OMJ
JF-Expert Member
- Apr 24, 2013
- 210
- 28
Acha mashine hizo zitumike ili wafanyabiashara wasikwepe kulipa kodi. ZAMA za kuleta janja ya nyani kula mahindi mabichi zimepita. Ukichunguza vizuri utagundua wengi wao hawazitaki hizi mashine kwa sababu moja tu, hawataki serikali iyajue mapato yao, ili waendelee kukwepa kulipa kodi.
Mbona wafanyakazi walioajiriwa, iwe serikalini au private sectors wanakatwa kodi moja kwa moja kabla hata hawajapokea mishahara yao, na hawalalamiki, sawa iweje hawa wafanyabiashara wakagomee mfumo huu wa matumizi wa mashine za EFD?
Wafanyabiashara tubadilike.
Tulipe kodi Kwa maendeleo ya nchi yetu. Tazama jirani zetu Kenya, asilimia kubwa ya bajeti yao inatokana na mapato ya ndani, yaani mfumo mzuri uliowekwa wa ukusanyaji wa kodi, na kiasi kidogo sana cha bajeti yao kinatokana nchi wafathili.
Mjadala mzuri, ila wafanyabiashara wanaumia sana. Imagine Mashine 700,000, Leseni Sh 300,000, Bado SDL (0.06) Ya jumla ya mshahara, kodi ya pango ( varies), na mengine mengi. Na pia mfumo wa kodi haueleweki longolongo nyingi. TRA wanachohitaji ni target za kufikia kiwango walichojiwekea kama dira yao. Hebu cheki;-Mfanyabiashara mdogo analipa hadi milioni 3 kwa mwaka. Je yupo kwa ajili ya kuendeleza maisha yake au kuifaidisha serikali?. Tutafakari ukweli!, Mazingira rafiki hakuna , madhara ni tax evasion