Shebbydo
JF-Expert Member
- Feb 12, 2015
- 1,174
- 1,937
Habari wakuu,
Mnamo mwaka 2011 serikali ya mheshimiwa Kikwete kupitia Wizara ya elimu wakiwakilishwa na taasisi ya elimu ya juu, iliamua kupunguza vigezo vya udahili wa wanafunzi wa elimu ya juu. Hii ilitokana na mtazamo wa kutaka kuongeza wigo wa Watanzania wengi kupata elimu ya chuo kikuu ambayo itawasaidia katika "mapambano dhidi ya mazingira"(struggle against nature).
Mnamo mwaka 2014 Baraza la mitihani la Taifa walianza kuhangaika na upangaji madaraja ya ufaulu bila sababu ya msingi. Hivi mwaka huu baraza limekuja na upangaji mpya wa viwango vya ufaulu. Katika viwango hivi vipya hasa kwa kidato cha sita kuna; A,B+,B,C,D na S. Kwa maana hiyo A=5, B+ =4, B=3,C=2,D=1,S=0.5.
Jana tume ya vyuo vikuu (TCU) wametoa taarifa ya mabadiliko ya viwango vya udahili katika taasisi za elimu ya juu. TCU wamegawanya katika mafungu matatu; Wa kabla ya mwaka 2014, wa mwaka 2014 na 2015 na wa mwaka 2016 na kuendelea. Vigezo vya mwaka 2016 TCU wanasema ili mtu adahiliwe lazima awe na pointi 4 ambazo wao wanasema ni D mbili. Kwa mujibu wa TCU wao wamekuwa tofauti na baraza la mitihani kwa kuwa wao wamepanga hivi ; D=2 na E=1. Je, TCU hiyo E wameitoa wapi? Mbona kwa mujibu wa NECTA D=1?
Kwa nini hizi taasisi mbili zinatofautiana, au hawashirikiani? Rai yangu kwa serikali hii, isiwaone watu wa serikali iliyopita kuwa wote hawakuwa na weledi kwani kwa kufanya hivyo watavuruga kila kitu na kujikuta huko mbele wanakwama.
Serikali hii imekuja na mkakati wa kupunguza idadi ya watu wanaodahiliwa elimu ya juu, mimi sidhani kama wazo zuri kwa kuwa tutakuwa tunarudi tulikotoka.