Kwa nini tunalalamika tu?

RUV ACTVIST.

JF-Expert Member
Jan 14, 2012
472
110
Nimejiuliza hili swali kwa muda mrefu, kwa nini watz tunalalamika tu bila kuchua hatua? Wasomi wanalalamika, wasiosoma wanalalamika nani achukue hatua?
Hivi kweli tukiungana wtz wote, wasomi wetu, viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa hawa mafisadi watatushinda? Hatuwezi kweli kuuondoa ufumo tunao ulalamikia? Au tunalalmika kiunafiki na kwamba tunaupenda mfumo unaolea wahalifu ili na sisi tukipata nafasi tuwe hivyohivyo?
Utakuta mtu anasema mi sipendi siasa, lakini haachi kulalamika, anataka nani amsaidie kudai haki yake? Au pengine watu hawajui siasa manake nini?
Mbaya zaidi sikuhizi kumezuka matindo wa watu kusema huyo ni chadema eti kwa kuwa anadai haki yake, imekaaje hii?
 
Vyama vipo, wanaharakati wapo, viongozi wa dini na wewe upo! Tuambie tuanzie wapi au tuanze vipi?
 
Muulize JK kwa nini analalamika kila siku, Pinda naye analalamika waulize kwanza nadhani ndio wao watatoa jibu sahii
 
Kulalamika siyo kubaya, ni hatua muhimu kudhihirisha kuchukia jambo na pia kunajenga hasira na chuki ambyo ni muhimu kuchukua hatua. Tatizo kama unavyosema wote tunaishia kulalamika.

Tufanye nini?

Tukubali tumekwama. Tutafuta tatizo linalotuzuia kwenda zaidi ya kulalamika ni nini na tupange mikakati ya kuondoa hiki kikwazo
 
Kila member wa JF atenge muda wa arudi kijijini kwao/katani kwao aeleze ubaya wa mfumo uliopo, aeleze kwa ndugu zake, marafiki, zake majilani, viongozi wa dini n.k kwa maana ya kutoa elimu ya uraia.
Tuwahimize watu umuhimu wa kujiandikisha na kupiga kula na kuzilinda. Tuwafundishe watu umuhimu wa kujua kudai uwajibikaji kuanzia ngazi ya kijiji. Mi nadhani tukifanya haya tutafanikiwa.
 
Kulalamika ni hatuwa ya mwanzo ya kutoridhika. Hatuwa inayofwata ni vitendo. Kumbuka.......Mfumo wenyewe unaokera unatumia kupiga ramli. Hata wananchi wanapoamua kuchukuwa hatuwa haraka wanatambulika na kupigwa stop. Bado hawakaa na njaa kwa masiku na hapo watapata mbinu za action za kisheria.
A HUNGRY MAN IS NA ANGRY MAN
 
Mpaka hapa bado sijapata saluhu . Kila aliyechangia ana element za kulalamika. Tumelalamika kwa miaka 50 naamini itatuchukua mingine km hiyo kuchukua hatua.
 
Nimejiuliza hili swali kwa muda mrefu, kwa nini watz tunalalamika tu bila kuchua hatua? Wasomi wanalalamika, wasiosoma wanalalamika nani achukue hatua?
Hivi kweli tukiungana wtz wote, wasomi wetu, viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa hawa mafisadi watatushinda? Hatuwezi kweli kuuondoa ufumo tunao ulalamikia? Au tunalalmika kiunafiki na kwamba tunaupenda mfumo unaolea wahalifu ili na sisi tukipata nafasi tuwe hivyohivyo?
Utakuta mtu anasema mi sipendi siasa, lakini haachi kulalamika, anataka nani amsaidie kudai haki yake? Au pengine watu hawajui siasa manake nini?
Mbaya zaidi sikuhizi kumezuka matindo wa watu kusema huyo ni chadema eti kwa kuwa anadai haki yake, imekaaje hii?

Hizo ndio zetu wa Bongo kulalamika tu, vitendo hatuwezi, tunaishia kusema nchi ina amani.
 
tatizo lingine ni kutojiamini na kupenda kupewa, angalia mafisadi wanavyomwaga sadaka makanisani na wanavyopewa heshima hapo ndio utatujua vizuri
 
Shibe kitu kibaya.mtoa hoja mpaka dakika ya mwisho lawama hazishi bali zinapungua kimtindo kuziba midomo ya kizazi kipya
 
Back
Top Bottom