Kwa nini Simu za Viganjani Huzuiwa Mashuleni TZ?

Simu za viganjani ziendelee kuzuiwa au ziruhusiwe kwa wanafunzi wa mashule ya Tanzania?

  • Ndio -- Ziendelee kuzuiwa

    Votes: 5 55.6%
  • Hapana -- Ni mawazo ya kijima kuzuia simu za viganjani karne hii ya 21

    Votes: 4 44.4%

  • Total voters
    9

Mlenge

R I P
Oct 31, 2006
2,125
2,291
Lengo la shule ni kumuandaa mwanafunzi aweze kuyakabili mazingira yake pindi amalizapo shule. Mazingira ya siku hizi ni pamoja na simu za viganjani. Ni kwa nini basi mashule mengi ya Tanzania simu za viganjani ni verboten?

Kwenye mashule mengi mwanafunzi kukutwa na simu ni kosa la kufukuzwa shule papohapo. Kwa nini?

Shule za nchi nyingine wanaruhusu wanafunzi wao kwenda na simu za viganjani, lakini wanawapa masharti ya kuzitumia wawapo shuleni. Wanafunzi wa mashule yetu wataweza kushindana na wa mashule hayo kwa usawa?

Simu za viganjani ziendelee kuzuiwa au ziruhusiwe kwa wanafunzi wa mashule ya Tanzania?

Mifano ya shule zinazoruhusu matumizi ya simu:

Willunga High School :: Mobile Phone Policy

Mobile Phone Policy

Mobile Phone Policy – Darwen Vale High School
 
Mbona hapa Arusha kuna shule wanafunzi simu wanazo? Au umelenga shule za gvt tu?
 
Shule za binafsi na za serikali. Mashule gani yanayoruhusu matumizi ya simu huko Arusha?
Siwezi kuandika hapa ila kuna shule zipo na sio kwamba kuna total ban kutumia ila kuna mda wanaruhusiwa.
Kwani mkuu ulipotaka kuandika hukufanya utafiti wa kina kujua shule zote , au ulichukulia kama shule zote za gvt? Anyway njoo ufanye utafiti kidogo utagundua.
NB: hazitumiki darasani mwalimu akifundisha, la hasha ila kuna mda wa kuzishika
 
Kwa kushuka huku kwa maadili kutokana na uangalizi/malezi hafifu wa wazazi/walezi ni bora wasitumie tu.
 
Lengo la shule ni kumuandaa mwanafunzi aweze kuyakabili mazingira yake pindi amalizapo shule. Mazingira ya siku hizi ni pamoja na simu za viganjani. Ni kwa nini basi mashule mengi ya Tanzania simu za viganjani ni verboten?

Kwenye mashule mengi mwanafunzi kukutwa na simu ni kosa la kufukuzwa shule papohapo. Kwa nini?

Shule za nchi nyingine wanaruhusu wanafunzi wao kwenda na simu za viganjani, lakini wanawapa masharti ya kuzitumia wawapo shuleni. Wanafunzi wa mashule yetu wataweza kushindana na wa mashule hayo kwa usawa?

Simu za viganjani ziendelee kuzuiwa au ziruhusiwe kwa wanafunzi wa mashule ya Tanzania?

Mifano ya shule zinazoruhusu matumizi ya simu:

Willunga High School :: Mobile Phone Policy

Mobile Phone Policy

Mobile Phone Policy – Darwen Vale High School
Wanaruhusu za mezani?
 
Kwa kushuka huku kwa maadili kutokana na uangalizi/malezi hafifu wa wazazi/walezi ni bora wasitumie tu.
Pamoja na kuzuiwa ila jahazi la naadili linashuka kwa kuwa wakirudi nyumbani wanazo na baadhi huwa nazo bila wazazi kujua. " There is no significant correlation between mobile phone use for students and moral decay amongst them"
 
Shuleni kipaumbele ni kufundisha maadili?!
 
Back
Top Bottom