Kwa nini wanashindwa kuongea live?

michelle, ni wachache sana wanafanya hivyo..labda hao wa chapchap..mimi kwa upande wangu, enzi zangu, nikikuzimia tu, sitaki kupata shida, nakuja tu laivu nakwambia kuwa nimekuzimia na ninataka either kukuoa au ...chochote...tena nakuangalia macho makavuu usoni bila wasiwasi..ukinikatalia mbona wanawake wengi tu mtaani, naenda kwa mwingine....ukiona mtu anazugazuga, sijui ni wa namna gani.

hivi bado kuna wanaopigwa vibuti miaka hii
 
ule ni uwoga na aibu ila huwa kuna umri ile hali huwa inapotea yenyewe.....so worry not guys
 
Kwa nini mtu mnakuwa pamoja kila siku, mnazungumza mambo mengi tu, lakini anapotaka kuanzisha uhusiano wa kimapenzi anakuandikia kadi au sms. Kwa nini watu wanashindwa kuongea live!?

Kukataliwa live nako kuna changamoto zake. Ila mimi naamini ni rahisi zaidi kumshawishi mtu kama ukimweleza live kuliko hii ya sms ambayo anaweza kabisa kukataa bila kuona soni.
 
Inaleta raha sana hii maana mwanaume anaonekana shujaa sana kama zamani watu shujaa tu ndio walikuwa wanapata madem sababu lazima ujitose mzimamziam sio siku hizi hata madomo zege nao wanatupa visms vyao wamemaliza, mapenzi yameingiliwa sana siku hizi

Ati mtu anatongozwa kwa sms na anakubali, duh!
 
Kwa nini mtu mnakuwa pamoja kila siku, mnazungumza mambo mengi tu, lakini anapotaka kuanzisha uhusiano wa kimapenzi anakuandikia kadi au sms. Kwa nini watu wanashindwa kuongea live!?

Hilo si sawa na maongezi mengine. Maongezi ya kawaida yanakuja kikawaida na kujibishana kikawaida lakii ya Mapenzi yanataka nakshi na huchukuwa muda kujibishana. Na ndio sababu wengi humpa nafasi mwenziwe afikirie kwa wasaa, hivyo kutumisha kadi au barua kunatowa nafasi kwako kufikiri cha kujibu.
 
Back
Top Bottom