Kwa nini tbc1 haionyeshi mechi zinazoihusu timu ya taifa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini tbc1 haionyeshi mechi zinazoihusu timu ya taifa?

Discussion in 'Sports' started by mlimbwa1977, Jun 12, 2011.

 1. m

  mlimbwa1977 Member

  #1
  Jun 12, 2011
  Joined: Feb 7, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ninavyoelemwa mimi chombo cha umma lazima kitumike kwa maslahi ya wote.TBC1 inaendeshwa kwa kodi za watanzania wote,kwanini inashindwa kuwapa furaha wapenzi wa mpira wa miguu kote nchini kupitia television yao? Sidhani kama suala la kusubiri wadhamini ndipo mchezo uonyeshwe kama ni haki kwa watanzania.udhamini ni muhimu kwa vyombo binafsi vinavyojiendesha kwa kuangalia faida zaidi.

  TBC1 ni Television inayojiendesha kibiashara lakini inapewa ruzuku kutoka serikalini,hakuna sababu washindwe kutuonyesha walau inapocheza timu ya taifa.Kama TIdo Mhando aliweza kwanini waliopo sasa washindwe? Viongozi wa sasa lazima muwe na uzalendo kwa nchi yenu,leo mpo hapo kesho watakuja wengine, lazima mjijengee heshima kwa jamii ili mkumbukwe kwa mema yenu,vinginevyo mtazomewa mtakapokuwa nje ya vyeo vyenu.

  Naomba majibu kutoka uongozi wa TBC1 ili watanzania tuelewe kinachowakwaza labda tutaacha kuwalaumu.
   
 2. m

  mbongopopo JF-Expert Member

  #2
  Jun 13, 2011
  Joined: Jan 24, 2008
  Messages: 1,113
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Labda hawana hati za kurusha michezo hiyo mie sielewi sana kuonyesha michezo kwenye tv ila najua ni lazima kununua haki kuonyesha michezo hawawezi kurusha tu esp kama kuna channel ingine/zingine zimenunua hiyo.
  I guess tz ni sawa tu na nchi nyingi zaidi duniani
   
 3. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #3
  Jun 13, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 827
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kwasababu hawana mkataba wa kuonyesha mechi hizo! Kwisha!!
   
Loading...