Kwa nini viongozi wengi wa Tanzania wanapenda UNAFIKI

Nzowa Godat

JF-Expert Member
Jun 15, 2011
2,783
819
NA KULWA MAGWA,
DODOMA
WAZIRI wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa,
Benard Membe, amesema
watuhumiwa wa suala la
ununuzi wa rada
uliolisababishia taifa hasara
kubwa, wanafahamika. Akijibu
hoja za wabunge mbalimbali
waliochangia hotuba ya bajeti
ya wizara yake juzi, Membe
alisema suala la watuhumiwa
hao linashughulikiwa na
mamlaka zinazohusika.
Alisema sio jukumu la wizara
hiyo kutaja majina wala
kushughulikia suala
linalohusiana na tuhuma hizo,
isipokuwa anachofanya kwa
sasa ni kuhakikisha fedha
zilizoamriwa na Mahakama ya
Uingereza kurejeshwa
Tanzania, zinarejesha.
"Watuhumiwa wa suala la rada
wapo, wanajulikana, ila hilo sio
suala la wizara yangu kutaja
(majina), lakini huko mbele ya
safari watajulikana tu, "alisema
Membe.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom