somea nje ya nchi. Wali somea kwenye nchi ambazo wange amua kubaki mshahara unge kuwa mkubwa zaidi. Waka rudi nyumbani waki tambua mishahara watakayo ipata ni midogo kuliko nchi walizo some. Je kwa nini wali rudi japo wali tambua hilo? Kwa nini wakati wa kurudi hawa kuona swala la pesa ni kigezo kikuu? Lakini at some point in their careers wanaona bora kuingia kwenye siasa?

Na mimi naamini kabisa wataalamu wetu wanaweza jiendeleza nje ya siasa. Mtu ukiwa kwa mfano daktari hauwezi anzisha hospitali yako? Ukiwa engineer hauwezi anzisha kampuni yako ya uhandisi nk? Na hawa wataalamu wetu siyo lazima waajiriwe kwenye public sector. Wanaweza hata ajiriwa kwenye private sector wakala mishahara inayo shindana na wabunge au hata mawaziri. Tena kuna baadhi ya kazi wanalipwa kuliko viongozi wa serikali. Kwa nini huko hawa kuoni wanaona siasa?
 
Vizuri umetowa mfano wa ulaya na marekani, ukiwa na kiwango hicho cha elimu, ukipata kazi huko at least unajuwa una hela za kukutosha kwa mahitaji yako.

Wengine hurudi kwa uzalendo ila baadae huwashinda njiani

Pia wanaporudi TZ huwa wanamidomo mingi zaidi ya kuilisha na wanakuwa wapo karibu. Huwa hawana njia ya kuwaepuka. Fikiria aje mjomba wako anakulilia shida mjomba sijala leo siku ya pili, n. k na watakuja wengi. Si unayajuwa maisha ya bongo?

Kweli, wengine hufanya kazi za consultancy, lakini mkuu wanapowatizama wanasiasa wanawaona wana-enjoy life na wao wanahenyeka. Huwa tempted kwenda huko. Kazi za wito huona hazina faida. Wengine wanavutwa huko na rafiki zao ili wapewe ulaji.

Nilisoma humu JF, kuna member ameuliza yule Masumbuko Lamwai yuko wapi? Itafute hii thread , utacheka na utahuzunika , jawabu zilivyokuja huko. Mmoja anasema kamtafute …. Beach huko kwenye nyumba yake ambayo hadi leo hajaimaliza kuijenga.

Sasa kama unamjuwa huyu dr. Lamwai na miaka aliyofundisha pale Mlimani na kama hayo ni kweli, utafahamu kwa nini aliingia siasa.
Nawapa nafasi wengine kuchangia,.. mimi … mambo ya nchi yangu yananitia kizungu zungu, mkuu.

Questt

Questt

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2009
Messages
3,013
Likes
30
Points
135
Questt

Questt

JF-Expert Member
Joined Oct 8, 2009
3,013 30 135
Chunguza Mishahara ya Wagomaji wa pale MNH na mishahara ya Wabunge, hata ukichukua difference tu itatosha kuwalipa walimu kama 100 hivi...Kifupi SIASA imekuwa the best short cut ya kuukacha Umasikini......... Sababu ni kama zifuatazo......

1. mazingira ya kazi. Umetolea mf. madaktari nami nibaki hukohuko, ukiangalia jinsi mwanasiasa anavyofanya kazi anakua kwenye mazingira Bora zaidi ya Dk pale Amana au Hosp yoyote ile nchini. Mbunge anakua mjengoni pale dododma. Full Mufindi (AC) hakuna joto na wala hakuna kuvaa Apron ila anavaa suti kali na tai na ataingiza hata kama hatasema neno lolote ndani ya Mjadala mzima wakati dk anakua na foleni ya wagonjwa......obvious dk atachoka

2. Heshima- Dk ana heshimikia sana katika jamii ila mbunge ni zaidi thus y huwa wanaitwa Waheshimiwa, na wengi wetu tunapenda kuheshimiwa kuliko kuheshimu.

3.Maslahi: hili ndiyo kubwa zaidi kaka, hawa wana kazi mbili tofauti, mmoja anatumia akili kdg na maneno mengi possibly bila NGUVU yoyote kutumika hapa namaanisha mwanasiasa na Dk atatumia akili nyingi, maneno kdg (hasa maswali kwa mgonjwa kupata history) na Nguvu s'time lakini mwanasiasa anamarupurupu na Mshahara wa Nguvu kuliko plus VX JIPYAAAAAAAA baada ya kuapishwa, nani halitaki hili??????
 
czar

czar

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2010
Messages
340
Likes
2
Points
0
czar

czar

JF-Expert Member
Joined Oct 11, 2010
340 2 0
Inalipa kuliko maelezo tena bila jasho hasa ubunge, kiinua mgongo baada ya aka 5 ni kama 45 something million sasa nani ataacha.
 
Forum statistics

Threads 1,236,936
Members 475,327
Posts 29,273,657